September 17, 2010

SHOW LOVE NA CAMERA YA DJ NASS

Dogo Janja Kachaa - Katika Pozi
Nass Pamoja Na Tunada man Tukishow Love Pamoja



Kachaa & Tunda Man

Kushoto Ni Mzee Mzima Nass Nikiwa Na Kichwa Kutoka Tip Top Tunda Man

Kushoto Ni Chege, Katikati Ni Bushoke na Kulia Ni Abdul Kachaa

September 7, 2010

JAMBO SQUAD

Hawa Ndio Jambo Squad Kutoka pande za Rchuga (Watoto wa Bibi)




 Ni Jambo Squad Kutoka Pande Arusha kwa sasa  wapo wanakamilisha album yao ndani ya studio za Grandmaster Records Arusha meneo ya Ngarenaoro,,ikiwa na nyimbo kama Ngastuka ambayo kwa sasa inaruka katikaTv na Radio  mbalimbali nchini pamoja na nchini Kenya,wakusindikiza,na shule yetu ambayo itafuata baada ya Ngastuka,album ya Jambo ipo katika hatua za mwisho na inatarajiwa kuingia mizungukoni soon..

September 6, 2010

TIMU YA YANGA KUKIPIGA NA AFC LEOPARD YA KENYA KATIKA UWANJA WA SHEIK AMRI ABEID -ARUSHA SEP 8

Picha  mratibu wa mchezo  wa kirafiiki baina ya timu ya Yanga ya jijini Dar es salaam na Timu ya AFC Leopard ya nchini Kenya George Wakuganda akiwa anaongea na waandishi wa habari katika ofisi ya chama cha mpira wa miguu mkoani Arusha iliyopo ndani ya uwanja wa Kumbukumbu za Sheikh Amri Abeidi mechi ambayo itachezwa septembar nane


Kampuni ya CXC Afrika imeandaa mchezo mmoja wa kirafiki wa kimataifa kati ya timu ya Yanga jijini Dar es salaam na timu ya AFC Leopard ya nchini Kenya mechi ambayo itachezwa September nane katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sheirk Amri Abeid jijini hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya chama cha mpira wa miguu mkoani hapa mratibu wa mchezo huo George Wakuganda alisema kuwa nia na madhumuni ya kuandaa mchezo huo ni kuwapa burudani wakazi wa mkoa wa Arusha pamoja na vitongoji vyake  kwa kuweza kuona mchezo wa kimataifa ambao wamekuwa wakizikosa kwa kipindi kirefu.

Alisama kuwa mbali ya kuwapa burudani wakazi wa Arusha pia mechi hii itakuwa ni fursa kwa wapenzi wa soka wa mkoa wa Arusha kuweza kuitambua na kuiona timu yao mpya ambayo imesheeni vipaji mbalimbali vya hapa nchini Afrika kwa ujumla na hata nje ya Afrika.

Alitaja baadhi ya wachezaji maarufu ambao watacheza katika mechi hizo na aliaanza na timu ya Yanga kuwa ni pamoja na Kenneth Assamoh,Ernest Boakye,Yew Berco,pamoja na Mawrbia Ivana Kzenevic.

Alibainisha kwa timu ya AFC Leopard kuwa kila mtu mtanzania anaifahamu na anajua ugumu wa timu za kenya na alisema kuwa ikumbukwe timu hii pamoja na Gormahia zilipotea kwa muda mrefu sana katika anga la soka na sasa zimerudi kwa nguvu mpya.

Alitaja viingilio vya mechi hii kuwa kwa upande wa jukwaa kuu kiingilio itakuwa shilingi 10000 huku mzunguko ikiwa ni shilingi elfu tatu tu na kuongeza kuwa wameamua kuweka kiasi hichi cha hela ili kila mtu aweze kushuhudia mechi hii.

Kwa upande wa katibu msaidizi wa chama cha mpira wa miguu mkoani hapa Jeradi Munisi alisema kuwa anawashukuru sana kampuni hii kwa kuwaletea mechi kubwa kama hii na kusema kuwa anawaomba watanzania wajitokeze kwa wingi kushuhudi mechi hii ili wathamini ambao wanaleta mechi kama hizi wasikate tamaa.

Alisema kuwa wao kama chama wanatarajia kuzipokea timu hizi zote kesho nawanawapongeza pia waandaaji kwa kuwapa kipaumbele na kuona kuwa uwanja wao unafaa kuleta mechi kama hizi kuchezewa hapa.

"tunawashukuru kampuni hii kwa kutuletea mchezo huu hapa kwani wakazi wa Arusha tumekuwa tunaambulia kuangalia izi timu katika tv  au ukitaka zaidi upande gari uende dar sasa tunashukuru sana wanatutia moyo na kutufanya tuone wanatujali "alisema Munisi

