July 12, 2011
SHOW LOVE NDANI YA TRIPLE A NIGHT CLUB
Picha juu Ni Wana Kibao tu wakila Bata _ Ndani Ya Triple A Night Club
picha zote Kwa Hisani ya Fullbata .com
June 24, 2011
MOPLUS NA JOHMAKINI WAKAMILISHA VIDEO YA XRAY

Moplus na JohMakini ndani ya video ya X-ray ilofanywa chini ya camera
za hoodpixx arachuga kwa uongozi wa producer/director DeFXtro,Track
inayopatikana ndani ya "babawa ukoo" Vol 1 album iiliyo kitaa tayari
kwa shillingi elfu tano za kitanzania holla @ +255 715 240 005
chek pia machiz wakizungumzia hiphop na mitaa inavobonga..
http://www.youtube.com/watch?v=qB0I9Xw9Nao
June 15, 2011
May 6, 2011
DOGO JANJA AZUNGUMZIA MUSIC NA SHULE
DOGO JANJA KATIKA POZI
Wiki hii namleta kwenu chalii anayekuja kwa kasi kwenye muziki wa kizazi kipya. Jina lake anaitwa Abdulaziz Chende lakini kisanii anafahamika kwa jina la Dogo Janja.Alizaliwa Arusha 1997 katika Hospitali ya Mount Meru. Alisoma Shule ya Msingi Unga Limited na kuhitimu mwaka 2010. Kwa sasa anasoma kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Makongo. Mengi zaidi kuhusu chalii huyu, ungana nami katika maswali kumi ambayo nilimuuliza.
NASS: Je, hapa Dar unaishi na nani na ni nani anayekulipia ada ya shule?
DOGO JANJA: Naishi na Madee na Tip Top Connection ndiyo wanaonilipia ada.
NASS: Ilikuwaje ukaingia katika familia ya Tip Top na wakaamua kugharamia elimu yako?
DOGO JANJA: Kwanza ifahamike kwamba, Madee siyo ndugu yangu ila alinikuta kwenye shoo Arusha akavutiwa na kipaji changu ndipo walipoamua kunichukua.
NASS: Umri wako bado ni mdogo, imekuwaje ukaingia kwenye fani hii mapema hivi?
DOGO JANJA: Nakumbuka nikiwa darasa la tatu mwalimu wa Somo la Stadi za Kazi alituambia kila mwanafunzi atunge wimbo na aimbe, mimi nilitunga wimbo unaohusu Ukimwi na nikaimba vizuri. Kuanzia hapo nikaanza kuimba muziki huku mwalimu huyo akiwa ananisaidia kwani na yeye alivutiwa na mimi.
NASS: Wazazi wako waliupokea vipi uamuzi wako wa kuingia kwenye muziki hasa ukichukulia kwamba wengi wanadhani muziki ni uhuni?
DOGO JANJA:Walikubaliana nami lakini wakaniambia ‘chonde chonde’ nisiache shule.
NASS: Je, wimbo wako wa kwanza kusikika uliitwaje?
DOGO JANJA: Ulikwenda kwa jina la ‘Sijafikia’ ambao kwa bahati mbaya ulisikika Arusha tu lakini mpaka sasa nina albamu moja inayokwenda kwa jina la Ngarenaro.
NASS: Mpaka sasa kuna mafanikio yoyote ambayo umeyapata kutokana na muziki?
DOGO JANJA: Yapo madogo madogo lakini kikubwa ni kwamba nimepata fursa ya kupata elimu bure.
NASS:Vipi kuhusiana na mchezo wa baba na mama, bado unaundeleza?
DOGO JANJA: Michezo hiyo nimeiacha kitambo, sasa niko ‘siriasi’ na masomo na muziki.
NASS: Hudhani kwamba muziki unaweza kukufanya ukashindwa kufanya vizuri darasani?
DOGO JANJA: Kwa hilo sidhani, ninachoamini ni kwamba naweza kufanya vitu vyote kwa wakati mmoja.
NASS: Ni matatizo gani ambayo umekuwa ukikumbana nayo kila siku?
DOGO JANJA: Ni ya kawaida tu, napambana nayo kuhakikisha hayaniharibii malengo yangu.
NASS: Nini matarajio yako ya baadaye?
