June 15, 2012

KAULI YA KWANZA YA DOGO JANJA BAADA YA KURUDISHWA KWAO NA MADEE.




Kama ulipitwa na hii stori ni kwamba msanii Madee wa TipTop Connection ambae ndio alikabidhiwa kumlea Dogo Janja na kumsimamia kwenye muziki alitangaza juzi kwamba amemrudisha Dogo Janja kwenye mikono ya wazazi wake baada ya kuona muelekeo wa Janja sio mzuri kitabia.
Alisema kwanza Janja alikua mtoro wa shule na mara kadhaa hakwenda shule na alikua akimdanganya, aliwahi kumkuta anaogoelea Ubungo Plaza wakati wenzake wako shule, amekuta msg za matusi ambazo Dogo Janja aliwatumia watu wengine kuhusu Madee na makosa mengine kadhaa.
Dogo Janja ambae sasa hivi karudi Arusha tayari amefunguka kila kitu katika Interview ya Dakika 40 Exclusive on millardayo.com na yafuatayo hapo chini ni baadhi ya mambo aliyoyazungumza.
Amesema “kwanza napenda watanzania wajue kwamba mimi nilikua siishi na Madee nilikua naishi na rafiki yake ambae ni Abdallah Doka Kimara jirani na Madee, Madee alikua haniangalii kwa chochote na niliweka kikao juzi kati tu hapa nilikua nataka nirudi kwetu, kula ni Doka, kuvaa Doka, Hela ya Shule Doka…. ninavyoongea hapa Dogo Janja sijawahi kulipwa hela zaidi ya laki tatu kwenye show, Tanzania hii nimeshaizunguka ujue alafu sioni faida yake nakwenda kwenye show nikirudi napewa laki moja alafu ukiuliza mtu anaweza kukununia sasa nikawa zinanikera lakini nikawa nashindwa kuongea sababu ndio niko pale kwa ajili ninasoma”

KUHUSU ACCOUNT YANGU BANK:
 “Madee alininyang’anya mpaka kadi yangu ya ATM yani mimi narudi Arusha ni kama nakwenda kuanza maisha mapya hamna ambacho useme labda narudi Arusha ni kama vile nakwenda kuanza maisha mapya hamna ambacho useme labda naweza kurudi Arusha labda kwenye account sijui nina shilingi ngapi, kachukua hela zangu zote kwenye account yani, mi nilikua namuona mwema ananijali aliniambia nenda kafungue account na kiuaminifu pale unatakiwa kuandia namba zako mimi sikuandika zangu nikaandika za Madee, taarifa yoyote ya bank inakutana na Madee, mi siwezi kumtusi yule nitakua namkosea sana hata akinipa radhi inaweza kunipata mi naongea kilicho moyoni mwangu mpaka nimechukua hatua hii”

KURUDISHWA KWANGU ADA SHULENI NA KIWANGO CHA PESA BANK
“Na jina lote hili Dogo Janja nilikua narudishwa ada nyumbani, nikachukua hatua nikaenda kufanya show ile hela yangu ya show baada ya kurudi nakumbuka alitoa laki mbili na 60, hela ilikua yangu akaniambia… Ahh Janja hapa sina hela nyingine nenda katoe kwenye account nitakurudishia.. ni brother alafu mi namuheshimu sana, kadi yangu ya bank yeye ndio alikua anaizuia lakini mwisho wa siku nakuja kuangalia account yangu, mbona account haisomi? na kadi yangu yeye ndio alikua nayo… Millard nakwambia ukweli wa mwenyenzi Mungu mimi account yangu haikuwahi kufikisha shilingi milioni moja na kila show ninayofanya nalipwa shilingi milioni moja, naongea mbele za mwenyenzi Mungu mimi mtoto wa kiislamu naitwa Abdulaziz”

