Waziri wa Habazri, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk Fenela Mkangara
akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya Simba Juma K. Juma baada ya timu ya
Simba kuifunga Yanga magoli 5-0 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar
salaam katika mchezo uliokuwa ni wa kumaliza michuano ya Ligi Kuu ya
Vodacom uliomalizika jioni hii kwenye uwanja wa Taifa, huku ikiwa
tayari ni mabingwa wapya wa ligi hiyo, Simba imefanikiwa kutunza
heshima yake baada ya kuifunga Yanga magoli 5 kupitia wachezaji wake
Emmanuel Okwi, goli la kwanza.
Goli la pili la Simba likafungwa na mchezaji Felix Sunzu kwa njia ya
penati na dakika chache baadae Emmanuel Okwi akaongeza goli la tatu ,
Juma Kaseja akaongeza goli la nne kwa penati wakati pia Patrick
Mafisango akafunga hesabu kwa kufunga goli la tano baada ya wachezaji
wa Yanga kufanya makosa katika eneo la hatari
|
No comments:
Post a Comment