Kama ulipitwa na hii
stori ni kwamba msanii Madee wa TipTop Connection ambae ndio alikabidhiwa
kumlea Dogo Janja na kumsimamia kwenye muziki alitangaza juzi kwamba
amemrudisha Dogo Janja kwenye mikono ya wazazi wake baada ya kuona muelekeo wa
Janja sio mzuri kitabia.
Alisema kwanza Janja
alikua mtoro wa shule na mara kadhaa hakwenda shule na alikua akimdanganya, aliwahi
kumkuta anaogoelea Ubungo Plaza wakati wenzake wako shule, amekuta msg za
matusi ambazo Dogo Janja aliwatumia watu wengine kuhusu Madee na makosa mengine
kadhaa.
Dogo Janja ambae sasa
hivi karudi Arusha tayari amefunguka kila kitu katika Interview ya Dakika 40
Exclusive on millardayo.com na yafuatayo hapo chini ni baadhi ya mambo
aliyoyazungumza.
Amesema “kwanza napenda
watanzania wajue kwamba mimi nilikua siishi na Madee nilikua naishi na rafiki
yake ambae ni Abdallah Doka Kimara jirani na Madee, Madee alikua haniangalii
kwa chochote na niliweka kikao juzi kati tu hapa nilikua nataka nirudi kwetu,
kula ni Doka, kuvaa Doka, Hela ya Shule Doka…. ninavyoongea hapa Dogo Janja
sijawahi kulipwa hela zaidi ya laki tatu kwenye show, Tanzania hii nimeshaizunguka
ujue alafu sioni faida yake nakwenda kwenye show nikirudi napewa laki moja
alafu ukiuliza mtu anaweza kukununia sasa nikawa zinanikera lakini nikawa
nashindwa kuongea sababu ndio niko pale kwa ajili ninasoma”
KUHUSU ACCOUNT YANGU
BANK:
“Madee alininyang’anya
mpaka kadi yangu ya ATM yani mimi narudi Arusha ni kama nakwenda kuanza maisha
mapya hamna ambacho useme labda narudi Arusha ni kama vile nakwenda kuanza
maisha mapya hamna ambacho useme labda naweza kurudi Arusha labda kwenye
account sijui nina shilingi ngapi, kachukua hela zangu zote kwenye account
yani, mi nilikua namuona mwema ananijali aliniambia nenda kafungue account na
kiuaminifu pale unatakiwa kuandia namba zako mimi sikuandika zangu nikaandika
za Madee, taarifa yoyote ya bank inakutana na Madee, mi siwezi kumtusi yule
nitakua namkosea sana hata akinipa radhi inaweza kunipata mi naongea kilicho
moyoni mwangu mpaka nimechukua hatua hii”
KURUDISHWA KWANGU ADA
SHULENI NA KIWANGO CHA PESA BANK:
“Na jina lote hili Dogo Janja nilikua narudishwa ada nyumbani,
nikachukua hatua nikaenda kufanya show ile hela yangu ya show baada ya kurudi
nakumbuka alitoa laki mbili na 60, hela ilikua yangu akaniambia… Ahh Janja hapa
sina hela nyingine nenda katoe kwenye account nitakurudishia.. ni brother alafu
mi namuheshimu sana, kadi yangu ya bank yeye ndio alikua anaizuia lakini mwisho
wa siku nakuja kuangalia account yangu, mbona account haisomi? na kadi yangu yeye
ndio alikua nayo… Millard nakwambia ukweli wa mwenyenzi Mungu mimi account
yangu haikuwahi kufikisha shilingi milioni moja na kila show ninayofanya
nalipwa shilingi milioni moja, naongea mbele za mwenyenzi Mungu mimi mtoto wa
kiislamu naitwa Abdulaziz”
KUHUSU SHOW YA MWISHO
KUIFANYA KABLA YA YEYE KUNIPIGA:
Madee alinipigia
simu jumapili akiwa Iringa ambapo jumanne wenzangu walikua wanaanza
mtihani,nilimwambia niko na Hassan nyumbani kwa Tunda akasema ana kaka yake
Kibaha alikua na show ya CCM alikua anamtaka lakini akaona hawezi na analove na
bro akashindwa kukataa, roho ilikua inaniuma mimi hapa mimi nakwenda kufanya
show kwa laki moja… alafu hapo niko na backup wangu nimempa elfu 20 mi nikabaki
na elfu 80 alafu hiyo 80 anakupigia…. wee sikia elfu 50 hiyo kaweke bank,
elfu 50 tumia…. mi nikafanya kipeace tu nikaenda kwenye show huyo brother wake
