February 15, 2011

JOH MAKINI AFIWA NA MDOGO WAKE ANAEITWA GEORGE - JIJINI ARUSHA

Taarifa nilizozipata ni kuwa mdogo wake na Joe Makini anaeitwa George amefariki dunia leo hii akiwa Arusha, George ni kijana na alikuwa amemaliza form four,ndie aliekuwa akimfata Nikki wa pili ki umri.Blog Ya Dj Inatoa Pole kwa familia nzima ya joe makini, ndugu jamaa pamoja na marafiki.MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI alifariki kwa sababu Gani?.... Soon Utaipata taarifa Kutoka hapa hapa kaatika blog makini ya Dj Nass

January 28, 2011

DOGO JANJA AANZA SHULE

Katiaka Picha hapo juu Ni Mwanamziki/Student(Mwanfunzi) Dogo Janja wa shule ya Makongo High School Iliyoko Jijini Dar es salaam Dogo Kashaanza School Tangu Tar 3/January/2011 kama onavyo onekana katika Picha hapo juu akiwa amevalia Sare zake za Shule (Uniform). Kwa sasa Dogo amesema Yupo Kishule Zaidi muziki amesimama kidogo. Bolog Ya Dj Nass Inakutakia Kila Lakheri katika masomo Na mafanikio Mema Amiin.

January 13, 2011

MAELFU WAJITOKEZA MAZISHI YA WAFUASI WA CHADEMA WALIO UWAWA NA POLICE KATIKA VURUGU ZILIZOTOKEA JAN 5 ARUSHA

Pichani juu na Wafuasi wa Chadema wakiwa wamebeba majeneza ya vijana wawili waliouwawa na polisi mkoani Arusha mapema wiki hii. Ibada ya kuwaombea marehemu ilifanyika katika uwanja wa NMCJana na kuhuduriwa na maelfu ya wakazi wa jijini Hapa.

January 10, 2011

WALIOKUFA KATIKA VURUGU ZA ARUSHA KUAGWA KATIKA UWANJA WA NMC

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeamua kuwazika watu wawili kati ya watatu waliokufa kwa kupigwa risasi wakati polisi walipokuwa wakijaribu kutawanya umati wa wafuasi wa chama hicho wiki iliyopita. Chadema inaandaa shughuli za kutoa heshima za mwisho katika uwanja wa NMC keshokutwa, uwanja ambao ulitumiwa na chama hicho kwa ajili ya mkutano wake wa hadhara siku kulipotokea machafuko, Januari 5 mwaka huu. Katika uwanja huo ndipo walipokubaliana kukutana baada ya maandamano yaliyokataliwa na Polisi na ndipo Katibu Mkuu wa Chadema, Willibrod Slaa aliposhawishi wananchi kwenda kuvamia kituo cha Polisi, ili kuwatoa kwa nguvu baadhi ya viongozi wa chama hicho waliokuwa wakihojiwa. Viongozi hao ni pamoja na mke wa Dk. Slaa, Josephine Mushumbusi, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Mbunge wa Rombo, Sebastian Selasini, Mbunge wa Viti Maalumu, Lucy Luwenya na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Arusha, Derick Magoma, gharama za maziko hayo ikiwa ni pamoja na jeneza, sanda na mahitaji mengine yote muhimu vitabebwa na chama hicho. Magoma alisema jana mjini hapa kuwa viongozi wa juu wa Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe wameshakwenda nyumbani kwa marehemu na kueleza azma ya chama hicho kugharimia kila kitu katika msiba huo. Maiti za wafuasi hao, Denis Mtui atakayezikwa Rombo mkoani Kilimanjaro na George Waitara atakayezikwa Usa River, watabebwa katika majeneza na magari yaliyopambwa kwa bendera za chama hicho na kwenda katika uwanja huo tayari kwa ajili ya utoaji wa heshima za mwisho. Mwenyekiti huyo aliwataka wananchi wa Mkoa wa Arusha na mikoa ya jirani kuja siku hiyo kuomboleza na kuaga miili hiyo na kufafanua kuwa utaratibu unaandaliwa kuishirikisha Polisi. Baada ya kumalizika shughuli ya kuaga maiti hao, Magoma alisema kutakuwa na msafara wa magari kwenda nyumbani kwao kwa ajili ya maziko. Kuhusu mwili wa Poul Kahele, raia wa Kenya mwenye kitambulisho cha uraia namba 25066938, Magoma alisema utaratibu unaandaliwa na uongozi wa juu wa chama kuangalia namna maiti huyo atakavyosafirishwa kwenda nchini kwao. Naye Frank Leonard, anaripoti kutoka Iringa kwamba wabunge wa chama hicho wamepanga kufanya maandamano kulaani hatua zilizochukuliwa na vyombo vya dola mkoani Arusha wakati wa kutawanya maandamano ya chama hicho. Wakizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, wabunge hao Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini) na Chiku Abwao (Viti Maalumu mkoa wa Iringa), walisema watapeleka taarifa Polisi na kama itakataliwa wametishia kufanya maandamano hayo kwa lazima. Akizungumzia matukio hayo ya Arusha, Mchungaji Msigwa alisema yanakiuka kwa makusudi haki za binadamu na uvunjifu wa demokrasia ndani ya nchi. Aliwataka wakazi wa Mkoa wa Iringa kujitokeza kutoa michango itakayowezesha majeruhi wa maandamano hayo kupata matibabu ya uhakika. Alisema michango hiyo inaweza kupitia moja kwa moja katika Ofisi ya Mbunge mjini Iringa na itawasilishwa kwa wahusika kwa uwazi ili iwasaidie. Alisema wabunge wote wa Chadema wanaendelea na michango yao na mpaka jana zaidi ya Sh milioni sita zilikuwa zimepatikana. Tayari Serikali kupitia Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, imetangaza nia ya kutafuta mpatanishi ili kukutanisha makundi hasimu na kurejesha amani na mshikamano mkoani Arusha.