KUHUSU SHOW YA MWISHO KUIFANYA KABLA YA YEYE KUNIPIGA: 
 Madee alinipigia simu jumapili akiwa Iringa ambapo jumanne wenzangu walikua wanaanza mtihani,nilimwambia niko na Hassan nyumbani kwa Tunda akasema ana kaka yake Kibaha alikua na show ya CCM alikua anamtaka lakini akaona hawezi na analove na bro akashindwa kukataa, roho ilikua inaniuma mimi hapa mimi nakwenda kufanya show kwa laki moja… alafu hapo niko na backup wangu nimempa elfu 20 mi nikabaki na elfu 80 alafu hiyo 80 anakupigia….  wee sikia elfu 50 hiyo kaweke bank, elfu 50 tumia…. mi nikafanya kipeace tu nikaenda kwenye show huyo brother wake kachelewa kuturudisha hapa saa saba usiku kwa sababu ujue mimi sina usafiri na yule jamaa alikua anasubiri mishe zake zote zikamilike alafu asubuhi nilikua natakiwa kuingia shule, kosa sio langu ni la huyo kaka yake Madee.. sikwenda shule jumatatu sababu nilichelewa.. hivi hata wewe Millard unaweza kulala saa saba ukaamka saa kumi??????! hiyo siku ndio nilitakiwa kwenda kuchukua namba ya mtihani nikapangwe la dawati langu ili jumanne nifanye mtihani, nilipoona nimechoka nilimpigia mwalimu wa Darasa nikamwambia siwezi kwenda shule jumatatu akaniambia hamna neno mi nikienda jumanne siku ya mtihani niende asubuhi nitapata”

JINSI MADEE ALIVYONIPIGA:  
Nilikua nyumbani kwa Tunda Man na Hassan ambae aliniacha baada ya kutumwa, nimekaa kidogo natoka hivi nakutana na Madee geitini hajaniuliza chochote zaidi ya kuanza kunipig, kanichezeshea mikono kanipiga makofi alafu kanidhalilisha yani mtaa mzima umekusanyana pale kwa Tunda Man, t shirt ilichanika na akanikatalia kupanda kwenye gari… roho iliniuma palepale alafu alivyonikatalia kupanda kwenye gari huku akiniambia anikute nyumbani baada ya dakika tano, roho iliniuma nikasema haya yote nayapata kwa sababu mimi ndio nataka na napenda muziki na napenda baadae niwe na maisha bora, niliongea na wazazi wakaniambia nivumilie lakini kiukweli nikasema siwezi tena kuishi Dar es salaam na leo June 13 2012 ndio siku ya mwisho kuishi Dar es salaam hapa ninavyoongea, jioni niliitisha kikao nikampigia Doka, Madee, na kaka yangu huyu nikaulizwa labda kuna kitu Madee hanifanyii mi nikashindwa kuongea nikasema bwana mimi sitaki chochote mi nirudisheni kwetu ujue Millard mpaka mimi nachukua maamuzi haya kwamba naomba nirudishwe kwetu, nimeomba nirudi kiroho safi tu lakini nashangaa yeye anapokwenda kuongea mambo mengine kwenye media, mi namshangaa yule ni mtu mzima anajielewa ujue, sasa mimi sijui kwa nini amekua hivyo”

