July 11, 2010

UJERUMANI YATWAA NAFASI YA TATU

                                                            Kikosi Cha Ujerumani
Ujerumani imenyakua nafasi ya tatu kwenye mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini, baada ya kuifunga Uruguay mabao 3-2 katika uwanja wa Nelson Mandela Bay, mjini Port Elizabeth.
Sami Khedira aliifungia Ujerumani bao la ushindi katika dakika ya 82 baada ya ngome ya ulinzi ya Uruguay kushindwa kuondosha mpira wa kona uliopigwa na Mesut Ozil.
Sekunde chache kabla ya mchuano kumalizika mshambuliaji wa Uruguay Diego Forlan alipiga mpira wa adhabu uliogonga mwamba.
Ujerumani ndio waliotangulia kufunga katika dakika ya 18 kupitia Thomas Muller, kabla ya Edinson Cavani kuisawazishia Uruguay dakika 10 baadaye.

Lala salama

Kipindi cha kwanza kilimalizika 1-1 na dakika 6 baada ya cha pili kuanza Diego Forlan alisukumiza wavuni pasi kutoka kwa Egidio Arevalo, Uruguay ikawa inaongoza 2-1.
Hilo lilikuwa bao la tano la Forlan kwenye michuano hiyo ya Kombe la Dunia, na ni miongoni mwa wafungaji bora.
Katika dakika ya 56, Marcell Jansen aliisawazishia Ujerumani kwa bao la kichwa baada ya krosi ya Jerome Boateng kumzidi mlinda mlango Fernando Muslera.
Baada ya Sami Khedira kuifungia Ujerumani bao la ushindi , Uruguay walizidisha mashambulizi bila mafanikio.
Kocha wa Ujerumani, Joachim Loew, aliwapumzisha wachezaji mashuhuri miongoni mwao mshambuliaji Miroslav Klose, Likas Podolsi na mlinzi Philip Lahm.
Klose alikosa nafasi ya kufikisha goli la 15 idadi ambayo mshambuliaji wa Brazil, Ronaldo amekwisha funga katika historia ya mashindano ya Kombe la Dunia.

July 10, 2010

KATIKA SAFU YA MAPENZI: Kwanini ukubali kuchangia penzi?

Kati ya vitu vinavyowaumiza wengi walio katika uhusiano ni pamoja na penzi la kuchangia! Yaani uwe na mpenzi wako, halafu awe na mtu mwingine tena zaidi yako. Hakika inauma sana. Uhusiano wenye ladha ni ule wa mwenzi mmoja. Uwe wake peke yako, awe wako peke yake!

Mapenzi ni sawa na bustani nzuri ya maua, wakati mwingine inahitaji mbolea, kumwagiliwa maji na hata kupaliliwa. Kwa kufanya hivyo utazidisha ladha ya mapenzi na kuyafanya yazidi kuwa na nguvu zaidi ya awali. Lakini kama hutamwagilia, hutaweka mbolea, hutapalilia, hesabu kwamba mapenzi yako yanaweza kuanza kupoteza nguvu taratibu na hatimaye kufa kabisa.

Kikubwa ambacho nimepanga kuzungumza nanyi leo ni jinsi ya kumfanya mpenzi wako awe wako peke yako. Umeshawahi kufikiria kwamba, kama ukishindwa kutimiza mambo fulani katika penzi au ndoa yako, mwenzi wako anaweza kuwa wa kushea?

Kama bado, inakubidi ufahamu hilo kuanzia leo. Mpenzi anahitaji mambo mengi ili aendelee kuwa mwaminifu kwenye penzi lenu. Ni kweli kwamba uaminifu upo kwa mtu mwenyewe, kama mtu ni mwaminifu basi atadumisha uaminifu uliopo ndani yake, lakini kama kuna mambo unakosea, lazima utasalitiwa!

Tena basi, kama mwenzi wako anakupenda, atakusaliti huku analia! Kwanini? Kwasababu analizwa na kitendo ambacho hajapenda kukifanya ila wewe mwenyewe ndiyo umemlazimisha afanye hivyo.

Wanatafuta nini kwa wengine?
Tukiachana na tamaa, hulka na ushawishi, wakati mwingine mpenzi anaweza kusaliti kwa kukosa yale ya muhimu zaidi katika penzi au ndoa yake.

Kwa bahati mbaya sana, watu wa aina hii huwa hawasemi moja kwa moja kuwa wanakosa vitu fulani au wanapenda vitu fulani, badala yake hutumia lugha za ishara zaidi na kama hutaelewa basi huona suluhisho na kutafuta pumziko lingine nje.

Hapa sasa mwenzi wako anakuwa si wako peke yako tena! Lakini lazima uhakikishe mpenzi wako anaendelea kuwa wako bila kushea na mtu yeyote na jambo hili linawezekana kabisa ikiwa wewe mwenyewe utataka iwe hivyo.

Zipo hatua au mambo mengi ya kumfanyia mpenzi wako ili awe wako peke yako, lakini hapa nitakupa yale ya msingi zaidi yatakayokusaidia katika penzi lako.