DOGO JANJA: Ndoto zangu ni kuja kuwa mwanamuziki mkubwa wa kimataifa, naamini hilo litatimia tu.
Interview By Nass.
May 5, 2011
MASHINDANO YA MISS NJIRO YAPAMBA MOTO
Washiriki Wakiwa Kambini
Msanii wa kizazi kipya Barinaba anayetamba na kibao cha’ Milele’ anatarajia kupamba shindano la kumsaka mrembo wa kitongoji cha NJiro ambacho yanatarajia kufanyika kesho May 6 katika ukumbi wa Naura spring uliopo jijini hapa.
Akiongea na gazeti hili mratibu wa shindano hilo Upendo Simwita alisema kuwa nia ya kuandaa mashindano haya ni kumtamfuta mrembo wa kitongoji cha njiro ambacho kwa miaka mingi Hakijapata mrembo ambaye atawakilisha mkoa kwenye mashindano ya urembo .
“ Arusha kunavitongoji vingi na katika kitongoji ambacho kitaanda ni kimoja tu ambacho ni Arusha city cetre hivyo tume amua kuandaa ili kuwepo na vitongoji vingi ambavyo vitaandaa na kukutana pamoja ili kumpata mrembo ambaye atawakili mashindano haya kumsaka miss arusha ambaye mrembo huyo ataweza kuwakilisha vyema hata katika miss Tanzania na kuleta taji mkoani hapa”alisema Simwita.
Alibainisha kuwa jumla ya warembo 10 wanashiriki katika kinyanganyiro huko na kufafanua kuwa warembo wote ni wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya mkoani hapa na kusema kuwa anaamini kabisa mrembo ambaye atapatika katika mashindano haya atawakilisha vyema kitongoji katika mashindano ya mkoa na hata taifa.
Aliwataja warembo ambao watashiriki shindano hilo kuwa ni Tunu Mamuya (19),Zamda Idd(18),Winnie Mogiga(20),Sylivia Selvatory(20),Docas Geerad(20),Maria Hamed (19),Angela Deo(20),Stella Willson(20),Elizaneth Daimal(19) pamoja na Genovever Mike (20).
Alisema kuwa mshindi wa kwanza wa mashindano haya anatarajiwa kuondoka na kitita cha shilingi milioni moja huku mshindi wa pili akiondoka na shilingi laki mbili huku watatu akiwa anatarajia kuondoka na kitita cha shilingi laki moja .
Alifafanua kuwa wathamini ambao wamejitokeza tofauti na wathamini wakuu ambao ni Vodacom lakini pia kunawathamini wengine ambao wamejitokeza ambao ni ngorongoro consavesheni,mwandago investimenti, Triple A radio, Saumu Fasheni,saprini power veto ,Victoria investisheni pamoja na wenyeji ambao ni Naura spring hoteli.
‘’kingine pia warembo watano ambao watashinda watapata ajira kutoka katika hoteli hii ya naura spiring hoteli ambayo imeaamua kuchukua wasichana watano ambao watapewa kazi na mbali na hilo pia naura watakuwa pia na shindano la kumsaka mrembo wa hoteli yao”alisema Shimwita
Alisema pia barinaba anatarajia kusindikizwa wasanii wengine ambao ni pamoja na boda 2boda,ndanda Kosovo pamoja na wengine wengi.
“Napenda kutoa wito kwa wakazi wa mkoa wa arusha wajitokeze kwa wingi kushuhudia shindano hilo kwani warembo wa mwaka huu wa miss njiro ni wazuri sana”alisema Shimwita.
Habari na Picha Woinde Shizza
May 1, 2011
NORTHDWELLERS TOKA GOROSKANI-
Northdwellers,kundi la raia kibao wakiwemo upcoming hiphop toka arachuga moja pande za makao mapya wamekuwa kimya kwa muda toka na na majukumu kadhaa ikiwemo masomo vyuoni,ukimya huu umevunjwa na pini walorekod na kumshirikisha m2 mzima Banx katika kiitikio."Track tumeshaigongea kioo pande za hoodpixx chini ya defxtro,ambae pia ndo alitusukia audio noizmekah s2dioz arif,so saa yoyote video itakapotambulishwa tv stations ndipo 2takapo release audio ya "Dough fo sho",much love kwa fans we2 wote toka arachuga and tz mzima machalii zenu 2nakaza ile ilee,ngenge ngenge oooooooooooooi...
