May 2, 2012

PHOTOS: DIAMOND ALIVYOWEKA HISTORIA DAR LIVE…!!

Mashabiki wakiwa na mzuka wakumpokea Raisi wa Wasafi Diamond

Nyomi yakutosha katika viwanja vya dar Live Mbagala

Diamond Akiwapa Burudani Mashabiki wake .....


Pamoja na mvua kunyesha, mzuka uko palepale.

Diamond

Diamond Platnum akiwa na Rubani wake wakielekea kwenye chopper.

Diamond Akisali Kabla Myama Hajapaa Angani

Akitoa saluti kabla ya kupasua anga.



Huu ndio uwanja wa Dar Live Ukionekana Kwa Juu

April 29, 2012

WARAKA WA “RAY” KUHUSIANA NA MAREHEMU “STEVEN KANUMBA”…!!

Yapata wiki tatu sasa tangu msanii mwenzangu Steven Kanumba aage dunia, na kama ilivyo kwa kila kitu kinapotokea huandamana na kila aina ya maneno na hisia mbali mbali kutokana na mitazamo ya watu kupishana kuhusiana na jambo husika. Kulingana na muktadha huo, msiba wa Steven Kanumba umekumbwa na maneno na hisia kama hizo,hususan mazingira ya kifo chake; kinachosikitisha zaidi watu wengi (ambao wanajitambulisha kama wapenzi wa Kanumba), na baadhi ya vyombo binafsi vya habari vimekuwa vikinihusisha na kifo hicho, kwa kusema kwamba kwa njia moja au nyingine ninahusika na mauaji ya Steven Kanumba.

Kwa muda wote huo tangu msiba ulipotokea mpaka leo hii nashika kalamu kujaribu kuyaweka sawa na kuondosha hisia chafu katika fikra za watu, nimekuwa nikipitia katika wakati mgumu sana kwa jinsi ambavyo nimekuwa nikinyooshewa vidole kila upande nikihusishwa na kifo hicho, kiujumla nimezingatia maoni ya wapenzi ya mashabiki wangu wakinitaka kuwa na subira, ila kuna ukweli usemao kwamba, uongo ukirudiwa sana jamii huusadiki na kuuona ukweli,nimeona nisikae kimya ila niweke sawa hili kwamba sihusiki na kifo cha Steven Kanumba.

Nasema wazi kwanza sihusiki kabisa na kifo cha Kanumba kwanza kwa kuzingatia mazingira yenyewe ya kifo kilivyotokea. Wakati kifo hicho kinatokea, nilikuwa sehemu nyingine kabisa na mimi nilikuwa mtu wa tatu kutaarifiwa kwamba Kanumba amepatwa na mkasa ambao baadae ulisababisha kifo chake. Na na hata nilipofika katika hospitali ya Muhimbili (tofauti na watu wanavyodhani kuwa nilifika nyumbani kwake; ukweli mimi nilimkuta tayari amepelekwa Muhimbili), nilikuta tayari alikuwa ameshafariki ndio maana hata Polisi wanaohusika na usalama wa raia, si tu kwamba hawakuniweka chini ya ulinzi, sikuitwa hata kuhojiwa kwa sababu hakuna mazingira yoyote yanayonihusisha mimi na kifo hicho.

Pili, watu wanahusisha tofauti za kibinadamu zilizokuwepo baina yetu na kifo hicho, nasema hii sio sahihi kwa sababu kwanza ni kawaida kwa binadamu kutofautiana,isipokuwa kwetu sisi baadhi ya vyombo vya habari vilikuwa vinakuza kwa sababu nisizozijua, hivyo jamii ikachukulia kuwa tofauti zile ni uadui kitu ambacho sio sahihi, kwani sisi hatukuwa watu pekee tunaotofautiana kwani huu ni mwenendo wa kawaida wa dunia; hivi jana tumeshuhudia Waziri mmoja akieleza bayana katika mkutano na waandishi wa habari kuwa na tofauti na naibu wake, lakini hatuajasikia ikiandikwa wana ‘bifu’ bali imetafutwa lugha nzuri ya kupamba tofauti hizo, kwa kuwa waliohusika ni waheshimiwa, ila kwa wengine kutokana na sababu tusizozijua, inaonekana kama ni haki yetu kuandikwa vibaya. Kinachosikitisha, kwa nini jambo hili linachukuliwa kwa mkazo mkubwa sana, kwani hatujawahi kusikia watu wakiwa wanatofautiana na ndugu jamaa hata na marafiki zao na inaonekana kawaida tu? Kwani vyombo vya habari havikuwahi kuandika kuwa marehemu Steven Kanumba alikuwa na tofauti na baba yake, na yeye mwenyewe alitamka hivyo katika vyombo vya habari, mbona wameliongea bila kuongeza chumvi, na jamii inaona kuwa ni jambo la kawaida la kibinadamu.

