November 8, 2011
October 26, 2011
CLUB AQ THIS FRIDAY - IN ARUSHA
SEIF JAMAL PROUDLY PRESENTS: “THRILLER”
TRENTON'S OFFICIAL HALLOWEEN COSTUME PARTY
THRILLER NIGHT FRIDAY OCT.28 LADIES FREE TILL 12AM WITH COSTUME
SATURDAY OCT. 29ST THE OFFICIAL HALLOWEEN COSTUME PARTY
SPECIAL GUEST AND LIVE SHOWS BOTH NIGHTS
TRENTON'S OFFICIAL HALLOWEEN COSTUME PARTY
THRILLER NIGHT FRIDAY OCT.28 LADIES FREE TILL 12AM WITH COSTUME
SATURDAY OCT. 29ST THE OFFICIAL HALLOWEEN COSTUME PARTY
SPECIAL GUEST AND LIVE SHOWS BOTH NIGHTS
Track Mpya Da Hustler-Mistakes (Prod. Daz Naledge).mp3
Click Here to Listening Hulkshare.com Da Hustler-Mistakes (Prod. Daz Naledge).mp3
Song......Mistake
Song......Mistake
Artist.........Ibra da Hustler
Produced by......Daz Naledge
Studio..............Watengwa Records
BAADA YA KIMYA KIREFU STOPPER ATADONDOSHA TRACK YAKE MPYA SOON
Baada ya kimya kingi,,,msanii wa hiphop toka Arrachugga Stopper The Rhymecaa arudi tena,,safari hii akiwa amemshirikisha Q the Don,''Nipo katika hatua za mwisho za kukamilisha video ya ngoma hii,nafurahi sana kwani nimekuta pia na Director wangu Dennis Mallya ndo alikua amemaliza kujipanga upya kabisa kwahiyo watu wangu wakae tu mkao wa kula kwani sijawaangusha'' alisema Stopper,audio ya kazi hii imetengenezwa ndani ya Studio za Mo Records-Mwanza na kideo ni toka Grandmaster Records-ArushaMuda wowote track hiyo itadondoka hapa hapa katika Blog yako Pendwa
www.djnasi.blogspot.com
August 30, 2011
DJ NASS BLOG WISHING YOU EID MUBAARAK
July 26, 2011
MGOMO WA DALADALA ARUSHA
Baadhi ya wadereva wa dala dala wakiwemo wapiga debe walilizonga gari aina ya haice ambalo lilionekana likikaidia amri ya kugoma na kuendelea kupakia.
HALI si shwari katika jiji la Arusha mara baada ya jeshi la polisi kuingilia kati na kuzima maandamano ya madereva wa daladala pamoja na makondakta kwa kwafayatulia mabomu ya machozi,walipokuwa wakiandamana asubuhi kuelekea katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha.
Madereva hao wametangaza mgomo usio na kikomo hadi pale madereva wenzao zaidi ya 50 waliopo mahabusu na magereza waachiwe huru bila masaharti yoyote.
Huduma za usafiri jijini Arusha zimesimama tangu majira ya saa 11;00 asubuhi baada ya madereva hao kushinikiza kilio chao kisikilizwe ambapo mojawapo ya madai yao ni pamoja na unyanyasaji kupitia askari wa usalama wa barabarani.
Maelfu ya wakazi wa jiji la Arusha wakiwemo wanafunzi wamelazimika kutembea kwa miguu kwa umbali mrefu kwa zaidi ya kilomita 50 kwenda maeneo mbalimbali katikati ya mji kutokana na mgomo huo hali iliyopelekea madereva wa pikipiki maarufu kama “bodaboda” waliazimika kupakia abiria hao ili kuwafikisha katika maeneo mbalimbali.
