March 22, 2012

CLUB MAISHA MTWARA SASA IPO TAYARI KWA BURUDANI KWA WAKAZI WA MTWARA.

Usiku huu hapa Club Maisha Mtwara ndio matengenezo ya mwisho na tayari kwa show ya uzinduzi itakayopigwa Alhamis ya leo. Picha ya juu na chini inaonyesha lango kuu lakuingilia ambapo kutakuwa na Red Carpet ya nguvu na watu mbalimbali pamoja na wageni waalikwa watapita katika zulia hilo jekundu.

Muonekano wa Nje Ya Club Maisha Mtwara

HK akikagua machine ya DJ kama imekaa pole na tv ile pale pembeni itakuwa inakuonyesha nyimbo zitakazochezwa hapo zitakuwa nizile zenye video so unacheza mziki huku ukimtizama aliyeimba wimbo huo kwenye kideo. Mpewe nini tena watu wangu wa Mtwara??? Club ndio kwanza mpyaaaaaaaa

KUTANA NA KUNDI JIPYA LA MADJ "EXTREME DEEJAYZ"

DJ Majey Majizo 4 Shizo

DJ Park making it happen


Xtreme Top Notchs, DJ Park,DJ Majizo and DJ Spark

December 5, 2011

GWASUMA WAWAPAGAWISHA WASHABIKI WAKE ARUSHA KATIKA UKUMBI WA TRIPLE A CLUB


Mnenguaji Mahiri Wa Bendi Hiyo Suzi Akifanya Mambo yake

 Walikamua vilivyo
 wadada walijiaachia balaaaaaaaaaaaaa

Wanenguaje wakiwaburudisha Mashabiki
 Mpiga kinanda nae alikuwa anajaituma mbaya siku iyo yote hayo kuwapa raha wapenzi wa bendi ya gwasuma

SHOW YA EPIQ NATION - ARUSHA

Maandalizi Ya Show Ya Epiq Nation Jukwaa Likitengenezwa Mida Ya Asubuhi


Mafundi Mitambo Wakiweka Mambo sawa Kabla ya show Kuanza

Dj AD A.K.A Mafuvu Akiwa Na Mafundi Mitambo


Maandalizi kabla ya Showa Ya Epiq Kuanza

Ilikuwa Ni Mapema kabisa Asubuhi Majira ya saa 2:30 watu Tayari walisha Ingia Uwanjani Kusubiria Show

DJ AD A.K.A Mafuvu Ndio Aliyehusika Mwanzo Mwisho Katika 1 & 2 Katika Mashine

CMB Prezzo Kutoka Kenya Akiwa Kwenye Stage Alipoteza ile Mbaya

JCB Mwenyeji Wa Showa Ya Epiq Akiwa Na The Nondo Chid Benz

Hawa Ni dancers Wa mwanamuziki toka Nchini kenya Prezzoo

Dancers Wa Prezoo Toka Kenya


Mtu  Mzima Prezo Juu Ya Jukwaa Akifanya Mambo

Watu wakimshangilia Mwanmuziki ambae kwa sasa Anafanya vizuri Katika Anga ya Mziki ROMA MKATOLIKI

Kulikuwa na Nyomi ya Kutosha Ndani ya Uwanja wa Sheikh Amri Abeid katika show  Ya Epiq Nation

Msanii ROMA Akiwa Juu ya Jukwa

Prezoo & Dogo Janja
Baada ya Show Ilikuwa Ni Ku show Love na Camera ya Dj Nass Hapo Ni Prezzo & Dogo Janja na MC Wa prezooKushoro
Wasanii Kutoka Arusha Jambo Squad katika Ni Masani wa Kike Lady Fire 