KUHUSU MADEE KUMUOMBA BABA YANGU ANIAMBIE NISIONGEE CHOCHOTE KWENYE MEDIA: “Alimpigia simu baba ya kumuomba nisizungumze chochote kwenye media akidai kwamba itakua aibu kwangu na kwake, mimi niko hewani lakini hakunipigia.. baadae nikapata simu kutoka kwa bro akaniambia niongee na mama nilipoongea nae akaniambia Madee kasema nisiseme chochote kwenye radio, sasa imefika jioni nikashangaa nikamsikia sasa nikajiuliza kwa nini kaongea? na mimi siwezi kumpigia yule simu yani nimeshaapia kwa mwenyeenzi Mungu siwezi kumpigia simu.
KUHUSU MIMI KUACHA MUZIKI: “Roho inaniuma kichizi nimeona hiviii, yani huu mziki huu kwa sababu haunisaidii chochote, mimi narudi Arusha ni kama narudi tena kuanza maisha mapya kwa hiyo mimi nimeona bora tu kama inawezekana huu muziki naweza kuacha na nitaishi kama zamani kwa sababu kwetu sijaua, nimeona bora nitulie nyumbani ujue mpaka Millard pale nimeomba kabisa jamani Eeehe nirudisheni nyumbani kwetu, nasema Inshallaah mwenyeenzi Mungu yupo na mimi na riziki hapangi Madee riziki anapanga Mungu”
KUHUSU KUSOMA DAR ES SALAAM: “Sitaki kabisa kusoma Dar es salaam mimi nakwenda kusoma Arusha au mkoa wowote sitaki tena.
Hiyo ni sehemu tu alichokisema Dogo Janja kuhusu yeye kuondoka kuwa chini ya Madee na kurudi nyumbani kwao Arusha, mengine utaendelea kuyasikia kupitia AMPLIFAYA ya CLOUDS FM leo saa moja usiku na pia hapa millardayo.com! kuna picha za hizo msg pamoja na msg ya mwisho Janja kumtumia 

 Source- millardayo.com


June 14, 2012

UNAJUA DOGO JANJA ALICHOKISEMA /KUFUNGUKA KUHUSU YEYE KUTEMANA NA TIP TOP? UKWELI HUU HAPA

Dogo Janja & Nass


Siku moja baada ya Dogo Janja kudaiwa kufukuzwa Tip Top Connection, ukweli halisi kuhusiana na uamuzi huo umewekwa wazi na yeye mwenyewe.Sababu zilizotajwa na Tip Top Connection ni kwamba Dogo Janja alilewa sifa na kuwa mtoro shuleni.

Kwa mujibu wa interview (ya pili kufanyiwa baada ya kipindi cha Amplifaya cha jana) tuliyofanya naye kwa simu saa moja asubuhi leo (June 14) akiwa stand kurejea nyumbani, uonevu na dhuluma ndivyo vilivyomchosha kuishi Dar es Salaam.

Anasema tangu aje Dar es Salaam hajawahi kusaidiwa chochote na Madee zaidi ya mambo ya muziki pekee huku kula, malazi na ada ya shule vikifanywa na rafiki yake Madee aitwaye Abdallah Doka ambaye (Dogo Janja) alikuwa akiishi kwake.

Anasema kutokana na ngoma zake kujipatia umaarufu alikuwa akipata show nyingi nchini na zote alikuwa halipwi chini ya milioni moja.Kilichokuwa kinamsikitisha anasema ni kulipwa hela kidogo isiyozidi laki mbili na hivyo kumfanya aishi kwa tabu licha ya kuingiza hela nyingi za show.

“Nilikuwa navumilia tu bro kwasababu kila nilipolalamika kuhusu mambo ya hela Madee alikuwa mkali sana,” ameongea uchungu.

Dogo anasema ilikuwa inafikia wakati akifanya show za ukumbuni hulipwa elfu hamsini au chini ya hapo na wakati mwingine alikuwa halipwi kabisa.Tamaa ilizidi kumwingia Madee kiasi cha kumnyang’anya kadi yake ya benki na kuanza kuchukua hela bila kujua password aliipata wapi.

“Kuna wakati nilikuwa nataka kumtumia mama laki moja, Madee akanikataza eti kwakuwa watadhani nina hela sana,” anasema.Mpaka tunaongea naye asubuhi hii, anasema kadi yake imebakiwa na shilingi 25,000 tu.

Ameendelea kudai kuwa juzi Madee alimpigia simu na kumwambia kuwa kaka yake wa Kibaha ameandaa show ya CCM na atamlipa shilingi laki moja.

“Hivi kweli bro mimi ni mtu wa kufanya show ya laki moja?”. Hata hivyo aliamua kukubali ili kuepusha lawama.
Baada ya show kumalizika anasema yeye na back up artist wake walirudishwa saa saba usiku wakati asubuhi yake alitakiwa kwenda shuleni kuchukua namba ya mtihani na kuandaa dawati la kukalia.

