
June 15, 2011
May 6, 2011
DOGO JANJA AZUNGUMZIA MUSIC NA SHULE
DOGO JANJA KATIKA POZI
Wiki hii namleta kwenu chalii anayekuja kwa kasi kwenye muziki wa kizazi kipya. Jina lake anaitwa Abdulaziz Chende lakini kisanii anafahamika kwa jina la Dogo Janja.Alizaliwa Arusha 1997 katika Hospitali ya Mount Meru. Alisoma Shule ya Msingi Unga Limited na kuhitimu mwaka 2010. Kwa sasa anasoma kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Makongo. Mengi zaidi kuhusu chalii huyu, ungana nami katika maswali kumi ambayo nilimuuliza.
NASS: Je, hapa Dar unaishi na nani na ni nani anayekulipia ada ya shule?
DOGO JANJA: Naishi na Madee na Tip Top Connection ndiyo wanaonilipia ada.
NASS: Ilikuwaje ukaingia katika familia ya Tip Top na wakaamua kugharamia elimu yako?
DOGO JANJA: Kwanza ifahamike kwamba, Madee siyo ndugu yangu ila alinikuta kwenye shoo Arusha akavutiwa na kipaji changu ndipo walipoamua kunichukua.
NASS: Umri wako bado ni mdogo, imekuwaje ukaingia kwenye fani hii mapema hivi?
DOGO JANJA: Nakumbuka nikiwa darasa la tatu mwalimu wa Somo la Stadi za Kazi alituambia kila mwanafunzi atunge wimbo na aimbe, mimi nilitunga wimbo unaohusu Ukimwi na nikaimba vizuri. Kuanzia hapo nikaanza kuimba muziki huku mwalimu huyo akiwa ananisaidia kwani na yeye alivutiwa na mimi.
NASS: Wazazi wako waliupokea vipi uamuzi wako wa kuingia kwenye muziki hasa ukichukulia kwamba wengi wanadhani muziki ni uhuni?
DOGO JANJA:Walikubaliana nami lakini wakaniambia ‘chonde chonde’ nisiache shule.
NASS: Je, wimbo wako wa kwanza kusikika uliitwaje?
DOGO JANJA: Ulikwenda kwa jina la ‘Sijafikia’ ambao kwa bahati mbaya ulisikika Arusha tu lakini mpaka sasa nina albamu moja inayokwenda kwa jina la Ngarenaro.
NASS: Mpaka sasa kuna mafanikio yoyote ambayo umeyapata kutokana na muziki?
DOGO JANJA: Yapo madogo madogo lakini kikubwa ni kwamba nimepata fursa ya kupata elimu bure.
NASS:Vipi kuhusiana na mchezo wa baba na mama, bado unaundeleza?
DOGO JANJA: Michezo hiyo nimeiacha kitambo, sasa niko ‘siriasi’ na masomo na muziki.
NASS: Hudhani kwamba muziki unaweza kukufanya ukashindwa kufanya vizuri darasani?
DOGO JANJA: Kwa hilo sidhani, ninachoamini ni kwamba naweza kufanya vitu vyote kwa wakati mmoja.
NASS: Ni matatizo gani ambayo umekuwa ukikumbana nayo kila siku?
DOGO JANJA: Ni ya kawaida tu, napambana nayo kuhakikisha hayaniharibii malengo yangu.
NASS: Nini matarajio yako ya baadaye?
DOGO JANJA: Ndoto zangu ni kuja kuwa mwanamuziki mkubwa wa kimataifa, naamini hilo litatimia tu.
Interview By Nass.
May 5, 2011
MASHINDANO YA MISS NJIRO YAPAMBA MOTO
Washiriki Wakiwa Kambini
Msanii wa kizazi kipya Barinaba anayetamba na kibao cha’ Milele’ anatarajia kupamba shindano la kumsaka mrembo wa kitongoji cha NJiro ambacho yanatarajia kufanyika kesho May 6 katika ukumbi wa Naura spring uliopo jijini hapa.