January 5, 2011

POLISI WAZUIA MAANDAMANO YA CHADEMA - MABOMU YA MACHOZI YACHUKUA NAFASI KUWATAWANYA RAIA

www.
H
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa mjini Arusha jana. Viongozi wa juu wa Chadema wamekamatwa wengine wamejeruhiwa vibaya, akiwemo mchumba wa Dk. Slaa, Bi Josephine (pichani juu). Picha za juu zinajieleza zenyewe jinsi gani mji wa Arusha jana uligeuka na kuwa Ukanda wa Gaza wa Palestina.

January 2, 2011

HAPPY NEW YEAR MA PEOPLE

LYRICS YA WIMBO ANAJUA BY ABDUL (DOGO JANJA)ft TUNDA MAN& MADEE




Intro-Madee
Yoo madee yooo hellow captian tunda man wa tip mchukue dogo huyo
mpigie chours nini dogo achane anajua or right

Chors-Tunda Man
Anajua ndo maana tumemchukua,akuna asiyejua kama dogo anajua,dogo
janja toka tip,mtoto mwenye bidii anakipaji unamkubali sema aahh,

Vers1-Dogo Janja
Kimbiza kinyama,mpaka maboya wanahema,
hakuna kuhanya,tunawameza tunawatema.
wataipatapata,fresh ya mwaka mpaka watatetemeka
kuona obey na mecca tuko full mzuka,
Magoro,mianzi up to ngarenaro,
Masoro,wameishiwa aidia wanatuberoo,, yeroo,
Sasa sisi za kiwilisniper,hakuna kugwaya viveMpaya
Tunachana mbaya like stopper ra wa fire
Dogo janja mimi,
Kachaa wa ungalim,
Sirushagi ngumi,
Nawachapa tu na ulimi,
Kwa michano kichomi kama ulikuwa unisomii,
Dogo janja sikwamii,
A.town hustler army,
Tupo japo atuvumi,
A.town sio miami,
Dogo janja kamanda,
Like coplo ndamanga,watoto wa mama leo tunawavisha kanga,

Chours-Tunda Man

Vers 2-Dogo Janja
Nazidi kupanda navuta na muda nazidi kimbiza na wida na shada nazidi kuvuta,
Nipe kipaza nipate kumeck makaki,
Nishike ni mic bunduki,
Napo kwenda ni mbali cha kushaangaza sifikii napiga push up,kuchana hip hop,
Nikama ni demu sitaki kunyapu,
Napiga sitaki kubip,
Watoto wa mama tunawavisha kapu yoo,sipigi masiga kiniger,wanajiona ma
hard core uku wakati wanaiga,na wale watoto wa mama wanaiga maskio
kutoga,a.town tutawamega viboga,
Kibaka kakaba kahaba kaiba mkoba katika mkoba kakuta kiroba kakuta
kizoba kakuta ratiba msiba hehehe uyoo kakuta ratiba msiba,,