Hata hivyo,katika hali isiyo ya kawaida askari wa usalama wa barabarani ambaye hakutambulika jina lake mara moja alijikuta katika wakati mgumu baada ya kushushiwa kipigo kikali na madereva hao wakiwemo wapiga debe katika eneo la Annex jijini hapa wakati akiongoza magari kitendo kilichopelekea kukimbilia katika duka la kuuza majokufu lililopo mkabala na jengo la Kimahama kwa lengo la kunusuru maisha yake.
Jeshi la polisi lililazimika kuzuia kundi la madereva hao wapatao 200 majira ya saa 4;00 asubuhi katika eneo la mnara wa Mwenge jijini hapa kwa kuwatawanya huku wakitumia mabomu ya machozi zaidi ya 10 hali iliyozua tafrani katikati ya jiji la Arusha na kupelekea shereha za mashujaa zilizokuwa zikifanyika katika ofisi ya mkoa kuingia dosari.
Magari ya jeshi la polisi yakiwa yemesheheni askari wenye silaha na mabomu yalikuwa yakizunguka katikakati ya jiji la Arusha kwa lengo la kuhakikisha usalama wa raia na mali zao jijini hapa.
Wakizunguza kwa nyakati tofauti madereva wa daladala pamoja na makondakta kwa nyakati tofauti walisema ya kuwa wao wanapinga vikali kitendo cha jeshi la polisi kuwakamata wenzao ambao ni zaidi ya 40 na kwa maksoa ya barabarani na kisha kuwafikisha jela kwa makosa ya ujambazi.
Madereva hao waliwataja askari hao kwa majina ya Modesta,Peter na Dan kuwa wamekuwa wakiwasumbua kwa kuwakamata mara kwa mara huku wakiwaomba rushwa ya kiasi cha sh,10,000 hadi sh,250,000 kitendo wanachodai sio haki.
Hata hivyo mkuu wa mkoa wa Arusha,Isdore shirima alitoa tamko la kuwataka madereva hao kurudisha magari barabarani wakati serikali na vyombo husika wakashughulikia suala lao
Katika hatua nyingine mahabusu waliofikishwa mahakamani majira ya saa 5;00 katika mahakama kuu kanda ya Arusha kwa lengo la kusikiliza hatma ya kesi zao waligoma kushuka ndani ya karandiga hilo huku wakidai kuwa kucheleweshwa kusikilizwa kwa keshi zao.
Kizaazaa hicho kiliibuka mahakamani hapo na kuepelekea mahabusu hao kurudishwa rumande baada ya kugoma kushuka katika karandiga hilo ambapo pamoja na juhudi za kuwashawishi kushuka ndani ya karandiga hilo kufanywa lakini waliendelea kugoma .
July 14, 2011
THT ARTIST JOIN USHER RAYMOND IN ATLANTA

THT Artists join Usher Raymond in Atlanta.
Usher's New Look Foundation, established in 1999 has invited THT artists to join him at the World Leadership Conference and Awards in Atlanta this week.
Mwasiti, Amini, Barnaba, Linah, Ditto & Keyboard player Mose Delema will be flying to the United States to join him at the World Conference where they will perform on stage with one of their most popular icons Usher Reymond.
Usher’s team has invited the THT Artists to participate in a 4-day conference that includes sharing experiences, discussing local, national and global issues, working together in an international choir featuring a solo performance by Usher as well as performing their own songs during the Awards Night.
Traveling with Ruge Mutahaba the Founder of Tanzania House of Talent and B12 popular Radio DJ from Clouds Fm, Ruge Mutahaba says ‘The artists have been given an amazing opportunity to travel to Atlanta to participate not only with an international artist for the Awards Night but to also contribute and learn by participating in the youth conference.’