September 4, 2010

UZUSHI KUHUSU MADHARA YA MAWASILIANO YA SIMU

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewataka watumiaji wa simu za mikononi kupuuza ujumbe wa tahadhari ulioanza kusambazwa jana na watu wasiojulikana, ikisema kuwa ni uzushi.
Jana kulikuwa na aina mbili za taarifa za tahadhari zilizokuwa zikitumwa kwa wateja wa simu za mikononi. Ujumbe wa kwanza unasema: “Ukipigiwa simu kwa private no (namba binafsi). au ikiandika call kwa red colour (rangi nyekundu) usipokee, ni mionzi, utapalarize (utapooza) na kufa.
Imetokea Kenya watu wamekufa. Julisha ndugu na jamaa wote.” Ujumbe mwingine unawataka watumiaji wa huduma hiyo wasipokee simu yoyote watakayopigiwa kupitia namba 7888308001, 9316048121, 9876266211, 9888854137 na 9876715587.
Ujumbe huo unasema: "Namba hii inapigwa na rangi nyekundu, unaweza kupata brain damage (tatizo la ubongo) kwa kupokea simu.
Watu 27 walifariki mara tuu baada ya kupokea simu iliyopigwa kutoka katika namba hizo." Ujumbe huo ulisababisha watumiaji wa simu kuingiwa na wasiwasi na baadhi waliwasiliana na chumba cha habari cha Mwananchi Communications kutaka ufafanuzi wa suala hilo na wengine wakieleza hofu ya kupooza.
Hata hivyo, taarifa iliyotumwa na msemaji wa TCRA, Innocent Mungy ambayo imesainiwa na kurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo, Profesa John Nkhoma, inasema: “Ujumbe huo unatakiwa kupuuzwa kwa kuwa ni uzushi usuokuwa na ukweli wowote.” Kutokana na ujumbe huo kusambazwa kwa watu wengi, TCRA imesema hakuna ukweli na hivyo kuwataka wananchi kuupuuzia. "Mamlaka ya Mawasiliano inapenda kuwahakikishia wananchi kwa ujumla kwamba taarifa zinazoenezwa ni za uzushi na sio za kweli.
Wananchi wanaombwa kupuuza uzushi huo kwa kua hauna ukweli wowote," inasema taarifa hiyo ya TCRA.
Ilifafanua kuwa kutokanha na maendeleo ya sayansi na teknolojia, kuna tafiti nyingi zimefanyika sehemu mbalimbali duniani ambazo zimeonyesha kwamba kiwango cha mawimbi ya mawasiliano hakina madhara kwa afya ya binadamu. 
TCRA iliwataka wote kuendelea kuwa na imani na teknolojia mpya zikiwemo za mawasiliano ya simu, utangazaji na utumiaji wa kompyuta ambazo zinatumiwa ulimwenguni kote bila madhara yoyote. "Madhumuni ya Mamlaka ya Mawasiliano na watoa huduma za mawasiliano kwa ujumla ni kuwaletea wananchi wa Tanzania mawasiliano bora kwa kujenga miundombinu, kutoa huduma bora na matumizi mema," inasema sheemu ya taarifa hiyo.
Mmoja wa watumiaji wa simu za mkononi, Frank Kimboyi ambaye naye alitumiwa ujumbe huo, alisema mwanzoni alipata wasiwasi mkubwa. "Baada ya kuupokea kidogo nilishituka, lakini baada ya kukaa na kutafakari uwezekano wa kitu kama hicho kutokea niliona ni mdogo na nikaamua kuupuuzia," alisema Kimboyi.

September 3, 2010


September 2, 2010

MJUE ZAIDI DJ MWENYE UMRI MDOGO KULIKO WOTE KATIKA JIJI LA TANGA

Dj Bob Nass Akiwakatika 1&2 Kisababisha Vilivyo
Dj Bob Nass Akifanya vitu vya ukweli ukweli

Jina lake kamili ni Nasr Thabit  wengi wanapenda kumuita Dj Bob Nass yupo Katika radio   Breez fm  ya Tanga  ni producer na dj.pia na ni mtangazaji wa kipindi cha flashback Siku ya  juma2 kuanzia saa 4 asubuhi mpaka 7 mchana
Na Huwa Anafanya kipindi cha mchana kinachoitwa  Track to Track Ni Kipindi ambacho Kinaanzia mida ya  saa 8 mpaka kumi jion kila siku  Ni Dj ambaye anapokuwa  ndani ya vipindi vyake lazima utavutiwa na vitu anavyovifanya

UBISHI WA KUFA MTU . HAWA JAMAA NOMA

Wapenda ligi watatu walibishana kuwa nani amekubuhu kwa ubishi kati yao. Wakaamua kila mmoja ahadithie ubishi wa haja alomfanyia mkewe
ili wapime nani kubobea zaidi kwenye hiyo fani.

Mbishi 1 akasema:
Mi siku moja nilivyokuwa nje ya nchi nilimpigia SIMU usiku mke wangu. Akapokea simu hakusema haloo...
Kulaleki  !!! na mimi nikakaa kimya sikuongea mpaka alfajiri wakati simu ilikuwa wazi.

Mbishi 2 akatia:
Mbona hiyo cha mtoto, mi siku moja nimerudi home nikagonga mlango mke wangu akaufungua lakini hakusema karibu mume wangu, aliniangalia tu.
Nikaona analeta madharau !!!
Sikuingia ndani nikasimama hapo hapo mlangoni mpaka asubuhi...huyoo nikatimua zangu job.

Mbishi 3 akaunganisha:
Hiyo nayo mbona cha mtoto tu, mi mke wangu tulipooana alikuwa anaona
haya kunigusa...ananidengulia eti  !!!
Na mimi sikumgusa na mpaka leo hatugusani.

Mbishi 1 na 2:
Aaaaaaaah FAZA acha usanii huo, nyie si mna watoto wawili ?
 
Mbishi 3:
Na hao watoto sijamuuliza kawaokota wapi... kwani mi nataka mchezo !!!.

Wazee nani anaweza kubishana na hawa jamaa?