March 12, 2011
IZZ PACHA WA WATENGWA ACHOMWA KISU NA KUFARIKI DUNIA
Kwa Habari nilizozipata Leo zinasema kuwa msanii kutoka Watengwa Pacha Izz amefariki dunia usiku wa kuamkia leo maeneo ya Clock Tower kwa kupigwa kisu.
Inasemekana Izz alikuwa anatokea club Mawingu wakati anarudi home akakutana na machangu doa, inasemekana marehemu Izz aliongea nao na kuwaambia kwanini mnatukana tukana ovyo ndipo changu mmoja alipomchoma kisu ubavuni na kufariki hapo hapo.
Dada huyo alikamatwa na kupelekwa kituo cha police lakini cha kushangaza baada ya mama mzazi wa Izz alipoambia aliomba dada yule aachiwe huru kwa haraka hara haikufahamika kwa nini mama Mzazi wa Izz Ameamua kufanya hivyo.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEM MAHALI PEMA PEPONI. AMEN
March 7, 2011
MAELFU YA WATU KUTOKA SEHEMMU MBALI MBALI WAZIDI KUMIMINIKA KWA MCHUNGAJI - HUKO LOLIONDO
Maelfu ya watu wanazidi kumiminika katika wilaya ya Ngorongoro kata ya Digodigo katika kijiji cha Samunge huku baadhi yao wakiwa mahututi sana na wengine wakilazimika kupoteza maisha kutokana na msongamano wa watu na kuchelewa kupata huduma.
Wananchi hao ambao wametoka katika mikoa mbalimbali huku wengine wakitoka nchi za jirani ikiwemo nchi ya Kenya na Uganda wamemiminika katika kujiji hicho wengi wao wakiwa wanataka dawa kutoka kwa mchungaji mstaafu, Ambilikile Mwasapile, ambaye anatibu maradhi ambayo yanawasumbua kwa muda mrefu na ambayo walikuwa hawategemei kama wangekaa wapate dawa zake.
Pamoja ya kuwa watu wengi wanazidi kumiminika wilayani ngorongoro kupata matibabu kwenye nyumba ya mchungaji huyo lakini pia mamia ya watu wengine wamekwama jijini Arusha na katika eneo la Mto wa Mbu kutokana na kukosa usafiri wa kuweza kuwafikisha nyumbani kwa Mchungaji Mwasapile huku wengine waliofika katika nyumba ya Mchungaji huyo na kupata huduma wakiwa wanashindwa kurudi makwao kutokana na kukosa usafiri mara baada ya magari ambayo yaliwaleta kuondoka kutokana na kukaa muda mrefu.
Mbali na kuacha na magari pia maelfu ya watu ambao wanaenda kupata matibabu wengi wao wamekuwa wakipata shida sana kwa ajili ya malazi na chakula kwani wanalazimika kulala kwa muda mrefu kutokana na wingi wa watu wanao wakuta hali inayowasababishia wananchi hao kukaa kwa muda hata wa siku tano, na kuendelea na kulazimika kulala chini na wengine kupata chakula kwa njia ya shida sana hali ambayo inaleta hofu kubwa kwani watu wengi wanaofia magonjwa ya milipuko ambayo yanaweza tokea kutokana na msongamano huo wa watu wengi .
Pia katika msongamano huo wa watu umeleata madhara kwani pia kunabaadhi ya wagonjwa ambao wameletwa wakiwa mahututi wamefariki kutokana na kuchelewa kupata huduma mapema na mpaka kufikia Juzi watu saba walikuwa wamefariki dunia akiwemo mtoto mmoja.
Mwandishi wa habari hizi aliweza kushuhudia maiti hizo ambapo mbali na kushuhudia maiti hizo bado aliwaona wagonjwa wengi ambao walikuwa wameletwa kupata huduma huku wengine wakiwa wanaonekana kufika sehemu hiyo wakiwa na dripu mikononi na wengine wakiwa hawajiwezi kabisa.
Pamoja ya kuwa mchungaji Mwasapile alijitaidi sana kuhudumia wagonjwa ambao walifika sehemu hile lakini haikusaidia na hadi kufika jana jioni ilibidi waongeze wachungaji wengine wawili kumsaidi mchungaji huyu ili kuweza kupunguza watu kwani kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo wagonjwa wanazidi kumiminika zaidi .