Akiongea na gazeti hili mratibu wa shindano hilo Upendo Simwita alisema kuwa nia ya kuandaa mashindano haya ni kumtamfuta mrembo wa kitongoji cha njiro ambacho kwa miaka mingi Hakijapata mrembo ambaye atawakilisha mkoa kwenye mashindano ya urembo .
“ Arusha kunavitongoji vingi na katika kitongoji ambacho kitaanda ni kimoja tu ambacho ni Arusha city cetre hivyo tume amua kuandaa ili kuwepo na vitongoji vingi ambavyo vitaandaa na kukutana pamoja ili kumpata mrembo ambaye atawakili mashindano haya kumsaka miss arusha ambaye mrembo huyo ataweza kuwakilisha vyema hata katika miss Tanzania na kuleta taji mkoani hapa”alisema Simwita.
Alibainisha kuwa jumla ya warembo 10 wanashiriki katika kinyanganyiro huko na kufafanua kuwa warembo wote ni wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya mkoani hapa na kusema kuwa anaamini kabisa mrembo ambaye atapatika katika mashindano haya atawakilisha vyema kitongoji katika mashindano ya mkoa na hata taifa.
Aliwataja warembo ambao watashiriki shindano hilo kuwa ni Tunu Mamuya (19),Zamda Idd(18),Winnie Mogiga(20),Sylivia Selvatory(20),Docas Geerad(20),Maria Hamed (19),Angela Deo(20),Stella Willson(20),Elizaneth Daimal(19) pamoja na Genovever Mike (20).
Alisema kuwa mshindi wa kwanza wa mashindano haya anatarajiwa kuondoka na kitita cha shilingi milioni moja huku mshindi wa pili akiondoka na shilingi laki mbili huku watatu akiwa anatarajia kuondoka na kitita cha shilingi laki moja .
Alifafanua kuwa wathamini ambao wamejitokeza tofauti na wathamini wakuu ambao ni Vodacom lakini pia kunawathamini wengine ambao wamejitokeza ambao ni ngorongoro consavesheni,mwandago investimenti, Triple A radio, Saumu Fasheni,saprini power veto ,Victoria investisheni pamoja na wenyeji ambao ni Naura spring hoteli.
‘’kingine pia warembo watano ambao watashinda watapata ajira kutoka katika hoteli hii ya naura spiring hoteli ambayo imeaamua kuchukua wasichana watano ambao watapewa kazi na mbali na hilo pia naura watakuwa pia na shindano la kumsaka mrembo wa hoteli yao”alisema Shimwita
Alisema pia barinaba anatarajia kusindikizwa wasanii wengine ambao ni pamoja na boda 2boda,ndanda Kosovo pamoja na wengine wengi.
“Napenda kutoa wito kwa wakazi wa mkoa wa arusha wajitokeze kwa wingi kushuhudia shindano hilo kwani warembo wa mwaka huu wa miss njiro ni wazuri sana”alisema Shimwita.
Habari na Picha Woinde Shizza
May 1, 2011
NORTHDWELLERS TOKA GOROSKANI-
Northdwellers,kundi la raia kibao wakiwemo upcoming hiphop toka arachuga moja pande za makao mapya wamekuwa kimya kwa muda toka na na majukumu kadhaa ikiwemo masomo vyuoni,ukimya huu umevunjwa na pini walorekod na kumshirikisha m2 mzima Banx katika kiitikio."Track tumeshaigongea kioo pande za hoodpixx chini ya defxtro,ambae pia ndo alitusukia audio noizmekah s2dioz arif,so saa yoyote video itakapotambulishwa tv stations ndipo 2takapo release audio ya "Dough fo sho",much love kwa fans we2 wote toka arachuga and tz mzima machalii zenu 2nakaza ile ilee,ngenge ngenge oooooooooooooi...
March 12, 2011
IZZ PACHA WA WATENGWA ACHOMWA KISU NA KUFARIKI DUNIA
Kwa Habari nilizozipata Leo zinasema kuwa msanii kutoka Watengwa Pacha Izz amefariki dunia usiku wa kuamkia leo maeneo ya Clock Tower kwa kupigwa kisu.