December 2, 2011

MR. EBBO AFARIKI DUNIA

Abel Rusheraa Motika, almaarufu – Mr Ebbo Enzi Za Uhai wake
MWIMBAJI nguli Tanzania aliyeibuka na staili ya bongofleva kwa ‘tune’ na staili ya Kimasai, Abel Rusheraa Motika, almaarufu – Mr Ebbo amefariki dunia.
Habari za uhakika zilizolifikia Blog Hii alfajiri ya leo zinaeleza kwa Mr. Ebbo alifariki kufuatia kusumbuliwa na ugonjwa wa Mshtuko Wa Moyo kwa muda mrefu. Amefariki akiwa nyumbani kwa familia yake, maeneo ya Usa River, Arusha.
Mwanamuziki huyo alifahamika zaidi kwa nyimbo zake zenye lafudhi ya Kimasai, ikiwamo – Mi Mmasai Bwana, Kamongo na nyingine nyingi zilizoteka uwanja wa muziki.
Pia alikuwa miongoni mwa wanamuziki walioinukia kwa kufanya ‘kolabo’ na wanamuziki wengine, hasa wanaotoka Mkoa wa Tanga wakiwamo; Wagozi wa Kaya.
Mipango ya mazishi inafanywa na familia yake na huenda akapumzishwa katika mashamba ya familia yake yaliyoko Usa River Mkoani Arusha .
Blog Hii  Inatoa pole kwa dunia ya mashabiki wa muziki, marafiki, watoto, ndugu jamaa na marafiki.

KILA NAFSI ITAONJA UMAUTI,  MUNGU AILAZE ROHO YAKE MALA PEMA PEPONI AMIN, 

November 30, 2011

MAAFA YALIYOSABABISHWA NA MAFURIKO KARATU MKOANI ARUSHA .

 Baadhi ya magari yaliyokumbwa na mafuriko hayo.
Mfanyakazi wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), Augustino Masige, aliyekuwa akiendesha gari namba T573 AHW, akitoka Arusha kwenda Musoma, akisimama kando ya gari lake lililosukumwa na maji umbali wa mita 50 toka barabarani.




Lori la mizigo lenye namba T190 AKW lililokuwa limebeba mitambo ya kutengeneza barabara likitoka Engaruka kwenda Arusha likiwa limezama kwenye maji.

  Polisi walifika eneo la tukio na kufanya ukaguzi wa matukio hayo ya ajali.
Baadae polisi wakatoa idhini ya mwili wa Samweli kutolewa katika eneo ulipopatikana.

  Hivi ndivyo kipande hicho cha barabara kilivyomegwa na maji.
Wananchi wakishuhudia maafa yaliyosababishwa na mafuriko hayo.

Hakika maafa yatokeapo hukumba kila kiumbe hai katika jamii. Mbwa huyu si kuwa aliathirika na mafuriko hayo bali alionesha uzalendo wake wa kweli na kufika katika eneo la tukio na kuangalia mwenyewe kilichojiri.

Mwili wa marehemu Samweli Julius ambaye alikuwa ni msaidizi wa mitambo ya kutengeza barabara, ukiwa umenasa juu ya mti.

November 28, 2011

RAISI WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AWATUNUKU VYEO WANAFUNZI MAOFISA JESHI -MONDULI

Katikati Ni Rais Wa Jamuhuri Ya Muungano Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwetwe Kulia ni Mh. Raila Odinga




Mh. Jakaya Mrisho Kikwete  Akipita Mbele Akikagua Gwaride

Vikosi vikipita mbele ya amirin jeshi mkuu
Maofisa Wanafunzi  5o6 wa jeshi la wananchi waliokuwa wanachukuwa mafunzo ya muda mfupi ya kijeshi wametunukiwa Kamishina na Raisi wa jamuhuri wa muungano wa Tanzania Amiri jeshi mkuu,Muheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete sherehe zilizofanyikia katika chuo cha kijeshi cha Monduli kilichopo mkoani Arusha

Katika sherehe hizo jumla ya wanafunzi maofisa 69 ni wanawake na wanaume walikuwa ni wanafunzi maofisa 447  na katika wa maafisa hao walio waliopewa kamishana kuna maafisa wa fani mbalimbali ikiwemo Wauguzi ,walimu ,wanasheria ,Wahasibu pamoja na waandishi wa habari .
PICHA KWA HISANI YA www.woindeshizza.blogspot.com