Mchungaji Mwasapile alipoongea na gazeti hili alisema kuwa analazimika kufanya kazi kwa muda mrefu ili kuweza kuwahudumia wagonjwa ambao wanafika hapo na pia alibainisha kuwa ameoteshwa kuwa watu watu bado wanaongezeka na wanatoka katika nchi mbalimbali na mabara mbalimbali hali ambayo itafikia mahali hata itamgarimu mtu kuchukua hata wiki tano kupata huduma.
Mchungaji huyo alisema kuwa yeye Mungu alinena naye kwa njia ya ndoto kuhusiana na dawa hiyo inayotokana na mti aina ya Mugariga ambao ni chakula maarufu cha Twiga, tangu mwaka 1991 lakini alianza kutibu ugonjwa mmoja ambao ni wa ukimwi tu na ilipofika mwaka jana mungu alinena naye tena na ndipo alimwambia dawa hiyo inatibu pia hayo magonjwa mengine.
“na Mungu aliponiotesha aliniambia kabisa na mtu ambaye nitaanza kumtibu, na kweli alikuja mama mmoja wa hapa hapa kijijini na nikampa akapona baada ya mama huyo walikuja wanafunzi wawili pia niliwatibu nao wakapona na ndipo wakaanza kueneza na watu wakaja nikawapa na wamepona kabisa”alisema Mwasapile
Alisema kuwa dawa hii hainyweki mara mbili tiba yake ni mara moja tu na alisema kuwa kwa upande wa watu wenye ugonjwa wa HIV itawatibu baada ya siku 21 ambapo alifafanua kuwa akienda kupima mara ya kwanza ataonekana anavyo ,mara ya pili ataonekana anavyo yaani wiki ya pili na akienda wiki ya tatu ambayo itakuwa ni baada ya wiki 21 atakuwa hana kwa upande wa watu wenye kisukari alisema kuwa wao wanapona baada ya kunywa iyo dawa tu.
"Wanaopona HIV waache kujiingiza katika matendo ya kupata maambuki kwani hawatapona tena, Hii dawa sio kinga ni tiba na hairuhusiwi kunywa zaidi ya kikombe kimoja,"alisema Mchungaji Mwasapile.
Kwa upande wa msaidizi wa mchungaji huyo(Babuu), Marko Nedula alisema kuwa watu wengi wanaofika kupata huduma kwa mchungaji huyo wanatoka nje ya wilaya ya Ngorongoro pamoja na wenyeji ambapo alifafanua kuwa awali wenyeji walikuwa wanazarau dawa hiyo na kusema kuwa hawamuamini lakini baada ya kuona wageni wengi wanajitokeza kwenda kunywa ndio na wao wameanza kujitokeza kwa wingi.
Pia alisema kuwa anapenda kuwasihi watu ambao wanawaleta wagonjwa wao kujitaidi kuwaleta wagonjwa wakiwa angalau wananafuu kwa kiasi na wasiwachukuwe wagonjwa wao hospitali wakiwa mahututi kwani kwa sasa ivi msongamano wawatu umezidi hali ambayo inafanya kuchelewa kuwahudumia .
”unajua napenda kuwaambia wasiwachukuwe wagonjwa wao wakiwa mahututi kwani ndo inaweza kuwasababishia madhara ikiwemo wakiwaleta hapa wanaweza kuwapoteza kwani wakija wanakuta kunawagonjwa wengine wamekuja na niwagonjwa zaidi hadi huduma kuwafikia itachukuwa mda kitu ambacho kama alimchukuwa mgonjwa mahututi hospitalini anaweza kupoteza maisha na kama wata wachukuwa basi wabebe dawa ambazo zitawasaidia hadi pale mchungaji atakapo wafikia kuwapa huduma.
Pia gazeti hili lilibahatika kuzungumza na mmoja wa wanakijiji wa kijiji hicho aliyejulikana kwa jina la Ana Mateyo ambaye yeye alisema kuwa wamefurahia sana dawa hiyo kupatikana katika kijiji chao kwani wamekuwa wakifanya biashara kwa kasi kubwa mno na kusema kuwa wamekuwa wakipata hela kwani soda tu wamekuwa wakiuza shilingi 1000 huku maji ya kunywa wakiwa wanauza shilingi 2000.