Inasemekana Izz alikuwa anatokea club Mawingu wakati anarudi home akakutana na machangu doa, inasemekana marehemu Izz aliongea nao na kuwaambia kwanini mnatukana tukana ovyo ndipo changu mmoja alipomchoma kisu ubavuni na kufariki hapo hapo.
Dada huyo alikamatwa na kupelekwa kituo cha police lakini cha kushangaza baada ya mama mzazi wa Izz alipoambia aliomba dada yule aachiwe huru kwa haraka hara haikufahamika kwa nini mama Mzazi wa Izz Ameamua kufanya hivyo.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEM MAHALI PEMA PEPONI. AMEN
March 7, 2011
MAELFU YA WATU KUTOKA SEHEMMU MBALI MBALI WAZIDI KUMIMINIKA KWA MCHUNGAJI - HUKO LOLIONDO
Maelfu ya watu wanazidi kumiminika katika wilaya ya Ngorongoro kata ya Digodigo katika kijiji cha Samunge huku baadhi yao wakiwa mahututi sana na wengine wakilazimika kupoteza maisha kutokana na msongamano wa watu na kuchelewa kupata huduma.
Wananchi hao ambao wametoka katika mikoa mbalimbali huku wengine wakitoka nchi za jirani ikiwemo nchi ya Kenya na Uganda wamemiminika katika kujiji hicho wengi wao wakiwa wanataka dawa kutoka kwa mchungaji mstaafu, Ambilikile Mwasapile, ambaye anatibu maradhi ambayo yanawasumbua kwa muda mrefu na ambayo walikuwa hawategemei kama wangekaa wapate dawa zake.
Pamoja ya kuwa watu wengi wanazidi kumiminika wilayani ngorongoro kupata matibabu kwenye nyumba ya mchungaji huyo lakini pia mamia ya watu wengine wamekwama jijini Arusha na katika eneo la Mto wa Mbu kutokana na kukosa usafiri wa kuweza kuwafikisha nyumbani kwa Mchungaji Mwasapile huku wengine waliofika katika nyumba ya Mchungaji huyo na kupata huduma wakiwa wanashindwa kurudi makwao kutokana na kukosa usafiri mara baada ya magari ambayo yaliwaleta kuondoka kutokana na kukaa muda mrefu.
Mbali na kuacha na magari pia maelfu ya watu ambao wanaenda kupata matibabu wengi wao wamekuwa wakipata shida sana kwa ajili ya malazi na chakula kwani wanalazimika kulala kwa muda mrefu kutokana na wingi wa watu wanao wakuta hali inayowasababishia wananchi hao kukaa kwa muda hata wa siku tano, na kuendelea na kulazimika kulala chini na wengine kupata chakula kwa njia ya shida sana hali ambayo inaleta hofu kubwa kwani watu wengi wanaofia magonjwa ya milipuko ambayo yanaweza tokea kutokana na msongamano huo wa watu wengi .
Pia katika msongamano huo wa watu umeleata madhara kwani pia kunabaadhi ya wagonjwa ambao wameletwa wakiwa mahututi wamefariki kutokana na kuchelewa kupata huduma mapema na mpaka kufikia Juzi watu saba walikuwa wamefariki dunia akiwemo mtoto mmoja.
Mwandishi wa habari hizi aliweza kushuhudia maiti hizo ambapo mbali na kushuhudia maiti hizo bado aliwaona wagonjwa wengi ambao walikuwa wameletwa kupata huduma huku wengine wakiwa wanaonekana kufika sehemu hiyo wakiwa na dripu mikononi na wengine wakiwa hawajiwezi kabisa.
Pamoja ya kuwa mchungaji Mwasapile alijitaidi sana kuhudumia wagonjwa ambao walifika sehemu hile lakini haikusaidia na hadi kufika jana jioni ilibidi waongeze wachungaji wengine wawili kumsaidi mchungaji huyu ili kuweza kupunguza watu kwani kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo wagonjwa wanazidi kumiminika zaidi .
Mchungaji Mwasapile alipoongea na gazeti hili alisema kuwa analazimika kufanya kazi kwa muda mrefu ili kuweza kuwahudumia wagonjwa ambao wanafika hapo na pia alibainisha kuwa ameoteshwa kuwa watu watu bado wanaongezeka na wanatoka katika nchi mbalimbali na mabara mbalimbali hali ambayo itafikia mahali hata itamgarimu mtu kuchukua hata wiki tano kupata huduma.