Chours Tunda Man

Out-Dogo Janja

Heloow poeple au sio bana bana dogo janjaroo toka mkoa wa
killimanjaro, hehe ausio bana hamna dogo anaeza kuchana kama mimi
hakuna hakuna mi mkali inaeleweka unaona mpaka na cheka hahahaha
pamoko au sio mapaiya,tajir wa mahaba toka manza bey tanga casim
mganga na tane luzaaaaa haha watazima fegii mkali

December 16, 2010

JCB KUMVISHA PETE MCHUMBA WAKE



Mwana Hip Hop Wa A town JCB Ikiwa leo anasherehekea siku yake ya kuzaliwa, mtu mzima JCB majira ya saa 11 jioni hivi Hapa Arusha sehemu moja inayoitwa Pentagoni karibu na shule ya Kimandolu ndio atamvalisha pete mchumba wake Diana (Mzungu) anayeonekana kwenye picha.
Happy B,day bro na pia mafanikio mema katika maisha yenu mtakayoishi huko mbeleni hadi mfikie hatua ya kufunga pingu za maisha. One

By Dj Nass - A town

December 5, 2010

DOGO JANJA AACHIA VIDEO YA ANAJUA.



DOGO JANJA

CHIPUKIZI wa hip hop toka kundi la Tip Top Connection, Dogo Janja ameachia video ya wimbo wake 'Anajua' katika vituo vya televisheni hapa nchini, video hiyo imetayarishwa na kampuni ya Emptysoulz. Nadani ya nyimbo hiyo akimshirikisha Tunda Man Kutoka Tip Top Pamoja na Madee. Na hivi Karibuni nilifanya interview Na Blog Hii na kusema kuwa hivi karibuni Ataachia Pini Jingine ambayo ndani yake kamshirikisha Mwamba wa Kaskazini Joh Makini ngoma hiyo hapo itakwenda kwa jina la "Tulia" Amabyo Kaifanya kwa P Fank Majani Itaajiwa Muda wowote hewani toka sasa.

November 22, 2010

DOGO JANJA TRACK FT TUNDA MAN & MADEE (ANAJUA)

KAZI ZA DOGO JANJA KATIKA SAFARI YAKE YA MUSIC




dogo janja

Abudalazizi Chende aka Dogo Janja msanii mdogo sana mwenye kipaji kikubwa cha kuimba, anayekuja kwa kasi ya ajabu katika fani ya muziki chini ya wakali wa Tip Top connection.

Dogo Janja leo aliongea na Mimi kwa njia ya simu Kutoka jijini Dar es Salama na kusema kuwa tayari ameshatoa singo moja ya 'Anajua' aliyemshirikisha Tunda na Madee ambayo kwa sasa inapigwa katika vituo vya redio hapa nchini, ambayo msanii huyo yuko mbioni kuifanyia video tayari kwa kuirusha hewani.Dogo anatarajia kutoa wimbo mwingine mpya 'Tulia' hivi karibuni akiwa amemshirikisha mkali wa rhymes, Joh Makini.

Dogo mwenye umri wa miaka 13 na tatu na alianza kuimba akiwa darasa la tatu baada ya mwalimu wa somo la Stadi za kazi kuwaambia kila mtu abuni kitu ambacho atafanya akatunga wimbo wa UKIMWI ambao uliweza kumshangaza mwalimu na wanafunzi wenzake hvyo wote kutambua kipaji cha dogo.

Msanii huyo alishiriki katika mashindano ya TAU yaliofanyika mwaka 2007 mjini Arusha akiwa darasa la tano na alibahatika kuwa mshindi wa kwanza na akiwa ndiye mwenye umri mdogo katika mashindano hayo, na kupata zawadi ya kurekodi nyimbo moja ya 'Sijafikia' ingawa haikuweza kutemba sana.

Dogo Janja anatarajia kuanza elimu yake ya sekondari mapema 2011 na amesema kuwa anatarajia kujikita na masomo zaidi kwani muziki ni kipaji ailichonacho na hakiondoki.