September 1, 2010

KATIKA SAFU YA MSANII LEO NAKULETEA MWANA HIP HOP KUTOKAKA ARUSHA - ABDUL KACHAA

Abdul Kachaa Katika Pozi Zito
Huyu Ni Kachaa Katika Pozi kwa kweli ni dogo ambaye anafanya vizuri katika game la Music


Dogo Anakwenda Kwa Jina La Abdul Kachaaa

 Maskani Ni Atown - Ngarenaro
Dogo ana Umri wa miaka 14 kwa sasa anasoma kidato cha pili katika shule Bishop Kisula secondary sc/School 

Ni dogo ambae anatamba na Track yake inakwenda kwa jina la Sijafikia ndani yake kamshirikisha Tob B ikiwa imefanyika pale Motown Rec sijafikia ni track ambayo inafanya vizuri katika Radio Station mbalimbali hapa tanzania -  chini ya mkono wa producer Triple
 na singo nyingine ilikwenda kwa jina la Nawakumbusha nae ikiwa ifanyika pale Nice Records  na track ya tatu ni Ghetto la Mjombaa akiwa ameifanya pale Golden records
Dogo anatarajia kutoka na singo nyingine  itakwenda kwa jina la Harakati zaidi ndani ya singo hiyo hapo atakuwepo msanii kutoka katika kundi na Nako 2 Nako
Si mwingine ila ni Buu Nako
Nilpo Muuliza Abdul kachaa swala zima la Shule na Musiki iknakuwaje hapo kuna kusoma kweli?
Alisema “Mimi kama mimi Naheshimu Sana Shule kwa sababu Siwezi Kufanya Musiki Bila ya kuwa na elimu kwa hiyo ili muziki wangu upendwe na ukubalike ni lazima niwe na Elimu”.

Ni Hayo tu Katika Safu  ya Msanii. 

Imeandaliwa na Nass
 



KATIKA SAFU YA MALOVEE:Amekutesa mara nyingi, kwanini unamng’ang’ania?


ASILIMIA sabini ya wanaonipigia simu wakiomba ushauri baada ya kusoma mada zangu magazetini, hulalamikia kuhusu kuteswa na wapenzi wao. Kitu cha kushangaza zaidi ni kwamba, kati yao, asilimia themanini huwa wanaumizwa na wapenzi ambao wanawapenda sana.

Niweke sawa kidogo hilo, yaani wanakuwa na wapenzi ambao wao wanawapenda kwa mioyo yao yote, lakini ndiyo wanatesa kwa mambo mbalimbali. Kila akifikiria kuachana naye, anakutana na ukuta wa mapenzi ya dhati!

Hao ndiyo ninaowazungumzia hapa. Aidha wapo wale ambao wanaumizwa lakini hawajui kama wanaumia, lakini pia kuna wanaomia lakini wanaendelea kuvumilia wakiamini hawana ‘option’ nyingine, yaani kwa wapenzi wao wamefika na hata wakiachana inakuwa vigumu kupata mwingine!

Hizi ni fikra potofu sana. Ndugu zangu, katika mapenzi neno MATESO, MANYANYASO, KUSIMANGWA hayakubaliki kabisa. Hebu nitoe mfano mmoja, juzi nilizungumza na dada mmoja ofisini kwangu, akajaribu kueleza matatizo anayokabiliana nayo katika uhusiano wake. Ni binti mwenye umri wa miaka 28, ana mtoto mmoja ambaye baba yake alimkana!

Anaishi kwa taabu kwasababu hana kazi, kila siku amekuwa akianzisha uhusiano na wanaume lakini wamemtumia na kumuacha! Ni mwanamke mzuri kwa kumtazama, anavutia na anaweza kumshawishi mwanaume yeyote aliye mkamilifu lakini changamoto anazokutana nazo ndiyo hizo!

Ameshalia mpaka machozi yamekauka, mwisho akafikiri huenda amelogwa! Lakini mwisho wa siku nilizungumza naye na aliondoka akitabasamu, badala ya machozi aliyokuja nayo! Alikuwa na mwanaye anayeitwa James (5), mwenye afya nzuri na mchangamfu sana. Sitapenda kutaja jina lake, lakini alichovuna kwangu anajua mwenyewe!

Msomaji wangu, inawezekana kabisa na wewe upo katika mateso kama ya dada yetu huyo na hujui njia ya kutokea, usijali. Mimi nakuambia futa machozi yako. Inawezekana kabisa, kuna mahali ulipokosea katika maisha yako ndiyo maana leo hii mapenzi kwako yamekuwa mateso, lakini hiyo isiyo sababu!

Bado unayo nafasi ya kujipanga na kuanza upya kufurahia mapenzi. Kila kitu kinawezekana rafiki yangu.
Lakini lazima tukubali kwamba, wakati mwingine mapenzi ni mateso, ni chanzo cha kuingia kwenye matatizo maishani mwako.

Ndiyo maana Wataalamu wa Saikolojia ya Mapenzi wanasema ukikosea kuchagua mke/mume, basi tarajia maisha mabaya siku zote. Hii ndiyo kusema kwamba, mwanzo wa mafanikio bora maishani ni kuwa na mwenzi sahihi.

Unayempenda, anayekupenda na unayefurahia kuwa naye. Wanasaikolojia ya Mapenzi wanakubaliana moja kwa moja na hoja hii. Kwamba wakati mwingine mapenzi yanaweza kuwa chanzo cha mateso katika maisha ya binadamu.

