October 1, 2010

JIACHIE NA CAMERA YA DJ NASS KATIKA MAHAFALI YA SHULE YA SEKONDARI KALOLENI

Dj Nass Katika Mitambo Nikihakikisha kila kitu Kipo Fresh





Add caption

MAHAFALI YA KIDATO CHA NNE 2010 KATIKA SHULE YA SEKONDARI KALOLENI - ARUSHA .

Mkuu Wa Shule ya Kaloloni rashid Munga akitoa Nasaha zake


Ilifika zamu ya wahitimu kuimba  hawa kuimba na hapa walikuwa wakiimba na kucheza wimbo wao mzuri kabisa wakitumia beat ya Waka waka ilikuwa Poa hiyo

Mezaa Kuu

Ilifika Zamu ya Kusomewa Risala



Wahitimu wa kidato cha Nne wakisikiliza kwa makini kabisa kwa yale waliokuwa wakihusiwa.



Mkuu wa Shule ya sekondari kaloleni Rashid Munga Akitoa Nasaha zake kwa wanafunzi wanahitimu na kwa wale wanobaki shuleni. akigusia sana sana swala zima la nidhamu.
hawa hapa walikuwa wakichana Mistari yao walifunika mbaya kabisha


Hawa ni ndugu jamaa Na Marafiki waliohudhuria Katika Mahafali ya kuhitimu Kidato cha Nne katika shule ya sekondari Kaloleni - Arusha

Katika Mahafali hayo Kulikuwa Na Mitindo Mbalimbali ya mavazi ambao wahitimu hao waliyaanda na huyu hapa alianza na Vazi la Kanga Ilikuwa Poa Hiyo.

Huyu Hapa yeye Alikuja Na Mavazi Ya Gereji

Ahmed (Mpemba)

Huyu hapo Anaitwa Ahmed (Mpemba) -  yeye alikuja na mavazi ya Kipemba alifunika vilivyo

Ilifika zamu ya wahitimu hawa kupokea gamba zao (Vyeti)

Mmoja wa wahitimu Akivishwa Taji Na Mama Yake Mzazi

Utaratibu wa Upokeaje Vyeti Uliendelea

Zawadi Pia hazikuwa Nyuma kutolewa

September 17, 2010

SHOW LOVE NA CAMERA YA DJ NASS

Dogo Janja Kachaa - Katika Pozi
Nass Pamoja Na Tunada man Tukishow Love Pamoja



Kachaa & Tunda Man

Kushoto Ni Mzee Mzima Nass Nikiwa Na Kichwa Kutoka Tip Top Tunda Man

Kushoto Ni Chege, Katikati Ni Bushoke na Kulia Ni Abdul Kachaa

September 7, 2010

JAMBO SQUAD

Hawa Ndio Jambo Squad Kutoka pande za Rchuga (Watoto wa Bibi)




 Ni Jambo Squad Kutoka Pande Arusha kwa sasa  wapo wanakamilisha album yao ndani ya studio za Grandmaster Records Arusha meneo ya Ngarenaoro,,ikiwa na nyimbo kama Ngastuka ambayo kwa sasa inaruka katikaTv na Radio  mbalimbali nchini pamoja na nchini Kenya,wakusindikiza,na shule yetu ambayo itafuata baada ya Ngastuka,album ya Jambo ipo katika hatua za mwisho na inatarajiwa kuingia mizungukoni soon..

September 6, 2010

TIMU YA YANGA KUKIPIGA NA AFC LEOPARD YA KENYA KATIKA UWANJA WA SHEIK AMRI ABEID -ARUSHA SEP 8

Picha  mratibu wa mchezo  wa kirafiiki baina ya timu ya Yanga ya jijini Dar es salaam na Timu ya AFC Leopard ya nchini Kenya George Wakuganda akiwa anaongea na waandishi wa habari katika ofisi ya chama cha mpira wa miguu mkoani Arusha iliyopo ndani ya uwanja wa Kumbukumbu za Sheikh Amri Abeidi mechi ambayo itachezwa septembar nane


Kampuni ya CXC Afrika imeandaa mchezo mmoja wa kirafiki wa kimataifa kati ya timu ya Yanga jijini Dar es salaam na timu ya AFC Leopard ya nchini Kenya mechi ambayo itachezwa September nane katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sheirk Amri Abeid jijini hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya chama cha mpira wa miguu mkoani hapa mratibu wa mchezo huo George Wakuganda alisema kuwa nia na madhumuni ya kuandaa mchezo huo ni kuwapa burudani wakazi wa mkoa wa Arusha pamoja na vitongoji vyake  kwa kuweza kuona mchezo wa kimataifa ambao wamekuwa wakizikosa kwa kipindi kirefu.