Mchungaji huyo alisema kuwa yeye Mungu alinena naye kwa njia ya ndoto kuhusiana na dawa hiyo inayotokana na mti aina ya Mugariga ambao ni chakula maarufu cha Twiga, tangu mwaka 1991 lakini alianza kutibu ugonjwa mmoja ambao ni wa ukimwi tu na ilipofika mwaka jana mungu alinena naye tena na ndipo alimwambia dawa hiyo inatibu pia hayo magonjwa mengine.
“na Mungu aliponiotesha aliniambia kabisa na mtu ambaye nitaanza kumtibu, na kweli alikuja mama mmoja wa hapa hapa kijijini na nikampa akapona baada ya mama huyo walikuja wanafunzi wawili pia niliwatibu nao wakapona na ndipo wakaanza kueneza na watu wakaja nikawapa na wamepona kabisa”alisema Mwasapile
Alisema kuwa dawa hii hainyweki mara mbili tiba yake ni mara moja tu na alisema kuwa kwa upande wa watu wenye ugonjwa wa HIV itawatibu baada ya siku 21 ambapo alifafanua kuwa akienda kupima mara ya kwanza ataonekana anavyo ,mara ya pili ataonekana anavyo yaani wiki ya pili na akienda wiki ya tatu ambayo itakuwa ni baada ya wiki 21 atakuwa hana kwa upande wa watu wenye kisukari alisema kuwa wao wanapona baada ya kunywa iyo dawa tu.
"Wanaopona HIV waache kujiingiza katika matendo ya kupata maambuki kwani hawatapona tena, Hii dawa sio kinga ni tiba na hairuhusiwi kunywa zaidi ya kikombe kimoja,"alisema Mchungaji Mwasapile.
Kwa upande wa msaidizi wa mchungaji huyo(Babuu), Marko Nedula alisema kuwa watu wengi wanaofika kupata huduma kwa mchungaji huyo wanatoka nje ya wilaya ya Ngorongoro pamoja na wenyeji ambapo alifafanua kuwa awali wenyeji walikuwa wanazarau dawa hiyo na kusema kuwa hawamuamini lakini baada ya kuona wageni wengi wanajitokeza kwenda kunywa ndio na wao wameanza kujitokeza kwa wingi.
Pia alisema kuwa anapenda kuwasihi watu ambao wanawaleta wagonjwa wao kujitaidi kuwaleta wagonjwa wakiwa angalau wananafuu kwa kiasi na wasiwachukuwe wagonjwa wao hospitali wakiwa mahututi kwani kwa sasa ivi msongamano wawatu umezidi hali ambayo inafanya kuchelewa kuwahudumia .
”unajua napenda kuwaambia wasiwachukuwe wagonjwa wao wakiwa mahututi kwani ndo inaweza kuwasababishia madhara ikiwemo wakiwaleta hapa wanaweza kuwapoteza kwani wakija wanakuta kunawagonjwa wengine wamekuja na niwagonjwa zaidi hadi huduma kuwafikia itachukuwa mda kitu ambacho kama alimchukuwa mgonjwa mahututi hospitalini anaweza kupoteza maisha na kama wata wachukuwa basi wabebe dawa ambazo zitawasaidia hadi pale mchungaji atakapo wafikia kuwapa huduma.
Pia gazeti hili lilibahatika kuzungumza na mmoja wa wanakijiji wa kijiji hicho aliyejulikana kwa jina la Ana Mateyo ambaye yeye alisema kuwa wamefurahia sana dawa hiyo kupatikana katika kijiji chao kwani wamekuwa wakifanya biashara kwa kasi kubwa mno na kusema kuwa wamekuwa wakipata hela kwani soda tu wamekuwa wakiuza shilingi 1000 huku maji ya kunywa wakiwa wanauza shilingi 2000.
Alisema kuwa pia wamefurahia sana kwani hata wao wenyewe kupitia babu huyo wanaweza kujikwamua katka maisha magumu kwani wanajiingizia kipato kila siku na wanafanya biashara kwa kiasi kikubwa sana.