B12 said ‘It’s great to see first hand how Usher Reymond is celebrating youth’s involvement in leadership. He is keen to demonstrate how young talent, education and public service can make a difference and I will be following the conference and giving updates regularly on Clouds FM.’
http://www.ushersnewlook.org/
July 12, 2011
SHOW LOVE NDANI YA TRIPLE A NIGHT CLUB
Picha juu Ni Wana Kibao tu wakila Bata _ Ndani Ya Triple A Night Club
picha zote Kwa Hisani ya Fullbata .com
June 24, 2011
MOPLUS NA JOHMAKINI WAKAMILISHA VIDEO YA XRAY

Moplus na JohMakini ndani ya video ya X-ray ilofanywa chini ya camera
za hoodpixx arachuga kwa uongozi wa producer/director DeFXtro,Track
inayopatikana ndani ya "babawa ukoo" Vol 1 album iiliyo kitaa tayari
kwa shillingi elfu tano za kitanzania holla @ +255 715 240 005
chek pia machiz wakizungumzia hiphop na mitaa inavobonga..
http://www.youtube.com/watch?v=qB0I9Xw9Nao
June 15, 2011
May 6, 2011
DOGO JANJA AZUNGUMZIA MUSIC NA SHULE
DOGO JANJA KATIKA POZI
Wiki hii namleta kwenu chalii anayekuja kwa kasi kwenye muziki wa kizazi kipya. Jina lake anaitwa Abdulaziz Chende lakini kisanii anafahamika kwa jina la Dogo Janja.Alizaliwa Arusha 1997 katika Hospitali ya Mount Meru. Alisoma Shule ya Msingi Unga Limited na kuhitimu mwaka 2010. Kwa sasa anasoma kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Makongo. Mengi zaidi kuhusu chalii huyu, ungana nami katika maswali kumi ambayo nilimuuliza.
NASS: Je, hapa Dar unaishi na nani na ni nani anayekulipia ada ya shule?
DOGO JANJA: Naishi na Madee na Tip Top Connection ndiyo wanaonilipia ada.
NASS: Ilikuwaje ukaingia katika familia ya Tip Top na wakaamua kugharamia elimu yako?
DOGO JANJA: Kwanza ifahamike kwamba, Madee siyo ndugu yangu ila alinikuta kwenye shoo Arusha akavutiwa na kipaji changu ndipo walipoamua kunichukua.
NASS: Umri wako bado ni mdogo, imekuwaje ukaingia kwenye fani hii mapema hivi?
DOGO JANJA: Nakumbuka nikiwa darasa la tatu mwalimu wa Somo la Stadi za Kazi alituambia kila mwanafunzi atunge wimbo na aimbe, mimi nilitunga wimbo unaohusu Ukimwi na nikaimba vizuri. Kuanzia hapo nikaanza kuimba muziki huku mwalimu huyo akiwa ananisaidia kwani na yeye alivutiwa na mimi.
NASS: Wazazi wako waliupokea vipi uamuzi wako wa kuingia kwenye muziki hasa ukichukulia kwamba wengi wanadhani muziki ni uhuni?
DOGO JANJA:Walikubaliana nami lakini wakaniambia ‘chonde chonde’ nisiache shule.
NASS: Je, wimbo wako wa kwanza kusikika uliitwaje?
DOGO JANJA: Ulikwenda kwa jina la ‘Sijafikia’ ambao kwa bahati mbaya ulisikika Arusha tu lakini mpaka sasa nina albamu moja inayokwenda kwa jina la Ngarenaro.
NASS: Mpaka sasa kuna mafanikio yoyote ambayo umeyapata kutokana na muziki?
DOGO JANJA: Yapo madogo madogo lakini kikubwa ni kwamba nimepata fursa ya kupata elimu bure.
NASS:Vipi kuhusiana na mchezo wa baba na mama, bado unaundeleza?
DOGO JANJA: Michezo hiyo nimeiacha kitambo, sasa niko ‘siriasi’ na masomo na muziki.
NASS: Hudhani kwamba muziki unaweza kukufanya ukashindwa kufanya vizuri darasani?
DOGO JANJA: Kwa hilo sidhani, ninachoamini ni kwamba naweza kufanya vitu vyote kwa wakati mmoja.
NASS: Ni matatizo gani ambayo umekuwa ukikumbana nayo kila siku?