Alisama kuwa mbali ya kuwapa burudani wakazi wa Arusha pia mechi hii itakuwa ni fursa kwa wapenzi wa soka wa mkoa wa Arusha kuweza kuitambua na kuiona timu yao mpya ambayo imesheeni vipaji mbalimbali vya hapa nchini Afrika kwa ujumla na hata nje ya Afrika.

Alitaja baadhi ya wachezaji maarufu ambao watacheza katika mechi hizo na aliaanza na timu ya Yanga kuwa ni pamoja na Kenneth Assamoh,Ernest Boakye,Yew Berco,pamoja na Mawrbia Ivana Kzenevic.

Alibainisha kwa timu ya AFC Leopard kuwa kila mtu mtanzania anaifahamu na anajua ugumu wa timu za kenya na alisema kuwa ikumbukwe timu hii pamoja na Gormahia zilipotea kwa muda mrefu sana katika anga la soka na sasa zimerudi kwa nguvu mpya.

Alitaja viingilio vya mechi hii kuwa kwa upande wa jukwaa kuu kiingilio itakuwa shilingi 10000 huku mzunguko ikiwa ni shilingi elfu tatu tu na kuongeza kuwa wameamua kuweka kiasi hichi cha hela ili kila mtu aweze kushuhudia mechi hii.

Kwa upande wa katibu msaidizi wa chama cha mpira wa miguu mkoani hapa Jeradi Munisi alisema kuwa anawashukuru sana kampuni hii kwa kuwaletea mechi kubwa kama hii na kusema kuwa anawaomba watanzania wajitokeze kwa wingi kushuhudi mechi hii ili wathamini ambao wanaleta mechi kama hizi wasikate tamaa.

Alisema kuwa wao kama chama wanatarajia kuzipokea timu hizi zote kesho nawanawapongeza pia waandaaji kwa kuwapa kipaumbele na kuona kuwa uwanja wao unafaa kuleta mechi kama hizi kuchezewa hapa.

"tunawashukuru kampuni hii kwa kutuletea mchezo huu hapa kwani wakazi wa Arusha tumekuwa tunaambulia kuangalia izi timu katika tv  au ukitaka zaidi upande gari uende dar sasa tunashukuru sana wanatutia moyo na kutufanya tuone wanatujali "alisema Munisi