Dogo Janja anaeleza kuwa inamuuma sana kwakuwa muziki haujampa chochote licha ya Madee ambaye huwa hapati hata show kumtumia kimaslahi na hadi leo hii anamalizia kujenga nyumba yake.

“Ni kama vile Madee alinipanda ili anivune.”
Ameendelea kusema kuwa hiyo juzi sasa hadi kufikia Tip Top watangaze kumfukuza alikuwa kwa Tundaman akipiga story na Madee akamuita kisha kuanza kumpiga. Alichukua simu yake akaondoka nayo. “Jamaa alianza kujitumia meseji kutoka kwenye simu yangu kwenda kwake za matusi ama kuwa nataka kumroga. Jana nimemuonesha Milard hizo meseji na amesikitika sana.” Anasema simu yake alipewa jana.

Kitendo cha kumwambia Madee kuwa amechoka na anataka kurudi nyumbani ndicho kimemfanya amfanyie yote hayo hadi kumwambia kuwa watahakikisha wanambania asifanye vizuri tena kwenye muziki. Pia amedai kuwa Madee aliwapigia simu wazazi wake ili wamkataze Dogo Janja asifanye interview na vyombo vya habari.

“Wanajua nikiongea wataabika sana.”

Story By Nass

May 6, 2012

HIVI NDIVYO SIMBA SC ILIVYO IFANYIZIA YANGA YA JANGWANI

Waziri wa Habazri, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk Fenela Mkangara akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya Simba Juma K. Juma baada ya timu ya Simba kuifunga Yanga magoli 5-0 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar salaam katika mchezo uliokuwa ni wa  kumaliza michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom uliomalizika jioni hii  kwenye uwanja wa Taifa, huku ikiwa tayari ni mabingwa wapya wa ligi hiyo, Simba imefanikiwa kutunza heshima yake baada ya kuifunga Yanga magoli 5 kupitia wachezaji wake Emmanuel Okwi, goli la kwanza. 

Goli la pili la Simba likafungwa na mchezaji Felix Sunzu kwa njia ya penati na dakika chache baadae Emmanuel Okwi akaongeza goli la tatu , Juma Kaseja akaongeza goli la nne kwa penati wakati pia Patrick Mafisango akafunga hesabu kwa kufunga  goli la tano baada ya wachezaji wa Yanga kufanya makosa katika eneo la hatari 



Nyomi ya Mashabiki wa Simba Wakifatilia Mechi Kwa Uzuri Kabisa

Kipindi Cha Kwanza Ubao Ulisomeka Kama inavyoonekana Hapo Juu


Kikosi Cha Simba Kabla Ya Mechi




Picha Kwa Hisani Ya Shafii Dauda

"NEW FLAVA" KUTOKA KWA HONCHO STOPA (YOKOI) KUTOKA MUDA WOTE KUANZIA SASA.


Mkali wa Hip Hop with crazy flow, style 3 and Boom bye bye Emcee, Stopa Tha Rhymecca anategemea kudondosha mpini wake mpya baada ya Boom bye bye, Ngoma hiyo mpya inaitwa "New Flava" touches za mtayarishaji wa mapigo ya muziki Tanzania "Q The Don" kutoka ndani ya studio za Mo Records ya jijini Mwanza, Stay tayari kwa New Flava kutoka kwa Stopa Tha Rhymecca time yeyote mzigo hewani paaaaaah! Hapo Stopa yupo na mtoto wake anaeitwa "Jenel"...Babe gal.

May 2, 2012

PHOTOS: DIAMOND ALIVYOWEKA HISTORIA DAR LIVE…!!

Mashabiki wakiwa na mzuka wakumpokea Raisi wa Wasafi Diamond

Nyomi yakutosha katika viwanja vya dar Live Mbagala

Diamond Akiwapa Burudani Mashabiki wake .....


