July 8, 2010

HISPANIA YAINGAMIZA UJERUMANI 1-0

Fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini itakuwa kati ya Hispania na Uholanzi.
Mpambano huo wa kihistoria umetokana na Hispania kuishinda Ujerumani bao 1-0 katika uwanja wa Moses Mabhida mjini Durban na kufuzu fainali kwa mara ya kwanza katika historia.
Bao pekee la mechi hiyo lilifungwa kwa kichwa na mlinzi Carles Puyol katika dakika ya 73, alipopanda mbele kucheza mpira wa kona.
Ujerumani walionekana kikosi tofauti kabisa na timu ambayo iliiondoa England kwa kuifunga mabao 4-1 na baadaye kuitandika Argentina mabao 4-0 kwenye mechi ya robo fainali.

Uchochoro

Pengo la mshambuliaji Thomas Muller ambaye alikuwa nje kutokana na adhabu ya kadi mbili za njano lilikuwa wazi kabisa kwenye safu ya ushambuliaji ya Ujerumani.
Muller ambaye ameshafunga mabao manne kwenye Kombe la Dunia alipata kadi ya pili ya njano kwenye mechi kati ya Ujerumani na Argentina, na bila yeye, kocha Joachim Loew alikosa kabisa mbinu za ushambuliaji kwa timu ya Ujerumani.
Hispania walidhibiti mchezo katika muda wote, na wangeweza kufunga mabao mengi zaidi lakini umaliziaji ukawa mbaya, pamoja na mlinda lango wa Ujerumani, Manuel Nuer kuokoa mipira kadhaa.
Fainali ya siku ya Jumapili kati ya Hispania na Uholanzi katika uwanja wa Soccer City mjini Johannesburg itawakutanisha wafungaji wanaaongoza kwa sasa; Wesley Snijder na David Villa.
Ni mara ya kwanza kwa Hispania kucheza fainali ya Kombe la Dunia, na kwa upande wa Uholanzi itakuwa mara ya tatu, ingawa bado hawajapata kushinda Kombe hilo.
Mechi ya kutafuta mshindi wa tatu na wanne itachezwa Jumamosi kati ya Uruguay na Ujerumani.

July 7, 2010

GHANA YAITAKA FIFA KUBADILISHA SHERIA





Waziri wa michezo wa Ghana amesema shirikisho la soka duniani FIFA linatakiwa kubadilisha sheria za mchezo wa soka kufuatia kuondolewa kwa Ghana kwenye robo fainali ya Kombe la Dunia baada ya kutumika mikono.
Waziri huyo Akua Sena Dansua hajasema ni sheria zipi angetaka zibadilishwe, lakini watu wengi wamekuwa wakisema mwamuzi wa mchuano wa robo fainali kati ya Ghana na Uruguay angetakiwa kuipa Ghana goli, wakati mchezaji wa Uruguay Luis Suarez alipoondosha kwa mikono mpira uliokuwa unaingia kwenye lango la timu yake.
Kwenye mechi hiyo mshambuliaji wa Ghana Dominic Adiyah alipiga mpira kwa kichwa ukaeleka kuingia katika lango la Uruguay ukibakia muda mfupi sana kabla ya mechi kumalizika, lakini Suarez ambaye ni mchezaji wa ndani akauondosha kwa mikono.
Mwamuzi alimwonyesha kadi nyekundu Suarez na akawapa Ghana penati ambayo Asamoah Gyan alipiga nje.
Adhabu hiyo ni kulingana na sheria zilizopo za shirikisho la soka dunia FIFA.
Mechi ilimalizika kwa sare, ikalazimika kuingia mikwaju ya penalti na Uruguay wakaibuka washindi wa mabao 4-2.
Ghana ilikuwa timu ya Afrika kufikia hatua ya robo fainali katika Kombe la Dunia.
Baada ya kurejea nyumbani Black Stars walipokelewa kwa shangwe na nderemo mjini Accra.
Rais wa Ghana John Atta Mills alisema wachezaji hao watapewa tuzo za kitaifa na pia dola 20,000 kila mmoja.
Mashabiki wa soka kote barani Afrika waliishabikia Ghana wakati wa mchuano huo, na wengi walipigika sana baada ya Black Stars kuondolewa.
Ilikuwa ni timu pekee ya Afrika iliyobakia kwenye mashindano baada ya timu zingine tano za Afrika kuondolewa kwenye raundi ya kwanza ya michuano hiyo.

JIACHIE NA KAMERA YA DJ NASS


Katika Jiachie na camera ya Dj Nass hawa hapa ni washakaji wa kitaa nao waliamua kujiachia namna hiyo.

ARUSHA BARABARA HAKUNA


Kadri siku zinavyokwenda Mkoa wa Arusha unakabiliwa na ukosefu wa barabara hilo limebainika hasa pale inapofika mida ya Asubuhi na Jioni kunakuwepo na msongamano mkubwa sana wa magari.

July 6, 2010

Nass

Hii ni Blog Mpya Kabisa Ambayo bado ipo katika Maintenance ya muda mfupi tu.
baada ya muda itakuwa na vitu vya kutosha kabisa hasa hasa Burudani/michezo habari mbali mabali