Blog ya Kali Kutoka Kanda ya Kaskazini Imempa shavu dogo, Big Up Yourself!

KUISIKILIZA TRACK YA DOGO -BOFYA HAPO JUU

Imeandaliwa Na Dj Nass -

November 20, 2010

NAKO 2NAKO "TUMEWAVALIA HATERS MAGWANDA"



NAKO 2 NAKO

"Nako 2 Nako soldiers 2mewavalia haters magwanda,na ni vita tu raundi hii",wasema machizi hawa wasanii wa hiphop wenye maskani yao pale ololoo a.k.a kaloleni arusha,na wamekamilisha video shoot ya track zao mbili chini ya kampuni ya Hoodpixx videos arusha,audio moja ikiwa ni "ndani ya nyumba" toka Bhitz na nyingine "kati kati" toka noizmekah pro arusha.kazi hizi zimetumia mazingira tofauti tofauti ya Atown,viwanja kama club AQ na Empire sports bar huku machizi na warembo kibao kuwapa support machiz wa "nako2nako" katika parts mbalimbali,video ya "kati kati" itatangulia kutimba media ikifatwa na "ndani ya nyumba" itayoachiwa mwezi baadaye,lord eyes asema "hatuwez ruhusu majembe yafie mahabusu,chama kubwa N2N sitakubali tu "kiseserere" hivi hivi (kuseserere-kuanguka)...na Gnako pia anawasisitizia washabiki wa n2n "kaeni macho kupata real ting'az toka kwa wakubwa wa kazi" huku Bou Nako a.k.a "ODINARI" awapa mashabiki na wadau wa hiphop uhakika wa vioo hivyo viwili walivyoshoot kutesa katika media kwa maana ni video mbili matata za madudez,makopo na mipini ya ukweli,huku anacheka,lord alimalizia kwa kusema "hatuwezi sema we are back!kwasababu ukweli ni kwamba we never left the building,nako 2 nako soldiers we battle hard!"..

November 11, 2010

KATIKA BUSTANI YA MALAVEDAVE: MAUMIVU YA KUACHANA WAKATI BADO MNAPENDANA JE UNAYAJUA ?


Ni jambo la kumshukuru Mungu kutukutanisha tena kupitia safu hii ambayo lengo lake kuu ni kuelimishana na kukumbushana juu ya mambo mbalimbali yanayogusa maisha yetu ya kimapenzi.

Wiki iliyopita nilizungumzia mada iliyokuwa inawagusa moja kwa moja wanawake na suala la kujirahisi kwa wanaume. Nilieleza namna ambavyo miili yao ina thamani kubwa kuliko wanavyofikiri.

Hivyo basi, wanaume ambao wanatakiwa kupata fursa ya kuichezea miili yao wawe wale ambao wamewapenda kwa dhati na mioyo yao imeridhia. Wasifanye hivyo kwa tamaa ya pesa ama kitu kingine.

Baada ya kugusia kidogo mada hiyo ya wiki iliyopita, leo nizungumzie jambo moja ambalo limekuwa likiniumiza sana na kujiuliza kwanini huwa linatokea. Wakati najaribu kupitiapitia mtandao, niliona waraka wa barua pepe ambayo dada mmoja alikuwa akimtumia mpenzi wake wa zamani. Naomba niuandike hapa chini kama ulivyo kabla ya kuendelea.

Kwako John, nilikupenda sana mpenzi wangu, nawe ulionesha mapenzi ya dhati kwangu lakini kwa kile kilichotokea ambacho siwezi kukiandika hapa, tuliachana wakati bado nakupenda. Wakati mwingine nahisi sikustahili kukuacha lakini hilo linakuja akilini mwangu nikiwa tayari nimefanya uamuzi.

Kurudi kwako tena nahisi hutanikubalia, nabaki nalia. Nakutakia maisha mema lakini jua nimekuacha wakati nakupenda.
Ni mimi Janeth.

Janeth anaumia kwa uamuzi aliochukua wa kuachana na mpenzi wake wakati bado walikuwa wanapendana. Yawezekana alifanya hivyo kutokana na hasira ama kasoro ambazo alizibaini kwa mpenzi wake. Labda nilizungumzie hili la kasoro za wapenzi wetu kama chanzo cha wengi kuachana wakati bado wanapendana.