Pamoja na mvua kunyesha, mzuka uko palepale.

Diamond

Diamond Platnum akiwa na Rubani wake wakielekea kwenye chopper.

Diamond Akisali Kabla Myama Hajapaa Angani

Akitoa saluti kabla ya kupasua anga.



Huu ndio uwanja wa Dar Live Ukionekana Kwa Juu

April 29, 2012

WARAKA WA “RAY” KUHUSIANA NA MAREHEMU “STEVEN KANUMBA”…!!

Yapata wiki tatu sasa tangu msanii mwenzangu Steven Kanumba aage dunia, na kama ilivyo kwa kila kitu kinapotokea huandamana na kila aina ya maneno na hisia mbali mbali kutokana na mitazamo ya watu kupishana kuhusiana na jambo husika. Kulingana na muktadha huo, msiba wa Steven Kanumba umekumbwa na maneno na hisia kama hizo,hususan mazingira ya kifo chake; kinachosikitisha zaidi watu wengi (ambao wanajitambulisha kama wapenzi wa Kanumba), na baadhi ya vyombo binafsi vya habari vimekuwa vikinihusisha na kifo hicho, kwa kusema kwamba kwa njia moja au nyingine ninahusika na mauaji ya Steven Kanumba.

Kwa muda wote huo tangu msiba ulipotokea mpaka leo hii nashika kalamu kujaribu kuyaweka sawa na kuondosha hisia chafu katika fikra za watu, nimekuwa nikipitia katika wakati mgumu sana kwa jinsi ambavyo nimekuwa nikinyooshewa vidole kila upande nikihusishwa na kifo hicho, kiujumla nimezingatia maoni ya wapenzi ya mashabiki wangu wakinitaka kuwa na subira, ila kuna ukweli usemao kwamba, uongo ukirudiwa sana jamii huusadiki na kuuona ukweli,nimeona nisikae kimya ila niweke sawa hili kwamba sihusiki na kifo cha Steven Kanumba.

Nasema wazi kwanza sihusiki kabisa na kifo cha Kanumba kwanza kwa kuzingatia mazingira yenyewe ya kifo kilivyotokea. Wakati kifo hicho kinatokea, nilikuwa sehemu nyingine kabisa na mimi nilikuwa mtu wa tatu kutaarifiwa kwamba Kanumba amepatwa na mkasa ambao baadae ulisababisha kifo chake. Na na hata nilipofika katika hospitali ya Muhimbili (tofauti na watu wanavyodhani kuwa nilifika nyumbani kwake; ukweli mimi nilimkuta tayari amepelekwa Muhimbili), nilikuta tayari alikuwa ameshafariki ndio maana hata Polisi wanaohusika na usalama wa raia, si tu kwamba hawakuniweka chini ya ulinzi, sikuitwa hata kuhojiwa kwa sababu hakuna mazingira yoyote yanayonihusisha mimi na kifo hicho.

Pili, watu wanahusisha tofauti za kibinadamu zilizokuwepo baina yetu na kifo hicho, nasema hii sio sahihi kwa sababu kwanza ni kawaida kwa binadamu kutofautiana,isipokuwa kwetu sisi baadhi ya vyombo vya habari vilikuwa vinakuza kwa sababu nisizozijua, hivyo jamii ikachukulia kuwa tofauti zile ni uadui kitu ambacho sio sahihi, kwani sisi hatukuwa watu pekee tunaotofautiana kwani huu ni mwenendo wa kawaida wa dunia; hivi jana tumeshuhudia Waziri mmoja akieleza bayana katika mkutano na waandishi wa habari kuwa na tofauti na naibu wake, lakini hatuajasikia ikiandikwa wana ‘bifu’ bali imetafutwa lugha nzuri ya kupamba tofauti hizo, kwa kuwa waliohusika ni waheshimiwa, ila kwa wengine kutokana na sababu tusizozijua, inaonekana kama ni haki yetu kuandikwa vibaya. Kinachosikitisha, kwa nini jambo hili linachukuliwa kwa mkazo mkubwa sana, kwani hatujawahi kusikia watu wakiwa wanatofautiana na ndugu jamaa hata na marafiki zao na inaonekana kawaida tu? Kwani vyombo vya habari havikuwahi kuandika kuwa marehemu Steven Kanumba alikuwa na tofauti na baba yake, na yeye mwenyewe alitamka hivyo katika vyombo vya habari, mbona wameliongea bila kuongeza chumvi, na jamii inaona kuwa ni jambo la kawaida la kibinadamu.