Kauli hii inashibishwa na hoja kwamba, mateso hayo yatasababisha na jinsi wewe mwenyewe utakavyokuwa umeingia na unavyoendesha uhusiano wako.

KWANINI MATESO?
Wapo ambao wanashangaa hoja hii, wanashangaa kwasababu tangu wamefahamu mambo ya mapenzi hawajawahi kuwa na uhusiano zaidi ya mpenzi mmoja ambaye pengine hivi sasa wapo katika ndoa yenye watoto kadhaa!

Kwao hili hawakubaliani nalo. Lakini wakati huo huo kuna ambao walianza uhusiano wa kimapenzi kwa matatizo na hivi sasa bado wapo katika matatizo katika maisha yao ya kimapenzi.

Kwa ufafanuzi zaidi hebu soma visa vifuatavyo ambayo ni vya watu wawili tofauti, hapana shaka utakuwa na jipya la kujifunza. Mosi: Hiki kinamhusu Ben, alipokuwa anasoma Elimu ya Sekondari alitokea kumpenda sana Lucy na kwa bahati nzuri Lucy naye alikuwa akimpenda sana, wakawa katika uhusiano kwa misingi ya upendo na uaminifu.

Wapenzi hawa walikuwa wakipendana sana na wakati wakianzisha uhusiano wao walikuwa kidato cha nne. Mpaka wanamaliza kidato cha sita hawakuwahi kukutana kimwili, baadaye kila mmoja akiwa anasoma chuo chake, walikutana nyumbani kwao Mbeya wakati wa likizo.

Wikiendi moja wakaenda club, hiyo ndiyo ikawa siku yao ya kwanza kufanya mapenzi na wote wawili ilikuwa mara yao ya kwanza kushiriki katika sayari ya wapendao.

Siku zikaenda na walipomaliza chuo na kupata kazi wakaoana, wanaishi kwa furaha na amani, ingawa kuna matatizo madogo madogo ya hapa na pale ambayo huwa wanayamaliza wenyewe. Hivi sasa Ben ana miaka 38 na Lucy miaka 34 wana watoto wawili katika ndoa yao ya amani na mapenzi ya dhati.

Kisa cha pili kinamhusu Lilian; Huyu ni msichana, akiwa darasa la sita tayari alishaanza mambo ya mapenzi, mpaka anafika kidato cha tatu alikuwa kashatembea na wanaume zaidi ya ishirini! Hakufanikiwa kufanya mtihani wake wa mwisho wa kidato cha nne kwa sababu aligundulika ana ujauzito wiki chache kabla ya mtihani huo, mwisho wa masomo yake ukawa hapo.

Alivyojifungua akaanza kufanya kazi ya kuuza genge na kwa bahati mbaya mwanaye hakuwa na baba, maana hakujua mimba ni ya nani na kati ya wanaume watatu aliowashuku kuwa wanaweza kuwa ni mimba ya mmoja wao, alipowafuata walimfukuza kama mbwa.

Baadaye Lilian aliamua kutulia na kwa bahati nzuri akapata mpenzi mwingine ambaye alitulia naye akiamini anaweza kufuta machungu yake katika historia yake ya mapenzi, cha ajabu sasa baadaye akaachwa solemba.

Akatafuta bwana mwingine akawa naye na kuachwa. Lilian sasa ana miaka 27 lakini ana watoto wanne na kila mmoja ana baba yake. Maisha yake siyo mazuri na chanzo kikubwa hapo ni mapenzi. Anajilaumu sana kujiingiza katika mapenzi ya utotoni. Maisha yake ni ya kubangaiza akiwa hana uhakika wa kupata mlo wa siku inayofuata.

Kwa leo kituo kikubwa kinakuwa hapa, wiki ijayo tutaendelea.
Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Mambo ya Mapenzi ambaye anaandikia magazeti ya Global Publishers, ameandika vitabu vya True Love na Secret Love. IMEANDALIWA NA SHALUWA

August 27, 2010

HAPPY BIRTHDAY JOE MAKINI




Siku kama ya leo tarehe 27 mwezi wa nane ni siku ambayo alizaliwa star wa hiphop kutoka kaskazini(A Town AKA Rchuga) joe makini Happy birthday Kaka Pamoja sana M/Mungu Akuzidishie Umri

August 20, 2010

A newly married Husband saved his wife's number on his mobile as..

A newly married Husband saved his wife's number on his mobile as
"MY LOVE";
After one year of marriage, it was found changed to
 "MY WIFE"
After Five years of Marriage:
"HOME"
and after Ten Years
"HITLER"
and after Silver Anniversary
"WRONG NUMBER" .

August 19, 2010

KATIKA ANGA ZA KISPOTI- TIMU YA MKOA WA ARUSHA AFC YATOA JEZI MPYA ZA LIGI KUUTANZANIA BARA .

 Mchezaji wa timu ya sekei Adinani Ally akipokea kombe mara baada ya kushinda katika mashindao ya kombe la sikukuu ya wakulima yaliyokuwa yameandaliwa na halimashauri ya jijij
 

 Wachezaji wa timu ya AFC wakiwa wanapewa mahelekezo na kocha wao Hatuga Manyundo wakati wa mapumziko ya mechi baina yao na timu ya Rhino ambayo kwa ivi sasa ni timu ya mkoa wa Arusha mara baada ya kununuliwa na mmiliki wa shule ya Bishop durnnig Mr.Sironga.

wachezaji wa AFC Wakipta Hili na Lile kutoka kwa Kocha wao Hatuga Manyundo

August 8, 2010

HIVI NDIVYO FIESTA DAR 2010 ILIVYOKUWA RAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA

Hapo ni Vijana kutoka Nigeria (Bracket) wakiimba Songi lao la  Yori Yori

ngoma ya 'aldji aladji' ikioneshwa namna inavyochezwa na wenyewe.