Kwa upande wa mgonjwa mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Maramu Juma alisema kuwa yeye anafurahi sana kwani alifika Ngorongoro akiwa anaumwa na amebebwa lakini tangu anywe iyo dawa amesimama mwenyewe na anatembea kitu ambacho amemshukuru Mungu kwa kumleta mtumishi huyu katika nchi ya Tanzania.
Mbali na wagonjwa ambao walihudhuria katika kujiji hicho waliomba jeshi la polisi mkoani Arusha kuongeza askari wa kutuliza gasia ambao wataweza kuwapanga watu na kuwaelekeza kufuata utaratibu uliowekwa ili kuweza kusaidia vurugu zisitokee.
Walisema kuwa mgambo ambao wapo katika eneo hilo hawawezi kutosha kutuliza vurugu hizo kwani jinsi siku zinavyozidi kwenda ndivyo wananchi wanavyozidi kuongezeka na wakija wale waliochelewa huleta fujo na kutaka kuanza kupewa dawa wao badala ya wale walio tangulia.
“tunaomba jeshi la polisi liongeze idadi ya askari waweze kusimamia utaratibu kwani muda mwingine babu anashindwa fanya kazi kutokana na vurugu unakuta mtu amekuja hapa leo na kuna mungine kaja juzi yule wa leo ataki kufuata utaratibu uliowekwa analeta fujo kitu ambacho kinaleta ata uvunjifu wa amani “alisema mmoja wawagonjwa aliyejulikana kwa jina la Godfrey Lymo.
Picha Na Story Kwa Hisani Ya www.woindeshizza.blogspot.com
March 2, 2011
DOGO JANJA APIGWA NA MWALIMU KOSA .. HILO HAPO CHINI
wiki iliyopita msanii mdogo kuliko wote Bongo, Abdul Azizi (Dogo janja) alipokea kipigo cha ngumi mateke pamoja na mtama kutoka kwa mwalimu wake wa shule aliyopo (Makongo high school).kwa maelezo ya dogo janja ni kuwa alikuwa akiongea na wanafunzi wenzake kabla ya kuskia mtu akimuita "Dogo Jinga mjoo hapa" kumtizama akaona ni mtu tu asieyenamuonekano wa uwalimu amevaa mlegezo ndipo akamjibu "Kubwa jinga nakuja" ndipo mwalim huyo alipomsubiri wakati wa paredi na kumfanyia mbaya.
SWALI LA KUJIULIZA JE NI SAWA KWA MWALIMU KUMPIGA MWANAFUNZI MATEKE & NGUMI???
February 28, 2011
Mo Plus ft Gnako - Request Line
Mwanahiphop mkongwe toka 009 a.k.a. ungalimited" pande za Arusha anayekwenda kwa jina "MoPlus" anakuja na album yake ya "baba wa ukoo" hivi karibuni itakayosheheni mapini zaidi ya kumi na nne alorekodia katika studios mbalimbali nchini ikiwemo banjo records,watengwa records,noizmekah studios,TGP records na studio zinginezo nyingi pamoja na ushirikiano alliofanya na artists wenzake akiwemo Papaya,JCB,Banx,Gnako,Pain,Frost,Nick wa pili,Narx,Chindo,Isaya,Chaba na Joh Makini....single zitakazotoka kwa ajili ya utambulisho wa "BABA WA UKOO" ni hii ya "request line" aliyoshirikiana na Gnako,Niko strong alopiga na Isaya pamoja na "X-RAY alorekodi na joh makini pale noizmekah...