Kama inavyoonekana hapo juu, nimeyafananisha mapenzi na bustani nzuri ambayo ina mahitaji yake. Sasa katika uchambuzi huu, nitaainisha jinsi ya kuitunza bustani (penzi) yako vizuri sana na kuifanya bora zaidi kila siku.

MOSI: Mapenzi yanahitaji mbolea. Hapa nazungumzia penzi ambalo tayari limeshakuwa penzi! Kama ni bustani basi tayari mboga-mboga zako zimemea vizuri.

Lakini ukumbuke kwamba, bustani yako haitaweza kuendelea kuwa bora kama haitakuwa na matunzo. Hapa penzi linahitaji mbolea. Mbolea ninayoizungumzia hapa ni maneno matamu yaliyojaa huba. Fikisha hisia zako kwa mwenzi wako kwa namna ya kipekee iliyojaa penzi la dhati.

Mweleze jinsi unavyompenda na jinsi maisha yako ambavyo hayawezi kukamilika bila yeye. Huu ni wakati wako wa kumsumbua kwa meseji zilizojaa tungo za mahaba, kadi, maua na zawadi ndogo ndogo.

Baadhi ya wanandoa wakishaoana, huacha utaratibu huu. Kuna wanaosema: “Ah! Hayo mambo ya kizamani bwana, kipindi akiwa demu wangu, sasa hivi yupo ndani, kwanini nihangaike?”
Haya ni makosa makubwa ndugu yangu. Shamba bila mbolea kuna mavuno kweli?

PILI: Bustani yako itahitaji maji kwa ajili ya kuzidisha ustawi wa mazao yako. Hapa unatakiwa kuwa mbunifu zaidi katika mambo yanayohusu mapenzi moja kwa moja.

Unatakiwa kubadilisha mitindo ya chumbani, mahali pa kukutana na hata sehemu za mitoko. Inashauriwa ili kuboresha penzi ni vizuri kutoka sehemu mbalimbali na mwenzi wako. Inapendeza zaidi angalau mara tatu kwa miezi sita, kulala na mwenzako hotelini.

Hapa utakuwa unanakshi zaidi penzi lako. ‘Outing’ yako ni vyema ikawa ya kimahaba zaidi, kuanzia mavazi, sehemu mnazotembelea n.k

Mfanyie mwenzi wako mambo ya kimahaba mnapokuwa wawili. Mbusu, mkumbatie, mwambie jinsi unavyojisikia wa pekee kuwa wake.

TATU: Baada ya muda bustani huota majani mengine ambayo si mboga! Yawezekana kabisa, kwa bahati mbaya uchafu ukaingia bustanini. Wakati wa palizi ni muda sahihi wa kuondoa vyote hivyo.
Hata katika mapenzi pia hutakiwa kufanya jambo hili. Kugombana au kupishana kiswahili kwa wapenzi ni jambo la kawaida sana, hivyo ni vyema kuweka sawa tofauti hizo mapema, kabla tatizo halijawa kubwa zaidi. Hii ndiyo palizi ninayoizungumzia.

Usikae na kinyongo moyoni mwako, kuwa mjanja, hata kama ni yeye ndiye aliyekosea, zungumza naye ukimweleza jinsi ambavyo hupendi mgombane, mkimweleza hisia zako kwamba unatamani sana muelewane katika siku zote za maisha yenu. Weka mambo sawa.

Kwa kufanya hivi, kwa hakika penzi lako litazidi kuwa imara zaidi na atakuwa wako peke yako. Hatakuwa wa kuchangia tena. Naamini umeibuka na kitu kipya leo. Ahsante sana kwa kunisoma, tuonane tena wiki ijayo.

Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Mambo ya Mapenzi ambaye anaandikia magazeti ya Global Publishers, ameandika Vitabu vya True Love na Secret Love. Kwa makala zaidi, hadithi na mijadala ya kimapenzi, mtembelee kwenye tovut

HIVI NDIVYO FIESTA 2010 JIPANGUZE RAAAAAAAAAAAA RAAAAAA ILIVYOKUWA

Kundi la  wazushi Kutoka  A-Town likipangusa vilivyo  katika Fiesta 2010
Wakiwa kwenye Fiesta Jipanguse 2010 jijini A-Taun toka shoto ni Marry,Meneja Vipipndi wa Clouds FM Sebastian Maganga,Mtangazaji wa kipindi cha Michezo Clouds FM Ibrahim Masoud a.k.a Maestro,Tirra,Kida Waziri pamoja na Sophia Kesy Wa Clouds Fm

Hao hapo ni  nyomi ya mashabiki waliohudhuria katika fiesta 2010 pale Matongee Carnival
watu walifiestika vilivyo
Mwanamuzi mkongwe wa muziki wa dansi Ndandaa Kossovo kulia na skwadi lake zima wakitumbuiza katika Fiesta Jipanguse 2010 usiku wa kuamkia leo ndani ya Matongee Club jijini Arusha.