Lilkim Akiwatumbuiza maelfu  ya mashabiki walifika katika Tamasha la fiesta

Kundi la Wanaume TMK toka shoto Mheshimiwa Temba, Chege na Kr Mulla jukwaani na wimbo wao wa 'Mambo bado
                         

palikuwa hapatoshi nyomi ya ukweli

                                Juma Kasim Kiroboto (Juma Nature) Akiimba na mwana dafada Lilkim

August 1, 2010

JAMANI! TUWE TUNASOMA UJUMBE MARA TUUPATAPO

Mgonjwa mmoja mahututi alikuwa hawezi kuongea,
alipofikishwa
hospitalini akawekewa oxygen. Basi mchungaji akaja kumuombea. WAKATI
AKIOMBEWA,
yule mgonjwa akachukua kalamu na karatasi, Akaandika haraka haraka na
akampa
yule Mchungaji. Ambaye badala ya kuisoma ile karatasi, akaitia kwenye mfuko
wa
joho na kuendelea na maombi hadi yule mgonjwa, AKAKATA ROHO. Mchungaji
hakuisoma ile karatasi akijua kua ni wosia wa marehemu. Akasubiri baada
ya
mazishi kwenye kikao cha ndugu akasema; "KUNA KITU NILIPEWA NA MAREHEMU
SIKU NILIYOKUA NAMUOMBEA" Akampa mmoja wa wanandugu akisome. Haya ndiyo
yaliyokuwa yameandikwa na yule mgonjwa: "UMEKANYAGA MPIRA WA OXYGEN,
NAKOSA HEWA"

July 31, 2010

NEEMA LUSANDA AFARIKI DUNIA NI MTANGAZAJI WA RADIO TRIPLE A FM - ARUSHA

                                            Marehemu Neema Lusanda Enzi za uwai Wake

MAREHEM NEEMA LUSANDA ALIYEKUWA MTANGAZAJI WA TRIPLE A FM AFARIKI DUNIA
MAREHEM ALIKUA MTANGAZAJI WA MUDA MREFU NA MWENYE UWEZO MKUBWA HAKIKA
TUMEPOTEZA MTU MUHIMU KATIKA HABARI NEEMA ALIFARIKI DUNIA KATIKA HOSPITALI
YA MOUNT MERU BAADA YA KUSUMBULIWA NA SHINIKIZO LA DAMU KWA WIKI KADHA KITU
AMBACHO KILICHOMPELEKEA UMAUTI WAKE HAPO JANA MAREHEM AMEACHA MTOTO MOJA
NA MJANE TAARIFA UTARATIBU WA MAZISHI NI KESHO KATIKA MAKABURI YA NJIRO
TAARIFA HIZI NI TOKA KWA RADIO MANAGER WA TRIPLE BWANA BORRY MBARAKA KWA
YEYETO ANAYETAKA KUWASILIANA NA CREW YA TRIPLE A FM APIGE NUMBER HII
0655707022

ROHO YA MAREHEMU ILALE MAHALI PEMA PEPONI AMINA

July 28, 2010

Ajali ya ndege yaua watu 152 Pakistan

                                          Eneo la ajali hakifikiki kwa njia ya barabara, waokoaji walitumia mikono mitupu
                                          kufukua mabaki ya ndege.


      Ramani kuonyesha maeneo yanayohusiana na ajali ya ndege nchini Pakistan

dege ya abiria imeanguka huko Islamabad, mji mkuu wa Pakistan na kuua watu wote 152 waliokuwa ndani yake.
Ndege hiyo, iliyokuwa katika safari kutoka Karachi kwenda Islamabad inaendeshwa na kampuni binafsi ya Airblue, ilianguka kwenye vilima vilivyoko kaskazini mwa jiji wakati ikijiandaa kutua.


Eneo la ajali hakifikiki kwa njia ya barabara, waokoaji walitumia mikono mitupu kufukua mabaki ya ndege.
Bofya Bofya hapa kuangalia picha zaidi
Hapakuwa na taarifa za awali kubaini chanzo cha ajali. Ingawa imeelezwa eneo hilo lilikuwa limetandwa na ukungu.
Televisheni za Pakistan zilionyesha picha za mabaki ya ndege yakiwaka moto, huku helikopta za uokoaji zikiranda juu.

Tathmini

Airblue ndiyo kampuni kubwa zaidi ya ndege binafsi, miongoni mwa mashirika yaliyoibuka nchini Pakistan katika miaka ya karibuni.
Kampuni hiyo na idara ya usimamizi wa safari za anga hawadhani ndege hiyo ilikutwa na matatizo ya kiufundi wakati ikiondoka Karachi.
Wanasema hapakuwa na dalili za hitilafu ya kiufundi katika mawasiliano kati ya rubani na mnara wa kuongozea ndege wa Karachi.
Hata hivyo, maafisa wa uwanja wa ndege waliieleza BBC kuwa ndege mbili zilizokuwa zitue kwenye mji huo mkuu zilikataliwa kabla ya ajali hiyo ya Airblue, katika ajali kubwa zaidi ya ndege kuwahi kutokea nchini Pakistan.
Ingawa sekta ya safari za anga imekuwa kwa kasi, wakosoaji wanasema viwango vimekuwa chini na haviendani na ukuaji wa huduma.
Marubani hulalamika wanalazimishwa kuruka kwa saa za ziada, jambo linalosababisha uchovu, ingawa mashirika ya ndege yanakana madai hayo.