Mo anasema "nimeshoot video ya "nipo strong" na ipo tayari kwa usambazaji na nipo katika harakati za kufunga album yangu ili niizindue ntakaposhoot video ya "x-ray" na joh makini kwa hivyo fans wangu wajiset tayari kupokea album hii muda si mrefu"
February 20, 2011
February 15, 2011
JOH MAKINI AFIWA NA MDOGO WAKE ANAEITWA GEORGE - JIJINI ARUSHA
Taarifa nilizozipata ni kuwa mdogo wake na Joe Makini anaeitwa George amefariki dunia leo hii akiwa Arusha, George ni kijana na alikuwa amemaliza form four,ndie aliekuwa akimfata Nikki wa pili ki umri.Blog Ya Dj Inatoa Pole kwa familia nzima ya joe makini, ndugu jamaa pamoja na marafiki.MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI
alifariki kwa sababu Gani?.... Soon Utaipata taarifa Kutoka hapa hapa kaatika blog makini ya Dj Nass
January 28, 2011
DOGO JANJA AANZA SHULE
Katiaka Picha hapo juu Ni Mwanamziki/Student(Mwanfunzi) Dogo Janja wa shule ya Makongo High School Iliyoko Jijini Dar es salaam Dogo Kashaanza School Tangu Tar 3/January/2011
kama onavyo onekana katika Picha hapo juu akiwa amevalia Sare zake za Shule (Uniform). Kwa sasa Dogo amesema Yupo Kishule Zaidi muziki amesimama kidogo.
Bolog Ya Dj Nass Inakutakia Kila Lakheri katika masomo Na mafanikio Mema Amiin.
January 13, 2011
MAELFU WAJITOKEZA MAZISHI YA WAFUASI WA CHADEMA WALIO UWAWA NA POLICE KATIKA VURUGU ZILIZOTOKEA JAN 5 ARUSHA
Pichani juu na Wafuasi wa Chadema wakiwa wamebeba majeneza ya vijana wawili waliouwawa na polisi mkoani Arusha mapema wiki hii. Ibada ya kuwaombea marehemu ilifanyika katika uwanja wa NMCJana na kuhuduriwa na maelfu ya wakazi wa jijini Hapa.
January 10, 2011
WALIOKUFA KATIKA VURUGU ZA ARUSHA KUAGWA KATIKA UWANJA WA NMC
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeamua kuwazika watu wawili kati ya watatu waliokufa kwa kupigwa risasi wakati polisi walipokuwa wakijaribu kutawanya umati wa wafuasi wa chama hicho wiki iliyopita.
Chadema inaandaa shughuli za kutoa heshima za mwisho katika uwanja wa NMC keshokutwa, uwanja ambao ulitumiwa na chama hicho kwa ajili ya mkutano wake wa hadhara siku kulipotokea machafuko, Januari 5 mwaka huu.
Katika uwanja huo ndipo walipokubaliana kukutana baada ya maandamano yaliyokataliwa na Polisi na ndipo Katibu Mkuu wa Chadema, Willibrod Slaa aliposhawishi wananchi kwenda kuvamia kituo cha Polisi, ili kuwatoa kwa nguvu baadhi ya viongozi wa chama hicho waliokuwa wakihojiwa.
Viongozi hao ni pamoja na mke wa Dk. Slaa, Josephine Mushumbusi, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Mbunge wa Rombo, Sebastian Selasini, Mbunge wa Viti Maalumu, Lucy Luwenya na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Arusha, Derick Magoma, gharama za maziko hayo ikiwa ni pamoja na jeneza, sanda na mahitaji mengine yote muhimu vitabebwa na chama hicho.
Magoma alisema jana mjini hapa kuwa viongozi wa juu wa Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe wameshakwenda nyumbani kwa marehemu na kueleza azma ya chama hicho kugharimia kila kitu katika msiba huo.
Maiti za wafuasi hao, Denis Mtui atakayezikwa Rombo mkoani Kilimanjaro na George Waitara atakayezikwa Usa River, watabebwa katika majeneza na magari yaliyopambwa kwa bendera za chama hicho na kwenda katika uwanja huo tayari kwa ajili ya utoaji wa heshima za mwisho.
Mwenyekiti huyo aliwataka wananchi wa Mkoa wa Arusha na mikoa ya jirani kuja siku hiyo kuomboleza na kuaga miili hiyo na kufafanua kuwa utaratibu unaandaliwa kuishirikisha Polisi.
Baada ya kumalizika shughuli ya kuaga maiti hao, Magoma alisema kutakuwa na msafara wa magari kwenda nyumbani kwao kwa ajili ya maziko. Kuhusu mwili wa Poul Kahele, raia wa Kenya mwenye kitambulisho cha uraia namba 25066938, Magoma alisema utaratibu unaandaliwa na uongozi wa juu wa chama kuangalia namna maiti huyo atakavyosafirishwa kwenda nchini kwao.