Pengine watu wanaojaribu kuongea hayo, hawajui mimi na Steven Kanumba tumetoka wapi? Sisi si watu tuliokutana barabarani, tuna historia katika kazi yetu ya sanaa na pia katika maisha maisha yetu. Mwanzoni kabisa, mimi ndiye niliyempokea Kanumba pale Kaole na ndiye niliyemfundisha sanaa pale (nadhani watu wanakumbuka tamthiliya za wakati huo ITV) na baada ya hapo tulienda pamoja katika kampuni ya Game 1st Quality pamoja na tukafanya filamu kama Johari, ‘Sikitiko Langu’, ‘Dangerous Desire’ na nyinginezo, na tuliendelea kuwa pamoja katika kampuni hiyo mpaka tulipofanya filamu ya ‘Oprah’ mwaka 2008 ambapo niliingia rasmi kufanya kazi za kampuni yangu, lakini tuliendelea kuwa pamoja hata wakati nikiendelea na kazi za kampuni yangu.

Pia mimi nilikuwa wa kwanza kuanza kufanya kazi na Steps na baadae Kanumba alipoanza kufanya kazi zake mwenyewe na kunikuta huko tuliendelea kuwa pamoja kama siku zote. Kitu kikubwa kilichokuwa kinaendelea baina yetu, ni kwamba tulijenga ushindani wa kuendeleza kazi mbele kwa kila mmoja akitoa kazi, mwingine anamjibu.

Isitoshe hata vitu vyetu binafsi utaona kama kuna kufanana; kuna wakati Kanumba alinunua Toyota Ruv 4 nyeusi mimi nikanunua ya kijani, aliponunua Harrier na mimi nikanunua pia, na hata gari za hivi karibuni, ukitazama utaona kuwa zinafana kwa karibu; hii ilikuwa ni kama maisha yetu, hatukuwa na uadui, ilikuwa tunapeana changamoto za maendeleo.

Watu wanaojaribu kuonesha kuwa tofauti zetu ilikuwa ni uadui, huwa hawajui wapi tulikotoka ndio maana wanasema wasemavyo na katika kuthibitisha kuwa tofauti hizo hazikufikia katika uadui, kuna watu ambao wanafanya kazi nami katika kampuni yangu ya RJ ndio hao hao Kanumba alikuwa anawatumia siku zote katika kazi zake, hata baada ya tofauti hizo hakuna aliyekoma kufanya kazi na yeyote kati yetu.

Hii inathibitisha kuwa tofauti ilikuwa kati yetu kama binadamu, sio chuki za kimafanikio, ingekuwa hivyo watu kama Junior Syaary ambaye mara nyingi hufanya final editing katika RJ ndio huyo huyo alikuwa akifanya na Kanumba, Ally Yakuti ambaye anaandika script za RJ, ndiye huyo huyo aliyekuwa anaandika kwa Kanumba, Steven Shoo ambaye ni mtaalamu wangu wa light, ndiye huyo huyo anayetumiwa na Kanumba na wengine wengi kama Juma Chikoka aliyecheza kikamilifu katika filamu ya ‘Kijiji cha Tambua Haki’, ambaye pia anashiriki filamu nyingi za RJ, na wote hao, hawakuanzia kwa Kanumba, wote wameanza kwangu mimi ndio niliompatia na hata baada ya hayo yanayosemwa kuwa kuwa ni uadui, sikuwahi kuwakataza kufanya kazi na Kanumba.