Picha Zote Na Nassir

July 8, 2010

HISPANIA YAINGAMIZA UJERUMANI 1-0

Fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini itakuwa kati ya Hispania na Uholanzi.
Mpambano huo wa kihistoria umetokana na Hispania kuishinda Ujerumani bao 1-0 katika uwanja wa Moses Mabhida mjini Durban na kufuzu fainali kwa mara ya kwanza katika historia.
Bao pekee la mechi hiyo lilifungwa kwa kichwa na mlinzi Carles Puyol katika dakika ya 73, alipopanda mbele kucheza mpira wa kona.
Ujerumani walionekana kikosi tofauti kabisa na timu ambayo iliiondoa England kwa kuifunga mabao 4-1 na baadaye kuitandika Argentina mabao 4-0 kwenye mechi ya robo fainali.

Uchochoro

Pengo la mshambuliaji Thomas Muller ambaye alikuwa nje kutokana na adhabu ya kadi mbili za njano lilikuwa wazi kabisa kwenye safu ya ushambuliaji ya Ujerumani.
Muller ambaye ameshafunga mabao manne kwenye Kombe la Dunia alipata kadi ya pili ya njano kwenye mechi kati ya Ujerumani na Argentina, na bila yeye, kocha Joachim Loew alikosa kabisa mbinu za ushambuliaji kwa timu ya Ujerumani.
Hispania walidhibiti mchezo katika muda wote, na wangeweza kufunga mabao mengi zaidi lakini umaliziaji ukawa mbaya, pamoja na mlinda lango wa Ujerumani, Manuel Nuer kuokoa mipira kadhaa.
Fainali ya siku ya Jumapili kati ya Hispania na Uholanzi katika uwanja wa Soccer City mjini Johannesburg itawakutanisha wafungaji wanaaongoza kwa sasa; Wesley Snijder na David Villa.
Ni mara ya kwanza kwa Hispania kucheza fainali ya Kombe la Dunia, na kwa upande wa Uholanzi itakuwa mara ya tatu, ingawa bado hawajapata kushinda Kombe hilo.
Mechi ya kutafuta mshindi wa tatu na wanne itachezwa Jumamosi kati ya Uruguay na Ujerumani.

July 7, 2010

GHANA YAITAKA FIFA KUBADILISHA SHERIA





Waziri wa michezo wa Ghana amesema shirikisho la soka duniani FIFA linatakiwa kubadilisha sheria za mchezo wa soka kufuatia kuondolewa kwa Ghana kwenye robo fainali ya Kombe la Dunia baada ya kutumika mikono.
Waziri huyo Akua Sena Dansua hajasema ni sheria zipi angetaka zibadilishwe, lakini watu wengi wamekuwa wakisema mwamuzi wa mchuano wa robo fainali kati ya Ghana na Uruguay angetakiwa kuipa Ghana goli, wakati mchezaji wa Uruguay Luis Suarez alipoondosha kwa mikono mpira uliokuwa unaingia kwenye lango la timu yake.
Kwenye mechi hiyo mshambuliaji wa Ghana Dominic Adiyah alipiga mpira kwa kichwa ukaeleka kuingia katika lango la Uruguay ukibakia muda mfupi sana kabla ya mechi kumalizika, lakini Suarez ambaye ni mchezaji wa ndani akauondosha kwa mikono.
Mwamuzi alimwonyesha kadi nyekundu Suarez na akawapa Ghana penati ambayo Asamoah Gyan alipiga nje.
Adhabu hiyo ni kulingana na sheria zilizopo za shirikisho la soka dunia FIFA.
Mechi ilimalizika kwa sare, ikalazimika kuingia mikwaju ya penalti na Uruguay wakaibuka washindi wa mabao 4-2.
Ghana ilikuwa timu ya Afrika kufikia hatua ya robo fainali katika Kombe la Dunia.
Baada ya kurejea nyumbani Black Stars walipokelewa kwa shangwe na nderemo mjini Accra.
Rais wa Ghana John Atta Mills alisema wachezaji hao watapewa tuzo za kitaifa na pia dola 20,000 kila mmoja.
Mashabiki wa soka kote barani Afrika waliishabikia Ghana wakati wa mchuano huo, na wengi walipigika sana baada ya Black Stars kuondolewa.
Ilikuwa ni timu pekee ya Afrika iliyobakia kwenye mashindano baada ya timu zingine tano za Afrika kuondolewa kwenye raundi ya kwanza ya michuano hiyo.

JIACHIE NA KAMERA YA DJ NASS


Katika Jiachie na camera ya Dj Nass hawa hapa ni washakaji wa kitaa nao waliamua kujiachia namna hiyo.

ARUSHA BARABARA HAKUNA


Kadri siku zinavyokwenda Mkoa wa Arusha unakabiliwa na ukosefu wa barabara hilo limebainika hasa pale inapofika mida ya Asubuhi na Jioni kunakuwepo na msongamano mkubwa sana wa magari.

July 6, 2010

Nass

Hii ni Blog Mpya Kabisa Ambayo bado ipo katika Maintenance ya muda mfupi tu.
baada ya muda itakuwa na vitu vya kutosha kabisa hasa hasa Burudani/michezo habari mbali mabali