Pengine watu wanaojaribu kuongea hayo, hawajui mimi na Steven Kanumba tumetoka wapi? Sisi si watu tuliokutana barabarani, tuna historia katika kazi yetu ya sanaa na pia katika maisha maisha yetu. Mwanzoni kabisa, mimi ndiye niliyempokea Kanumba pale Kaole na ndiye niliyemfundisha sanaa pale (nadhani watu wanakumbuka tamthiliya za wakati huo ITV) na baada ya hapo tulienda pamoja katika kampuni ya Game 1st Quality pamoja na tukafanya filamu kama Johari, ‘Sikitiko Langu’, ‘Dangerous Desire’ na nyinginezo, na tuliendelea kuwa pamoja katika kampuni hiyo mpaka tulipofanya filamu ya ‘Oprah’ mwaka 2008 ambapo niliingia rasmi kufanya kazi za kampuni yangu, lakini tuliendelea kuwa pamoja hata wakati nikiendelea na kazi za kampuni yangu.

Pia mimi nilikuwa wa kwanza kuanza kufanya kazi na Steps na baadae Kanumba alipoanza kufanya kazi zake mwenyewe na kunikuta huko tuliendelea kuwa pamoja kama siku zote. Kitu kikubwa kilichokuwa kinaendelea baina yetu, ni kwamba tulijenga ushindani wa kuendeleza kazi mbele kwa kila mmoja akitoa kazi, mwingine anamjibu.

Isitoshe hata vitu vyetu binafsi utaona kama kuna kufanana; kuna wakati Kanumba alinunua Toyota Ruv 4 nyeusi mimi nikanunua ya kijani, aliponunua Harrier na mimi nikanunua pia, na hata gari za hivi karibuni, ukitazama utaona kuwa zinafana kwa karibu; hii ilikuwa ni kama maisha yetu, hatukuwa na uadui, ilikuwa tunapeana changamoto za maendeleo.

Watu wanaojaribu kuonesha kuwa tofauti zetu ilikuwa ni uadui, huwa hawajui wapi tulikotoka ndio maana wanasema wasemavyo na katika kuthibitisha kuwa tofauti hizo hazikufikia katika uadui, kuna watu ambao wanafanya kazi nami katika kampuni yangu ya RJ ndio hao hao Kanumba alikuwa anawatumia siku zote katika kazi zake, hata baada ya tofauti hizo hakuna aliyekoma kufanya kazi na yeyote kati yetu.

Hii inathibitisha kuwa tofauti ilikuwa kati yetu kama binadamu, sio chuki za kimafanikio, ingekuwa hivyo watu kama Junior Syaary ambaye mara nyingi hufanya final editing katika RJ ndio huyo huyo alikuwa akifanya na Kanumba, Ally Yakuti ambaye anaandika script za RJ, ndiye huyo huyo aliyekuwa anaandika kwa Kanumba, Steven Shoo ambaye ni mtaalamu wangu wa light, ndiye huyo huyo anayetumiwa na Kanumba na wengine wengi kama Juma Chikoka aliyecheza kikamilifu katika filamu ya ‘Kijiji cha Tambua Haki’, ambaye pia anashiriki filamu nyingi za RJ, na wote hao, hawakuanzia kwa Kanumba, wote wameanza kwangu mimi ndio niliompatia na hata baada ya hayo yanayosemwa kuwa kuwa ni uadui, sikuwahi kuwakataza kufanya kazi na Kanumba.

Tatu kumtuhumu mtu kwa namna yoyote ile bila ya uthibitisho wa tuhuma hizo, ni kosa kwa sheria za nchi na pia kama ni mfuasi wa dini yoyote ni dhambi, kwani wakati ukisema hayo huku hujui uhalisia bali unasukumwa na nguvu za hisia tu ni sawa na kumchafua mtu huyo katika jamii bila ya kujua jamii inamchukuliaje. Napenda kusema wazi wazi kuwa, kwa kila anayetekwa na wimbi hili, ajaribu kufikiria leo ipo kwangu mimi, kesho inaweza kuhamia kwako, kwani mimi sio wa kwanza kufikwa na haya, inaweza kukukuta hata wewe au ndugu yako, utajisikiaje.