DOGO JANJA: Ni ya kawaida tu, napambana nayo kuhakikisha hayaniharibii malengo yangu.
NASS: Nini matarajio yako ya baadaye?
DOGO JANJA: Ndoto zangu ni kuja kuwa mwanamuziki mkubwa wa kimataifa, naamini hilo litatimia tu.
Interview By Nass.
May 5, 2011
MASHINDANO YA MISS NJIRO YAPAMBA MOTO
Washiriki Wakiwa Kambini
Msanii wa kizazi kipya Barinaba anayetamba na kibao cha’ Milele’ anatarajia kupamba shindano la kumsaka mrembo wa kitongoji cha NJiro ambacho yanatarajia kufanyika kesho May 6 katika ukumbi wa Naura spring uliopo jijini hapa.
Akiongea na gazeti hili mratibu wa shindano hilo Upendo Simwita alisema kuwa nia ya kuandaa mashindano haya ni kumtamfuta mrembo wa kitongoji cha njiro ambacho kwa miaka mingi Hakijapata mrembo ambaye atawakilisha mkoa kwenye mashindano ya urembo .
“ Arusha kunavitongoji vingi na katika kitongoji ambacho kitaanda ni kimoja tu ambacho ni Arusha city cetre hivyo tume amua kuandaa ili kuwepo na vitongoji vingi ambavyo vitaandaa na kukutana pamoja ili kumpata mrembo ambaye atawakili mashindano haya kumsaka miss arusha ambaye mrembo huyo ataweza kuwakilisha vyema hata katika miss Tanzania na kuleta taji mkoani hapa”alisema Simwita.
Alibainisha kuwa jumla ya warembo 10 wanashiriki katika kinyanganyiro huko na kufafanua kuwa warembo wote ni wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya mkoani hapa na kusema kuwa anaamini kabisa mrembo ambaye atapatika katika mashindano haya atawakilisha vyema kitongoji katika mashindano ya mkoa na hata taifa.
Aliwataja warembo ambao watashiriki shindano hilo kuwa ni Tunu Mamuya (19),Zamda Idd(18),Winnie Mogiga(20),Sylivia Selvatory(20),Docas Geerad(20),Maria Hamed (19),Angela Deo(20),Stella Willson(20),Elizaneth Daimal(19) pamoja na Genovever Mike (20).
Alisema kuwa mshindi wa kwanza wa mashindano haya anatarajiwa kuondoka na kitita cha shilingi milioni moja huku mshindi wa pili akiondoka na shilingi laki mbili huku watatu akiwa anatarajia kuondoka na kitita cha shilingi laki moja .
Alifafanua kuwa wathamini ambao wamejitokeza tofauti na wathamini wakuu ambao ni Vodacom lakini pia kunawathamini wengine ambao wamejitokeza ambao ni ngorongoro consavesheni,mwandago investimenti, Triple A radio, Saumu Fasheni,saprini power veto ,Victoria investisheni pamoja na wenyeji ambao ni Naura spring hoteli.
‘’kingine pia warembo watano ambao watashinda watapata ajira kutoka katika hoteli hii ya naura spiring hoteli ambayo imeaamua kuchukua wasichana watano ambao watapewa kazi na mbali na hilo pia naura watakuwa pia na shindano la kumsaka mrembo wa hoteli yao”alisema Shimwita
Alisema pia barinaba anatarajia kusindikizwa wasanii wengine ambao ni pamoja na boda 2boda,ndanda Kosovo pamoja na wengine wengi.
“Napenda kutoa wito kwa wakazi wa mkoa wa arusha wajitokeze kwa wingi kushuhudia shindano hilo kwani warembo wa mwaka huu wa miss njiro ni wazuri sana”alisema Shimwita.
Habari na Picha Woinde Shizza
Subscribe to:
Posts (Atom)





