Naye Frank Leonard, anaripoti kutoka Iringa kwamba wabunge wa chama hicho wamepanga kufanya maandamano kulaani hatua zilizochukuliwa na vyombo vya dola mkoani Arusha wakati wa kutawanya maandamano ya chama hicho.
Wakizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, wabunge hao Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini) na Chiku Abwao (Viti Maalumu mkoa wa Iringa), walisema watapeleka taarifa Polisi na kama itakataliwa wametishia kufanya maandamano hayo kwa lazima.
Akizungumzia matukio hayo ya Arusha, Mchungaji Msigwa alisema yanakiuka kwa makusudi haki za binadamu na uvunjifu wa demokrasia ndani ya nchi.
Aliwataka wakazi wa Mkoa wa Iringa kujitokeza kutoa michango itakayowezesha majeruhi wa maandamano hayo kupata matibabu ya uhakika.
Alisema michango hiyo inaweza kupitia moja kwa moja katika Ofisi ya Mbunge mjini Iringa na itawasilishwa kwa wahusika kwa uwazi ili iwasaidie.
Alisema wabunge wote wa Chadema wanaendelea na michango yao na mpaka jana zaidi ya Sh milioni sita zilikuwa zimepatikana.
Tayari Serikali kupitia Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, imetangaza nia ya kutafuta mpatanishi ili kukutanisha makundi hasimu na kurejesha amani na mshikamano mkoani Arusha.
January 9, 2011
January 5, 2011
January 4, 2011
January 2, 2011
LYRICS YA WIMBO ANAJUA BY ABDUL (DOGO JANJA)ft TUNDA MAN& MADEE

Intro-Madee
Yoo madee yooo hellow captian tunda man wa tip mchukue dogo huyo
mpigie chours nini dogo achane anajua or right
Chors-Tunda Man
Anajua ndo maana tumemchukua,akuna asiyejua kama dogo anajua,dogo
janja toka tip,mtoto mwenye bidii anakipaji unamkubali sema aahh,
Vers1-Dogo Janja
Kimbiza kinyama,mpaka maboya wanahema,
hakuna kuhanya,tunawameza tunawatema.
wataipatapata,fresh ya mwaka mpaka watatetemeka
kuona obey na mecca tuko full mzuka,
Magoro,mianzi up to ngarenaro,
Masoro,wameishiwa aidia wanatuberoo,, yeroo,
Sasa sisi za kiwilisniper,hakuna kugwaya viveMpaya
Tunachana mbaya like stopper ra wa fire
Dogo janja mimi,
Kachaa wa ungalim,
Sirushagi ngumi,
Nawachapa tu na ulimi,
Kwa michano kichomi kama ulikuwa unisomii,
Dogo janja sikwamii,
A.town hustler army,
Tupo japo atuvumi,
A.town sio miami,
Dogo janja kamanda,
Like coplo ndamanga,watoto wa mama leo tunawavisha kanga,
Chours-Tunda Man
Vers 2-Dogo Janja
Nazidi kupanda navuta na muda nazidi kimbiza na wida na shada nazidi kuvuta,
Nipe kipaza nipate kumeck makaki,
Nishike ni mic bunduki,
Napo kwenda ni mbali cha kushaangaza sifikii napiga push up,kuchana hip hop,
Nikama ni demu sitaki kunyapu,
Napiga sitaki kubip,
Watoto wa mama tunawavisha kapu yoo,sipigi masiga kiniger,wanajiona ma
hard core uku wakati wanaiga,na wale watoto wa mama wanaiga maskio
kutoga,a.town tutawamega viboga,
Kibaka kakaba kahaba kaiba mkoba katika mkoba kakuta kiroba kakuta
kizoba kakuta ratiba msiba hehehe uyoo kakuta ratiba msiba,,
Chours Tunda Man
Out-Dogo Janja
Heloow poeple au sio bana bana dogo janjaroo toka mkoa wa
killimanjaro, hehe ausio bana hamna dogo anaeza kuchana kama mimi
hakuna hakuna mi mkali inaeleweka unaona mpaka na cheka hahahaha
pamoko au sio mapaiya,tajir wa mahaba toka manza bey tanga casim
mganga na tane luzaaaaa haha watazima fegii mkali
December 16, 2010
JCB KUMVISHA PETE MCHUMBA WAKE

Mwana Hip Hop Wa A town JCB Ikiwa leo anasherehekea siku yake ya kuzaliwa, mtu mzima JCB majira ya saa 11 jioni hivi Hapa Arusha sehemu moja inayoitwa Pentagoni karibu na shule ya Kimandolu ndio atamvalisha pete mchumba wake Diana (Mzungu) anayeonekana kwenye picha.