Na kama kweli mimi nimehusika na kifo cha Kanumba kwa namna yoyote ile, basi Mungu atanihukumu na kila aliye hai atashuhudia, ila kama sijahusika kwa lolote, Mungu hatonihukumu na badala yake ataniinua, kwa kuwa ninapita katika kipindi kigumu mno sasa hivi kwa madhila haya.

Mwisho kabisa napenda kumaliza kwa msemo usemao, ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke, kwani kadri mambo haya yanavyoendelea, usidhani yataishia kwangu, kwani mkono wa dhuluma haushii karibu, ukisikia jirani anapiga kelele za mwizi, usilale kamsaidie, usiseme kuwa hatuhusiki kwani hayupo kwetu, kesho utafikwa na wewe utakosa wa kukusaidia. cha msingi kama tunampenda sana ndugu yetu ni kumuombea kwa Mungu, kwani hatujui makao yake huko aliko, na sio kuunda vitu ambavyo kamwe hata yeye angekuwa hai asingeviafiki.”

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU STEVEN KANUMBA MAHALI PEMA PEPONI.

MUNGU IBARIKI AFRIKA MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Gwaii - Kazaa Kamua



 
Here is a clip shot of Gwaii’s “Kazaa Kamua” from his Thymuzik EP. The Official Music Video will be released in a few weeks from the people to enjoy it. shortly after that he will be releasing his official single from the upcoming album as well.

You can follow Gwaii on twitter @GwaiiThyword and also like him on facebook: http://www.facebook.com/gwaiimusic Gwaii’s EP is available on itunes, “Thymuzik” CDbaby and Amazon now!!

AACUSA - Proud To Be (Official Music Video HD)


African Artist Coalition USA (AACUSA) was formed with two goals in mind – promoting and exposing African arts and culture to the global/mainstream market, and creating a central platform that would showcase the arts and culture. With that vision in mind we created the PROUD TO BE project (P2B Project) to jump start our efforts towards achieving these goals.

This project brings together African artists who live in the USA for a joint project that represents African pride – proud of who we are in spite of our struggles, celebrating our accomplishments and looking forward to the journey ahead. This will involve a group of like minded young people and those young in heart, that love who they are and are ready to share this with the world.

Though there many reasons that motivated us to give birth to AACUSA, including addressing and providing aid to social, political and economical struggles that African is experiencing, we hope to shine a light to our culture and welcome all to embrace it. We also intend close the generational gap or the disconnect that exists between the young generation and that of Africa’s decision makers for a brighter future for all. Together we can be the change that Africa desires and deserves.

aacusa.net

Directed By: Dallas, Henry, & John
Shot by: Dallas, Henry, & John
Artists: Proud 2B African.
Song: Co-written by John Mahundi, Webiro Wassira & Lambert Tibaigana


ROMA MKATOLIKI KUYAWEKA MAISHA YAKE YA MZIKI KWENYE DOCUMENTARY YAKE MPYA.

Msanii anayeiwakilisha TANGA katika bongo fleva ROMA, baada ya kuchukua tuzo mbili za Kilimanjaro kama Msanii bora wa Hip Hop na wimbo wake Mathematics kuchukua kama wimbo bora wa Hip Hip hivi sasa anatengeneza Documentary yake inayoeleza maisha yake kimuziki toka alivyoanza mziki shida alizopitia mpaka kufikia hivi sasa alipofikia. 
Roma akiwa katika studio ya Tongwe Rec akiitengeneza DVD hiyo ambayo amesema nimapema sana kusema itatoka lini ila haitochelewa kutoka na anaamini watu wataipenda na italeta utofauti kidogo maana story iliyomo ndani ya Documentary hiyo iko kitofauti na itamgusa kila mmoja.