Tuelewe kwamba, kila binadamu ana kasoro huku zikitofautiana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Kama ni mfuatiliaji mzuri wa safu hii utakumbuka niliwahi kuandika makala inayosema kuwa, tuvumiliane hasa tunapobaini kuwa wapenzi tulio nao wana kasoro fulani.

Wakati nikiandika hivyo, leo nalazimika kulizungumzia hili la namna ya kukabiliana na kasoro za wapenzi wetu kutokana na ushauri alioomba mmoja wa wasomaji wangu.

“Naitwa Rehema, nina mpenzi wangu ambaye tunapendana sana lakini miongoni mwa vitu ambavyo vinatufanya tusilifurahie penzi letu ni kasoro za kiuanaume alizo nazo. Ananipa kila ninachokitaka lakini tunapokuwa faragha mambo hayaendi.

“Imefika wakati amekuwa akitoa machozi na kunieleza kuwa, tatizo lake la kimaumbile (jogoo kutoamka) analishangaa kwani humjia anapokutana na mimi tu. Mwenyewe anadai aliyemfanyia mchezo huo ni mpenzi wake wa zamani. Nampenda lakini kasoro hiyo aliyo nayo mpenzi wangu inaniweka njia panda.”

Wapo watu wengi walio katika uhusiano usiokuwa na furaha kutokana na kasoro ndogo ndogo ama kubwa walizonazo wapenzi wao. Katika hili kwanza lazima tujue kwamba, hakuna binadamu aliyekamilika!

Leo hii unaweza kumuacha mpenzi wako kutokana na kutokuridhisha katika tendo la ndoa tu lakini ukaingia kwenye uhusiano na mtu mwingine ambaye yeye ni ‘mzuri’ faragha ila ni mlevi na mkorofi.

Ndiyo maana siku zote tumekuwa tukitakiwa kuzifanyia tathmini kasoro walizonazo wapenzi wetu kabla ya kuchukua hatua ya kuwaacha au uamuzi mwingine usiofaa.

Tufahamu kwamba, mapenzi ndiyo yanayotangulia, moyo wako unapompenda fulani hauangalii kasoro alizo nazo kwasababu moyo wenyewe unajua kuwa, kasoro alizonazo mtu haziuzuii kupenda.

Ndiyo maana leo hii unamkuta mwanamke yuko katika uhusiano na mwanaume mkorofi kupita maelezo lakini mwanamke huyo anakueleza kuwa, hawezi kumuacha kwakuwa moyo wake umependa. Anachokifanya ni kumvumilia ili kutokwenda kinyume na matakwa ya moyo wake.

Kwa mfano, mpenzi wako hayajui mapenzi! Hiyo ni kasoro kubwa ambayo wapenzi wengi wamekuwa wakiilalamikia. Mara ooh! Mpenzi wangu hayajui mambo, ni goigoi awapo uwanjani. Mara ooh! Mpenzi wangu akienda mzunguko mmoja tu hoi.

Sawa! Hayo ni mambo yanayokukwaza lakini ndiyo uchukue hatua ya kumuacha kweli? Sidhani kama utakuwa ni uamuzi sahihi na wale wanaowaacha wapenzi wao eti kwasababu wana kasoro fulani wanadhihirisha kutokuwa na mapenzi ya dhati.
Kasoro za wapenzi wetu haziwezi kuwa sababu sahihi za kuwaacha, kama moyo wako umempenda huyo uliye naye na yeye akaonesha kukupenda, kasoro alizo nazo zichukulie kama changamoto kwako.

Tambua kwamba unaweza kubahatika kuingia kwenye uhusiano na mtu ambaye hana kasoro kubwa za kukukwaza lakini akawa hana mapenzi ya kweli, matokeo yake akawa mtu wa kukuliza kila siku.

Cha msingi, unapokuwa katika uhusiano na mtu kwa muda fulani ni lazima utabaini kasoro alizo nazo lakini na yeye pia atakuwa amekusoma na kukujua vizuri. Kama kweli mnapendana, mnachotakiwa kufanya ni kuangalia njia sahihi za kukabiliana na kasoro zenu. Zifanyieni kazi, rekebishaneni, yatafutieni ufumbuzi matatizo yenu ili mwisho kasoro hizo zisije zikawafanya mkaachana wakati bado mnapendana kwani inauma sana.

Ni hayo tu kwa leo, tukutane tena hapa wiki ijayo.