Jangwa kubwa

Imtiaz Elahi, mwenyekiti wa Capital Development Authority, mamlaka inashughulikia dharura, alisema ajali hiyo "inavunja moyo".
"Ni janga kubwa, na ninaweza kuthibitisha kwa uchungu kwamba hapakuwa na watu waliosalimika," alilieleza shirika la habari la Associated Press.
Ndege hiyo, inayosemekana kuwa ni muundo wa Airbus A321 ikiwa na abiria 146 na wafanyakazi sita ndani yake, inaaminika kuwa iliondoka Karachi saa mbili kasorobo asubuhi majira ya huko.

Hakuna walionusurika

Awali, Wizara ya mambo ya ndani ya Pakistan, ilisema watu wasiopungua watano walikuwa wamenusurika kifo na kupelekwa hospitalini, lakini maafisa wa maeneo hayo baadaye walisema taarifa hizo hazikuwa sahihi.
Televisheni za maeneo hayo zilionyesha vipande vya mabati na chuma vikining'inia kutoka juu ya miti na kutapakaa ardhini.Kifaa cha kutunza kumbukumbu za safari kimekwishapatikana.
Maafisa wanasema waokoaji waliokuwa wakitafuta watu walionusurika, walikuwa wakitumia mikono mitupu kufukua mabaki hayo. Eneo la ajali lililoko kwenye mlima mkali, halifikiki kwa barabara.
Bofya Bofya hapa kuangalia picha za ajali hiyo.


July 24, 2010

BRAZILI YAPATA KOCHA MPYA- Muricy Ramalho

                                                    Muricy Ramalho ndiye ataifunza Brazil.
Timu ya taifa ya kandanda ya Brazil imempata kocha mpya Muricy Ramalho kushika nafasi ya Dunga aliyejiuzulu baada ya Brazil kutolewa mapema kwenye michuano ya mwaka huu ya Kombe la Dunia nchini Afrika ya Kusini.
Ramalho ambaye ni kocha mkuu wa klabu ya Fluminense ya Rio de Janeiro, alijipatia umaarufu kwa kuiongoza klabu ya Sao Paulo kunyakua ubingwa wa Brazil kwa miaka mitatu mfululizo kati ya 2006 na 2008.
Ramalho anasifika kuwa ni miongoni mwa makocha hodari nchini Brazil na aliwahi kuichezea timu ya taifa ya Brazil katika miaka ya 70.
Timu yake ya Fluminese hivi sasa ndiyo inaongoza ligi ya taifa ya Brazil na kuteuliwa kwake kumefurahiwa na wengi.
Je Ramalho atauweza mfupa aliouacha Dunga? Jibu litapatikana katika harakati za Brazil kujiandaa kwa Kombe la Dunia la 2014, fainali zitakazofanyika Brazil.
Ingawa, 2014 ni mbali sana kwa lugha ya soka, na kama matokeo ya awali yatakuwa mabovu kwake, basi ataonyeshwa mlango kama waliomtangulia.

July 13, 2010

KATIKA SAFU YA MAPENZI: JINSI GANI YA KUMRIDHISHA MUMEO .


1- Mapokezi mazuri

a) Baada ya kurejea kutoka kazini, skuli, safarini, au popote pale palipowatenganisha, anza kwa maamkizi mazuri.

b) Mpokee kwa uso mchangamfu

c) Jipambe na ujitie manukato (Perfume)

d) Anza na habari nzuri na chelewesha habari yoyote mbaya mpaka atapokwisha pumzika

e) Mpokee kwa maneno ya mapenzi na hamu/shauku

f) Fanya jitihada kubwa katika mapishi mazuri na kitayarishe kwa wakati

2- Ipambe na ilainishe sauti

Ni kwa ajili ya mumeo peke yake, isitumike mbele ya wanaume wasio mahram (wanaume wanaoweza kukuoa iwapo utakuwa huna mume)

3- Harufu nzuri na kujipamba mwili

a) Ushughulikie vyema mwili wako na afya yako.

b) Vaa nguo za kuvutia na jitie manukato.

c) Koga mara kwa mara, na baada ya siku za hedhi, safisha madoa madoa yote ya damu na ondosha harufu mbaya.

d) Jiepushe kuonekana na mumeo ukiwa na nguo chafu au ukiwa ovyo.

e) Jiepushe na mapambo yaliyokatazwa, mfano wa tattoo.(kuchorwa mwili kwa kitu cha moto kwa ajili ya pambo.)

f) Tumia aina ya manukano, rangi, na nguo ambazo mumeo anazipenda.

g) Badilisha mtindo wa nywele, manukato n.k. mara kwa mara.

h) Hata hivyo usifanye isirafu katika vitu hivi, na bila shaka fanya hivyo mbele ya mahram zako na wanawake wenzako tu.

