Abel Rusheraa Motika, almaarufu – Mr Ebbo Enzi Za Uhai wake
MWIMBAJI nguli Tanzania aliyeibuka na staili ya bongofleva kwa ‘tune’
na staili ya Kimasai, Abel Rusheraa Motika, almaarufu – Mr Ebbo
amefariki dunia.
Habari za uhakika zilizolifikia Blog Hii alfajiri ya leo zinaeleza
kwa Mr. Ebbo alifariki kufuatia kusumbuliwa na ugonjwa wa Mshtuko Wa Moyo kwa
muda mrefu. Amefariki akiwa nyumbani kwa familia yake, maeneo ya Usa
River, Arusha.
Mwanamuziki huyo alifahamika zaidi kwa nyimbo zake zenye lafudhi ya
Kimasai, ikiwamo – Mi Mmasai Bwana, Kamongo na nyingine nyingi
zilizoteka uwanja wa muziki.
Pia alikuwa miongoni mwa wanamuziki walioinukia kwa kufanya ‘kolabo’ na
wanamuziki wengine, hasa wanaotoka Mkoa wa Tanga wakiwamo; Wagozi wa
Kaya.
Mipango ya mazishi inafanywa na familia yake na huenda akapumzishwa katika mashamba ya familia yake yaliyoko Usa River Mkoani Arusha .
Blog Hii Inatoa pole kwa dunia ya mashabiki wa muziki, marafiki, watoto, ndugu jamaa na marafiki.
KILA NAFSI ITAONJA UMAUTI, MUNGU AILAZE ROHO YAKE MALA PEMA PEPONI AMIN,