April 15, 2012

WASHINDI WA KILIMANJARO MUSIC AWARD WAPATIKA 2012


Hawa ndio washereheshaji  wa shughuli nzima Kushoto ni Milard Ayo Na Mwana dafada Vanessa Mdee

Mwakilishi wa kundi la Arusha Gold Akipokea Tuzo wimbo Bora wa Ragga

Baada ya Shughuli nzima kutia nanga Maojiano yaliendelea na waandishi mbali mbali wa Habari Ndani ya Ukumbi  







 Diamond & Ommy Dimpoz
  Mchekeshaji Kutoka Kundi la Ze Comrdy Mpoki Akitambulisha moja ya kikundi    

MPAKA MWISHO WA MCHAKATO WASHINDI WA TUZO ZA KILI MUSIC AWARDS WALIPATIKANA.

1. WIMBO BORA WA RAGGAE.
-ARUSHA GOLD BY WARRIORS FROM EAST.

2. WIMBO BORA WA DANCE HALL.
- MANENO MANENO BY QUEEN DARLIN.

3. WIMBO BORA WA ZOUK RHUMBA.
- DUSHELELE BY ALI KIBA.

4.BORA WENYE VIONJO VYA KIASILI.
- VIFUU UTUNDU BY A.T-

5. WIMBO BORA WA TAARABU.
- NANI KAMA MAMA BY MASHAUZI CLASSIC ( AISHA MASHAUZI).

6. WIMBO BORA WA KISWAHILI.
- DUNIA DARAJA BY TWANGA PEPETA-

7. WIMBO BORA WA AFRO POP.
- HAKUNAGA BY SUMA LEE-

8. WIMBO BORA WA R&B.
- NUMBER ONE FAN BY BEN PAUL-

9. WIMBO BORA WA HIP HOP.
- MATHEMATICS BY ROMA-

10. MSANII BORA ANAECHIPUKIA.
- OMMY DIMPOZ (NAI NAI SINGER).

11. RAPA BORA WA BAND.
- KALIJO KITOKOLOLO-

12. MSANII BORA WA HIP HOP.
- ROMA MKATOLIKI-

13. WIMBO BORA WA KUSHIRIKISHWA.
 - NAI NAI BY OMMY DIMPOZ FT. ALI KIBA-

14. WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI.
-KIGEUGEU BY JAGUAR-

15. MTUMBWIZAJI BORA WA KIKE.
- KHADIJA KOPA-

17. MTUNZI BORA WA MWAKA.
    - DIAMOND-

16. MTUMBWIZAJI BORA WA KIUME
- DIAMOND-

18. MTAYARISHAJI BORA WA MAPIGO YA MUZIKI.
- MANEKE-

19. VIDEO BORA YA MWAKA.
- MAWAZO BY DIAMOND-

20. WIMBO BORA WA MWAKA.
- HAKUNAGA BY SUMA LEE-

21. HALL OF FAME.
     -  TAASISI JKT-

22. HALL OF FAME KWA MTU BINAFSI.
      - KING KIKII-

23. HALL OF FAME KWA MTU BINAFSI.
     - DR. REMMY ONGALA-

24. MWIMBAJI BORA WA KIKE.
     - LADY JAY DEE-

25. MWIMBAJI BORA WA KIUME.
      - BARNABA-


New Video KPD Wanyamwezi - Reloaded


New Video JJ FEAT MR BLUE - UMENIACHA ( EMPTYSOULZ ) OFFICIAL HD VIDEO


Nwe Video - Gangwe Mobb ft. Dulayo - Ndio dawa yao (Official Video).flv


April 10, 2012

MOTO MKUBWA WATOKEA KATIKATI YA JIJI LA ARUSHA - MAJENGO ALMAARUFU CHINI YA MTI



















Umati wa Watu waliokuwa wakishuhudia Moto huo


Askari polisi walikuwepo Kuhakikisha Usalama Unapatikana Sehemu hiyo.


Moja Ya Duka Likiteketea kwa moto


Hawa ni vijana Walikuwa wakisaidia Kuzima Moto




Moto Mkubwa Watokea Katikati ya Jiji La Arusha sehemu ya  Majengo alimaarufu Chini Ya Mti  Mchana wa leo
Moto huo ambao chanzo chake hakijajulikana mara moja. Moto huo uliweza kuunguza Maduka Takribani 9 , Japokuwa gari la fire liliwahi katika Eneo la tukio lakini halikuweza kufanikiwa kuuzima moto huo kwani gari hilo lilishiwa na Maji , na ndipo magari megine ya zima moto kuwasili na kuweza kuuzima moto huo.


PICHA NA NASS (www.djnasi.blogspot.com)