Happy B,day bro na pia mafanikio mema katika maisha yenu mtakayoishi huko mbeleni hadi mfikie hatua ya kufunga pingu za maisha. One
By Dj Nass - A town
December 10, 2010
December 5, 2010
DOGO JANJA AACHIA VIDEO YA ANAJUA.

DOGO JANJA
CHIPUKIZI wa hip hop toka kundi la Tip Top Connection, Dogo Janja ameachia video ya wimbo wake 'Anajua' katika vituo vya televisheni hapa nchini, video hiyo imetayarishwa na kampuni ya Emptysoulz. Nadani ya nyimbo hiyo akimshirikisha Tunda Man Kutoka Tip Top Pamoja na Madee. Na hivi Karibuni nilifanya interview Na Blog Hii na kusema kuwa hivi karibuni Ataachia Pini Jingine ambayo ndani yake kamshirikisha Mwamba wa Kaskazini Joh Makini ngoma hiyo hapo itakwenda kwa jina la "Tulia" Amabyo Kaifanya kwa P Fank Majani Itaajiwa Muda wowote hewani toka sasa.
November 24, 2010
November 22, 2010
KAZI ZA DOGO JANJA KATIKA SAFARI YAKE YA MUSIC


dogo janja
Abudalazizi Chende aka Dogo Janja msanii mdogo sana mwenye kipaji kikubwa cha kuimba, anayekuja kwa kasi ya ajabu katika fani ya muziki chini ya wakali wa Tip Top connection.
Dogo Janja leo aliongea na Mimi kwa njia ya simu Kutoka jijini Dar es Salama na kusema kuwa tayari ameshatoa singo moja ya 'Anajua' aliyemshirikisha Tunda na Madee ambayo kwa sasa inapigwa katika vituo vya redio hapa nchini, ambayo msanii huyo yuko mbioni kuifanyia video tayari kwa kuirusha hewani.Dogo anatarajia kutoa wimbo mwingine mpya 'Tulia' hivi karibuni akiwa amemshirikisha mkali wa rhymes, Joh Makini.
Dogo mwenye umri wa miaka 13 na tatu na alianza kuimba akiwa darasa la tatu baada ya mwalimu wa somo la Stadi za kazi kuwaambia kila mtu abuni kitu ambacho atafanya akatunga wimbo wa UKIMWI ambao uliweza kumshangaza mwalimu na wanafunzi wenzake hvyo wote kutambua kipaji cha dogo.
Msanii huyo alishiriki katika mashindano ya TAU yaliofanyika mwaka 2007 mjini Arusha akiwa darasa la tano na alibahatika kuwa mshindi wa kwanza na akiwa ndiye mwenye umri mdogo katika mashindano hayo, na kupata zawadi ya kurekodi nyimbo moja ya 'Sijafikia' ingawa haikuweza kutemba sana.
Dogo Janja anatarajia kuanza elimu yake ya sekondari mapema 2011 na amesema kuwa anatarajia kujikita na masomo zaidi kwani muziki ni kipaji ailichonacho na hakiondoki.
Blog ya Kali Kutoka Kanda ya Kaskazini Imempa shavu dogo, Big Up Yourself!
KUISIKILIZA TRACK YA DOGO -BOFYA HAPO JUU
Imeandaliwa Na Dj Nass -
Subscribe to:
Posts (Atom)


