4- Jimai (Tendo la ndoa)

a) Harakisha kufanya jimai pale mumeo anapokuwa na hamu ya tendo hilo.

b) Weka mwili wako safi na wenye kunukia kadri iwezekanavyo pamoja na kujisafisha maji maji yanayotoka wakati wa jimai.

c) Semeshaneni maneno ya mapenzi na mumeo.

d) Mwachie mumeo atosheleze kabisa hamu yake.

e) Chagua wakati muwafaka na muda mzuri wa kumchangamsha mumeo, na kumtia hamu ya kufanya jimai, mfano baada ya kurudi safari, mwisho wa wiki, n.k.

5- Kutosheka na kile ulichojaaliwa na Allaah (S.W.T.)

a) Usiwe mnyonge kwa kuwa mumeo ni maskini au na aina ya kazi anayofanya.

b) Uwaangalie masikini, wagonjwa, na vilema na kumkumbuka Allaah (S.W.T.) kwa yote yale uliyopewa.

c) Ni lazima ukumbuke kuwa utajiri wa kweli upo katika Iman na ucha Mungu

6- Kutoshughulishwa na mambo ya kidunia

a) Usiichukulie dunia hii kuwa ya matumaini na kushughulishwa nayo.

b) Usimdai mumeo vitu vingi visivyo na ulazima.

c) Kutosheka na kuishi maisha ya kawaida hakuna maana ya kutofurahia/kutotumia kilicho kizuri na kilichoruhusiwa (halali), bali kunamaanisha mtu kuangalia akhera yake na kutumia kile ambacho Allah Amempa kwa ajili ya kupata Pepo (Jannah).

d) Muhimize mumeo kupunguza matumizi na kubakisha fedha kwa ajili ya kutoa sadaka na kuwalisha masikini na wasiojiweza

7- Shukurani

a) Kutokana na hadithi ya Mtume (S.A.W.), wengi wa watu wa motoni ni wanawake kwa sababu hawana shukurani na kutoridhia wema wanaofanyiwa.

b) Matokeo ya kuwa na shukurani ni kuwa mumeo atakupenda zaidi na atafanya awezalo kukufurahisha kwa njia nyingi.

c) Matokeo ya kutokuwa na shukurani ni kuwa mumeo atavunjika moyo na ataanza kujiuliza: Kwa nini nilazimike kumfanyia wema hali ya kuwa hana shukurani?

8- Kujitolea na Twaa

a) Hususan nyakati za maharibiko/matatizo makubwa katika mwili wa mumeo au katika kazi yake, mfano ajali au kufilisika.

b) Kumpa msaada kwa kufanya kazi, msaada wa fedha, na vitu vyengine iwapo utahitajika.

9- Kumtii

a) Kumtii katika yote anayokuamrisha, isipokuwa katika yale yaliyoharamishwa.

b) Katika Uislam, mume ndie kiongozi wa familia, na mke ni msaidizi na mshauri wake.

10- Kumliwaza anapokasirika

a) Kwanza kabisa, jaribu kujiepusha na kile ambacho una uhakika kuwa kitamkasirisha.

b) Bali iwapo imetokezea kuwa huwezi, basi jaribu kuepusha ugomvi kwa njia zifuatazo:

1. Iwapo wewe ndiye uliyekosea, basi mtake radhi (muombe msamaha)

2. Iwapo yeye ndiye aliyekosea basi:

- Endelea kunyamaza badala ya kubishana au

- Samehe haki yako au

- Subiri hadi zitakapokwisha hasira zake na mlijadili suala hilo kwa amani

3. Iwapo amekasirishwa na mambo nje ya nyumba basi:

- Endelea kunyamaza kimya hadi hasira zake zitapokwisha

- Mpe udhuru (wa hasira zake), mfano kuchoka, matatizo kazini, kuna mtu amemuudhi.

- Usimuulize masuala mengi na kushikilia kujua nini kimetokezea, mfano (kumwambia) (1) Ni lazima unieleze nini kimetokezea. (2) Ni lazima nijue nini kimekukasirisha namna hiyo. (3) Unanificha kitu, na mimi nina haki ya kujua.

11- Muongozo (na majukumu) anapokuwa hayupo:

a) Jilinde na mahusiano yoyote yaliyokatazwa.

b) Zidhibiti siri za familia, hususan jimai (tendo la ndoa) na mambo ambayo mumeo hapendi watu wengine wayajue.

c) Ishughulikie nyumba na watoto.

d) Ishughulikie mali yake na vitu vyake.

e) Usitoke nje ya nyumba yako bila ya ruhusa yake na bila ya hijab iliyo kamili.

f) Usikaribishe watu ambao mumeo hapendi kuja kwao.

g) Usimruhusu mwanamme yeyote asie mahram wako kuwa nawe faragha pahala popote.

h) Kuwa mwema kwa wazazi wake na jamaa zake akiwa hayupo.

12- Kuonyesha heshima kwa familia yake na rafiki zake

a) Ni lazima uwakaribishe wageni wake na ujaribu kuwafurahisha, hususan wazazi wake.

b) Ni lazima uepuke matatizo kati yako na jamaa zake kwa kadri iwezekanavyo.

c) Ni lazima uepuke kumuweka pahala ambapo inambidi achague kati ya mama yake na mkewe.

d) Onyesha urafiki (makaribisho mazuri) kwa wageni wake kwa kuwatayarishia pahala pazuri pa kuketi, chakula kizuri, kuwakaribisha vizuri wake zao, n.k.

e) Muhimize kuwatembelea jamaa zake na uwaalike nyumbani kwako.

f) Wapigie simu wazazi na dada zake, watumie barua, na wanunulie zawadi, wasaidie wakati wanapoharibikiwa, n.k.