Alisema kuwa pia wamefurahia sana kwani hata wao wenyewe kupitia babu huyo wanaweza kujikwamua katka maisha magumu kwani wanajiingizia kipato kila siku na wanafanya biashara kwa kiasi kikubwa sana.
Kwa upande wa mgonjwa mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Maramu Juma alisema kuwa yeye anafurahi sana kwani alifika Ngorongoro akiwa anaumwa na amebebwa lakini tangu anywe iyo dawa amesimama mwenyewe na anatembea kitu ambacho amemshukuru Mungu kwa kumleta mtumishi huyu katika nchi ya Tanzania.
Mbali na wagonjwa ambao walihudhuria katika kujiji hicho waliomba jeshi la polisi mkoani Arusha kuongeza askari wa kutuliza gasia ambao wataweza kuwapanga watu na kuwaelekeza kufuata utaratibu uliowekwa ili kuweza kusaidia vurugu zisitokee.
Walisema kuwa mgambo ambao wapo katika eneo hilo hawawezi kutosha kutuliza vurugu hizo kwani jinsi siku zinavyozidi kwenda ndivyo wananchi wanavyozidi kuongezeka na wakija wale waliochelewa huleta fujo na kutaka kuanza kupewa dawa wao badala ya wale walio tangulia.
“tunaomba jeshi la polisi liongeze idadi ya askari waweze kusimamia utaratibu kwani muda mwingine babu anashindwa fanya kazi kutokana na vurugu unakuta mtu amekuja hapa leo na kuna mungine kaja juzi yule wa leo ataki kufuata utaratibu uliowekwa analeta fujo kitu ambacho kinaleta ata uvunjifu wa amani “alisema mmoja wawagonjwa aliyejulikana kwa jina la Godfrey Lymo.
Picha Na Story Kwa Hisani Ya www.woindeshizza.blogspot.com
March 2, 2011
DOGO JANJA APIGWA NA MWALIMU KOSA .. HILO HAPO CHINI
wiki iliyopita msanii mdogo kuliko wote Bongo, Abdul Azizi (Dogo janja) alipokea kipigo cha ngumi mateke pamoja na mtama kutoka kwa mwalimu wake wa shule aliyopo (Makongo high school).kwa maelezo ya dogo janja ni kuwa alikuwa akiongea na wanafunzi wenzake kabla ya kuskia mtu akimuita "Dogo Jinga mjoo hapa" kumtizama akaona ni mtu tu asieyenamuonekano wa uwalimu amevaa mlegezo ndipo akamjibu "Kubwa jinga nakuja" ndipo mwalim huyo alipomsubiri wakati wa paredi na kumfanyia mbaya.
SWALI LA KUJIULIZA JE NI SAWA KWA MWALIMU KUMPIGA MWANAFUNZI MATEKE & NGUMI???
February 28, 2011
Mo Plus ft Gnako - Request Line
Mwanahiphop mkongwe toka 009 a.k.a. ungalimited" pande za Arusha anayekwenda kwa jina "MoPlus" anakuja na album yake ya "baba wa ukoo" hivi karibuni itakayosheheni mapini zaidi ya kumi na nne alorekodia katika studios mbalimbali nchini ikiwemo banjo records,watengwa records,noizmekah studios,TGP records na studio zinginezo nyingi pamoja na ushirikiano alliofanya na artists wenzake akiwemo Papaya,JCB,Banx,Gnako,Pain,Frost,Nick wa pili,Narx,Chindo,Isaya,Chaba na Joh Makini....single zitakazotoka kwa ajili ya utambulisho wa "BABA WA UKOO" ni hii ya "request line" aliyoshirikiana na Gnako,Niko strong alopiga na Isaya pamoja na "X-RAY alorekodi na joh makini pale noizmekah...
Mo anasema "nimeshoot video ya "nipo strong" na ipo tayari kwa usambazaji na nipo katika harakati za kufunga album yangu ili niizindue ntakaposhoot video ya "x-ray" na joh makini kwa hivyo fans wangu wajiset tayari kupokea album hii muda si mrefu"
Subscribe to:
Posts (Atom)






