Tatu kumtuhumu mtu kwa namna yoyote ile bila ya uthibitisho wa tuhuma hizo, ni kosa kwa sheria za nchi na pia kama ni mfuasi wa dini yoyote ni dhambi, kwani wakati ukisema hayo huku hujui uhalisia bali unasukumwa na nguvu za hisia tu ni sawa na kumchafua mtu huyo katika jamii bila ya kujua jamii inamchukuliaje. Napenda kusema wazi wazi kuwa, kwa kila anayetekwa na wimbi hili, ajaribu kufikiria leo ipo kwangu mimi, kesho inaweza kuhamia kwako, kwani mimi sio wa kwanza kufikwa na haya, inaweza kukukuta hata wewe au ndugu yako, utajisikiaje.

Na kama kweli mimi nimehusika na kifo cha Kanumba kwa namna yoyote ile, basi Mungu atanihukumu na kila aliye hai atashuhudia, ila kama sijahusika kwa lolote, Mungu hatonihukumu na badala yake ataniinua, kwa kuwa ninapita katika kipindi kigumu mno sasa hivi kwa madhila haya.

Mwisho kabisa napenda kumaliza kwa msemo usemao, ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke, kwani kadri mambo haya yanavyoendelea, usidhani yataishia kwangu, kwani mkono wa dhuluma haushii karibu, ukisikia jirani anapiga kelele za mwizi, usilale kamsaidie, usiseme kuwa hatuhusiki kwani hayupo kwetu, kesho utafikwa na wewe utakosa wa kukusaidia. cha msingi kama tunampenda sana ndugu yetu ni kumuombea kwa Mungu, kwani hatujui makao yake huko aliko, na sio kuunda vitu ambavyo kamwe hata yeye angekuwa hai asingeviafiki.”

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU STEVEN KANUMBA MAHALI PEMA PEPONI.

MUNGU IBARIKI AFRIKA MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Gwaii - Kazaa Kamua



 
Here is a clip shot of Gwaii’s “Kazaa Kamua” from his Thymuzik EP. The Official Music Video will be released in a few weeks from the people to enjoy it. shortly after that he will be releasing his official single from the upcoming album as well.

You can follow Gwaii on twitter @GwaiiThyword and also like him on facebook: http://www.facebook.com/gwaiimusic Gwaii’s EP is available on itunes, “Thymuzik” CDbaby and Amazon now!!

AACUSA - Proud To Be (Official Music Video HD)


African Artist Coalition USA (AACUSA) was formed with two goals in mind – promoting and exposing African arts and culture to the global/mainstream market, and creating a central platform that would showcase the arts and culture. With that vision in mind we created the PROUD TO BE project (P2B Project) to jump start our efforts towards achieving these goals.

This project brings together African artists who live in the USA for a joint project that represents African pride – proud of who we are in spite of our struggles, celebrating our accomplishments and looking forward to the journey ahead. This will involve a group of like minded young people and those young in heart, that love who they are and are ready to share this with the world.

Though there many reasons that motivated us to give birth to AACUSA, including addressing and providing aid to social, political and economical struggles that African is experiencing, we hope to shine a light to our culture and welcome all to embrace it. We also intend close the generational gap or the disconnect that exists between the young generation and that of Africa’s decision makers for a brighter future for all. Together we can be the change that Africa desires and deserves.

aacusa.net

Directed By: Dallas, Henry, & John
Shot by: Dallas, Henry, & John
Artists: Proud 2B African.
Song: Co-written by John Mahundi, Webiro Wassira & Lambert Tibaigana


ROMA MKATOLIKI KUYAWEKA MAISHA YAKE YA MZIKI KWENYE DOCUMENTARY YAKE MPYA.