kachelewa kuturudisha hapa saa saba usiku kwa sababu ujue mimi sina usafiri na
yule jamaa alikua anasubiri mishe zake zote zikamilike alafu asubuhi nilikua
natakiwa kuingia shule, kosa sio langu ni la huyo kaka yake Madee.. sikwenda
shule jumatatu sababu nilichelewa.. hivi hata wewe Millard unaweza kulala saa
saba ukaamka saa kumi??????! hiyo siku ndio nilitakiwa kwenda kuchukua namba ya
mtihani nikapangwe la dawati langu ili jumanne nifanye mtihani, nilipoona
nimechoka nilimpigia mwalimu wa Darasa nikamwambia siwezi kwenda shule jumatatu
akaniambia hamna neno mi nikienda jumanne siku ya mtihani niende asubuhi
nitapata”
JINSI MADEE
ALIVYONIPIGA:
Nilikua nyumbani kwa
Tunda Man na Hassan ambae aliniacha baada ya kutumwa, nimekaa kidogo natoka
hivi nakutana na Madee geitini
hajaniuliza chochote zaidi ya kuanza kunipig,
kanichezeshea mikono kanipiga makofi alafu kanidhalilisha yani mtaa mzima
umekusanyana pale kwa Tunda Man, t shirt ilichanika na akanikatalia kupanda
kwenye gari… roho iliniuma palepale alafu alivyonikatalia kupanda kwenye gari
huku akiniambia anikute nyumbani baada ya dakika tano, roho iliniuma nikasema
haya yote nayapata kwa sababu mimi ndio nataka na napenda muziki na napenda
baadae niwe na maisha bora, niliongea na wazazi wakaniambia nivumilie lakini
kiukweli nikasema siwezi tena kuishi Dar es salaam na leo June 13 2012 ndio
siku ya mwisho kuishi Dar es salaam hapa ninavyoongea, jioni niliitisha kikao
nikampigia Doka, Madee, na kaka yangu huyu nikaulizwa labda kuna kitu Madee
hanifanyii mi nikashindwa kuongea nikasema bwana mimi sitaki chochote mi
nirudisheni kwetu ujue Millard mpaka mimi nachukua maamuzi haya kwamba naomba
nirudishwe kwetu, nimeomba nirudi kiroho safi tu lakini nashangaa yeye
anapokwenda kuongea mambo mengine kwenye media, mi namshangaa yule ni mtu mzima
anajielewa ujue, sasa mimi sijui kwa nini amekua hivyo”
KUHUSU MADEE KUMUOMBA
BABA YANGU ANIAMBIE NISIONGEE CHOCHOTE KWENYE MEDIA: “Alimpigia simu baba ya kumuomba
nisizungumze chochote kwenye media akidai kwamba itakua aibu kwangu na kwake,
mimi niko hewani lakini hakunipigia.. baadae nikapata simu kutoka kwa bro
akaniambia niongee na mama nilipoongea nae akaniambia Madee kasema nisiseme
chochote kwenye radio, sasa imefika jioni nikashangaa nikamsikia sasa
nikajiuliza kwa nini kaongea? na mimi siwezi kumpigia yule simu yani
nimeshaapia kwa mwenyeenzi Mungu siwezi kumpigia simu.
KUHUSU MIMI KUACHA
MUZIKI: “Roho inaniuma kichizi
nimeona hiviii, yani huu mziki huu kwa sababu haunisaidii chochote, mimi narudi
Arusha ni kama narudi tena kuanza maisha mapya kwa hiyo mimi nimeona bora tu
kama inawezekana huu muziki naweza kuacha na nitaishi kama zamani kwa sababu
kwetu sijaua, nimeona bora nitulie nyumbani ujue mpaka Millard pale nimeomba
kabisa jamani Eeehe nirudisheni nyumbani kwetu, nasema Inshallaah mwenyeenzi
Mungu yupo na mimi na riziki hapangi Madee riziki anapanga Mungu”
KUHUSU KUSOMA DAR ES
SALAAM: “Sitaki kabisa kusoma Dar es salaam mimi nakwenda kusoma Arusha au mkoa
wowote sitaki tena.
Hiyo ni sehemu tu
alichokisema Dogo Janja kuhusu yeye kuondoka kuwa chini ya Madee na kurudi
nyumbani kwao Arusha, mengine utaendelea kuyasikia kupitia AMPLIFAYA ya CLOUDS
FM leo saa moja usiku na pia hapa millardayo.com! kuna picha za hizo msg pamoja
na msg ya mwisho Janja kumtumia
Source- millardayo.com
No comments:
Post a Comment