September 4, 2010

UZUSHI KUHUSU MADHARA YA MAWASILIANO YA SIMU

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewataka watumiaji wa simu za mikononi kupuuza ujumbe wa tahadhari ulioanza kusambazwa jana na watu wasiojulikana, ikisema kuwa ni uzushi.
Jana kulikuwa na aina mbili za taarifa za tahadhari zilizokuwa zikitumwa kwa wateja wa simu za mikononi. Ujumbe wa kwanza unasema: “Ukipigiwa simu kwa private no (namba binafsi). au ikiandika call kwa red colour (rangi nyekundu) usipokee, ni mionzi, utapalarize (utapooza) na kufa.
Imetokea Kenya watu wamekufa. Julisha ndugu na jamaa wote.” Ujumbe mwingine unawataka watumiaji wa huduma hiyo wasipokee simu yoyote watakayopigiwa kupitia namba 7888308001, 9316048121, 9876266211, 9888854137 na 9876715587.
Ujumbe huo unasema: "Namba hii inapigwa na rangi nyekundu, unaweza kupata brain damage (tatizo la ubongo) kwa kupokea simu.
Watu 27 walifariki mara tuu baada ya kupokea simu iliyopigwa kutoka katika namba hizo." Ujumbe huo ulisababisha watumiaji wa simu kuingiwa na wasiwasi na baadhi waliwasiliana na chumba cha habari cha Mwananchi Communications kutaka ufafanuzi wa suala hilo na wengine wakieleza hofu ya kupooza.
Hata hivyo, taarifa iliyotumwa na msemaji wa TCRA, Innocent Mungy ambayo imesainiwa na kurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo, Profesa John Nkhoma, inasema: “Ujumbe huo unatakiwa kupuuzwa kwa kuwa ni uzushi usuokuwa na ukweli wowote.” Kutokana na ujumbe huo kusambazwa kwa watu wengi, TCRA imesema hakuna ukweli na hivyo kuwataka wananchi kuupuuzia. "Mamlaka ya Mawasiliano inapenda kuwahakikishia wananchi kwa ujumla kwamba taarifa zinazoenezwa ni za uzushi na sio za kweli.
Wananchi wanaombwa kupuuza uzushi huo kwa kua hauna ukweli wowote," inasema taarifa hiyo ya TCRA.
Ilifafanua kuwa kutokanha na maendeleo ya sayansi na teknolojia, kuna tafiti nyingi zimefanyika sehemu mbalimbali duniani ambazo zimeonyesha kwamba kiwango cha mawimbi ya mawasiliano hakina madhara kwa afya ya binadamu. 
TCRA iliwataka wote kuendelea kuwa na imani na teknolojia mpya zikiwemo za mawasiliano ya simu, utangazaji na utumiaji wa kompyuta ambazo zinatumiwa ulimwenguni kote bila madhara yoyote. "Madhumuni ya Mamlaka ya Mawasiliano na watoa huduma za mawasiliano kwa ujumla ni kuwaletea wananchi wa Tanzania mawasiliano bora kwa kujenga miundombinu, kutoa huduma bora na matumizi mema," inasema sheemu ya taarifa hiyo.
Mmoja wa watumiaji wa simu za mkononi, Frank Kimboyi ambaye naye alitumiwa ujumbe huo, alisema mwanzoni alipata wasiwasi mkubwa. "Baada ya kuupokea kidogo nilishituka, lakini baada ya kukaa na kutafakari uwezekano wa kitu kama hicho kutokea niliona ni mdogo na nikaamua kuupuuzia," alisema Kimboyi.

September 3, 2010


September 2, 2010

MJUE ZAIDI DJ MWENYE UMRI MDOGO KULIKO WOTE KATIKA JIJI LA TANGA

Dj Bob Nass Akiwakatika 1&2 Kisababisha Vilivyo
Dj Bob Nass Akifanya vitu vya ukweli ukweli

Jina lake kamili ni Nasr Thabit  wengi wanapenda kumuita Dj Bob Nass yupo Katika radio   Breez fm  ya Tanga  ni producer na dj.pia na ni mtangazaji wa kipindi cha flashback Siku ya  juma2 kuanzia saa 4 asubuhi mpaka 7 mchana
Na Huwa Anafanya kipindi cha mchana kinachoitwa  Track to Track Ni Kipindi ambacho Kinaanzia mida ya  saa 8 mpaka kumi jion kila siku  Ni Dj ambaye anapokuwa  ndani ya vipindi vyake lazima utavutiwa na vitu anavyovifanya

UBISHI WA KUFA MTU . HAWA JAMAA NOMA

Wapenda ligi watatu walibishana kuwa nani amekubuhu kwa ubishi kati yao. Wakaamua kila mmoja ahadithie ubishi wa haja alomfanyia mkewe
ili wapime nani kubobea zaidi kwenye hiyo fani.

Mbishi 1 akasema:
Mi siku moja nilivyokuwa nje ya nchi nilimpigia SIMU usiku mke wangu. Akapokea simu hakusema haloo...
Kulaleki  !!! na mimi nikakaa kimya sikuongea mpaka alfajiri wakati simu ilikuwa wazi.

Mbishi 2 akatia:
Mbona hiyo cha mtoto, mi siku moja nimerudi home nikagonga mlango mke wangu akaufungua lakini hakusema karibu mume wangu, aliniangalia tu.
Nikaona analeta madharau !!!
Sikuingia ndani nikasimama hapo hapo mlangoni mpaka asubuhi...huyoo nikatimua zangu job.

Mbishi 3 akaunganisha:
Hiyo nayo mbona cha mtoto tu, mi mke wangu tulipooana alikuwa anaona
haya kunigusa...ananidengulia eti  !!!
Na mimi sikumgusa na mpaka leo hatugusani.

Mbishi 1 na 2:
Aaaaaaaah FAZA acha usanii huo, nyie si mna watoto wawili ?
 
Mbishi 3:
Na hao watoto sijamuuliza kawaokota wapi... kwani mi nataka mchezo !!!.

Wazee nani anaweza kubishana na hawa jamaa?