Msanii anayeiwakilisha TANGA katika bongo fleva ROMA, baada ya kuchukua tuzo mbili za Kilimanjaro kama Msanii bora wa Hip Hop na wimbo wake Mathematics kuchukua kama wimbo bora wa Hip Hip hivi sasa anatengeneza Documentary yake inayoeleza maisha yake kimuziki toka alivyoanza mziki shida alizopitia mpaka kufikia hivi sasa alipofikia. 
Roma akiwa katika studio ya Tongwe Rec akiitengeneza DVD hiyo ambayo amesema nimapema sana kusema itatoka lini ila haitochelewa kutoka na anaamini watu wataipenda na italeta utofauti kidogo maana story iliyomo ndani ya Documentary hiyo iko kitofauti na itamgusa kila mmoja.

April 15, 2012

WASHINDI WA KILIMANJARO MUSIC AWARD WAPATIKA 2012


Hawa ndio washereheshaji  wa shughuli nzima Kushoto ni Milard Ayo Na Mwana dafada Vanessa Mdee

Mwakilishi wa kundi la Arusha Gold Akipokea Tuzo wimbo Bora wa Ragga

Baada ya Shughuli nzima kutia nanga Maojiano yaliendelea na waandishi mbali mbali wa Habari Ndani ya Ukumbi  







 Diamond & Ommy Dimpoz
  Mchekeshaji Kutoka Kundi la Ze Comrdy Mpoki Akitambulisha moja ya kikundi    

MPAKA MWISHO WA MCHAKATO WASHINDI WA TUZO ZA KILI MUSIC AWARDS WALIPATIKANA.

1. WIMBO BORA WA RAGGAE.
-ARUSHA GOLD BY WARRIORS FROM EAST.

2. WIMBO BORA WA DANCE HALL.
- MANENO MANENO BY QUEEN DARLIN.

3. WIMBO BORA WA ZOUK RHUMBA.
- DUSHELELE BY ALI KIBA.

4.BORA WENYE VIONJO VYA KIASILI.
- VIFUU UTUNDU BY A.T-

5. WIMBO BORA WA TAARABU.
- NANI KAMA MAMA BY MASHAUZI CLASSIC ( AISHA MASHAUZI).

6. WIMBO BORA WA KISWAHILI.
- DUNIA DARAJA BY TWANGA PEPETA-

7. WIMBO BORA WA AFRO POP.
- HAKUNAGA BY SUMA LEE-

8. WIMBO BORA WA R&B.
- NUMBER ONE FAN BY BEN PAUL-

9. WIMBO BORA WA HIP HOP.
- MATHEMATICS BY ROMA-

10. MSANII BORA ANAECHIPUKIA.
- OMMY DIMPOZ (NAI NAI SINGER).

11. RAPA BORA WA BAND.
- KALIJO KITOKOLOLO-

12. MSANII BORA WA HIP HOP.
- ROMA MKATOLIKI-

13. WIMBO BORA WA KUSHIRIKISHWA.
 - NAI NAI BY OMMY DIMPOZ FT. ALI KIBA-

14. WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI.
-KIGEUGEU BY JAGUAR-

15. MTUMBWIZAJI BORA WA KIKE.
- KHADIJA KOPA-

17. MTUNZI BORA WA MWAKA.
    - DIAMOND-

16. MTUMBWIZAJI BORA WA KIUME
- DIAMOND-

18. MTAYARISHAJI BORA WA MAPIGO YA MUZIKI.
- MANEKE-

19. VIDEO BORA YA MWAKA.
- MAWAZO BY DIAMOND-

20. WIMBO BORA WA MWAKA.
- HAKUNAGA BY SUMA LEE-

21. HALL OF FAME.
     -  TAASISI JKT-

22. HALL OF FAME KWA MTU BINAFSI.
      - KING KIKII-

23. HALL OF FAME KWA MTU BINAFSI.
     - DR. REMMY ONGALA-

24. MWIMBAJI BORA WA KIKE.
     - LADY JAY DEE-

25. MWIMBAJI BORA WA KIUME.
      - BARNABA-