13- Wivu wenye kukubalika

a) Wivu ni aina ya mapenzi ya mke kwa mumewe bali ni lazima ubakie katika mipaka ya Uislam, mfano kutowatukana na kuwasengenya wengine, kuwavunjia heshima zao, n.k.

b) Usifuate au kuanzisha tuhuma zisizo na msingi

14- Subira na kumpa moyo

a) Kuwa na subira mnapokabiliwa na umasikini na hali ngumu (kimaisha na kifamilia).

b) Wakati mnapokabiliwa na majanga na maharibiko ambayo yanaweza kutokea kwako, kwa mumeo, kwa watoto wako, jamaa au mali, mfano magonjwa, ajali, kifo, n.k.

c) Wakati mnapokabiliwa na matatizo katika Da’wah (kufungwa jela, kukamatwa, n.k.), kuwa na subira na mhimize katika kubaki katika njia ya Allaah na kumkumbusha kuhusu Pepo.

d) Anapokufanyia uovu, mlipe uovu wake kwa kumfanyia wema.

15- Msaidie katika kumtii Allah, Da'awah (Ulinganiaji) na Jihad

a) Shirikiana na mumeo na mkumbushe ibada mbali mbali za faradhi na za Sunnah.

b) Muhimize kusali usiku.

c) Sikiliza na soma Qur’an peke yako na ukiwa pamoja na mumeo.

d) Mkumbuke (mtaje) Allaah (S.W.T.) sana, hasa hasa baada ya Alfajiri na kabla ya Magharibi.

e) Pangeni pamoja shughuli za Da’wah kwa wanawake na watoto.

f) Jifunze hukumu za Kiislam na adabu za Kiislam kwa wanawake.

g) Msaidie mumeo katika shughuli zake kwa kumhimiza, kumpa ushauri mwema, kumliwaza machungu yake, n.k.

h) Samehe baadhi ya haki zako na samehe sehemu ya muda wako wa kuwa pamoja na mumeo kwa ajili ya Da’wah.

i) Mhimize kwenda Jihad anapohitajika na mkumbushe kuwa wewe na watoto mtakuwa katika hifadhi ya Allaah (S.W.T.)

16. Utunzaji mzuri wa Nyumba

a) Iweke nyumba safi, weka mapambo na iweke katika mpangilio mzuri.

b) Badilisha mpangilio wa nyumba mara kwa mara ili kuzuia kupoteza hamu nayo na kuchoshwa nayo.

c) Tayarisha chakula kizuri na chenye afya.

d) Jifunze ujuzi wowote wa muhimu kuhusu uangalizi wa nyumba, mfano kushona, n.k.

e) Jifunze namna ya kuwalea vyema watoto na kwa njia ya Kiislam

17- Kuhifadhi/Kutunza fedha na familia



a) Usitumie fedha zake, hata kwa sadaka bila ya ruhusa yake labda uwe na uhakika kuwa atakubaliana na matumizi hayo.

b) Ilinde nyumba yake, gari, n.k. anapokuwa hayupo.

                                                                                                              Imeandaliwa na Nass

July 12, 2010

Uhispania washindi wa Kombe la Dunia


                            kikosi cha Spain Kilicho twaa ubingwa wa kombe la Dunia 2010


Andres Iniesta alifunga goli dakika nne kabla ya muda ulioongezwa kumalizika na kusababisha Uhispania kupata ushindi wao kwa mara ya kwanza kwenye Kombe la Dunia kwa bao 1-0 dhidi ya Uholanzi.

July 11, 2010

UJERUMANI YATWAA NAFASI YA TATU

                                                            Kikosi Cha Ujerumani
Ujerumani imenyakua nafasi ya tatu kwenye mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini, baada ya kuifunga Uruguay mabao 3-2 katika uwanja wa Nelson Mandela Bay, mjini Port Elizabeth.
Sami Khedira aliifungia Ujerumani bao la ushindi katika dakika ya 82 baada ya ngome ya ulinzi ya Uruguay kushindwa kuondosha mpira wa kona uliopigwa na Mesut Ozil.
Sekunde chache kabla ya mchuano kumalizika mshambuliaji wa Uruguay Diego Forlan alipiga mpira wa adhabu uliogonga mwamba.
Ujerumani ndio waliotangulia kufunga katika dakika ya 18 kupitia Thomas Muller, kabla ya Edinson Cavani kuisawazishia Uruguay dakika 10 baadaye.

Lala salama

Kipindi cha kwanza kilimalizika 1-1 na dakika 6 baada ya cha pili kuanza Diego Forlan alisukumiza wavuni pasi kutoka kwa Egidio Arevalo, Uruguay ikawa inaongoza 2-1.
Hilo lilikuwa bao la tano la Forlan kwenye michuano hiyo ya Kombe la Dunia, na ni miongoni mwa wafungaji bora.
Katika dakika ya 56, Marcell Jansen aliisawazishia Ujerumani kwa bao la kichwa baada ya krosi ya Jerome Boateng kumzidi mlinda mlango Fernando Muslera.
Baada ya Sami Khedira kuifungia Ujerumani bao la ushindi , Uruguay walizidisha mashambulizi bila mafanikio.
Kocha wa Ujerumani, Joachim Loew, aliwapumzisha wachezaji mashuhuri miongoni mwao mshambuliaji Miroslav Klose, Likas Podolsi na mlinzi Philip Lahm.
Klose alikosa nafasi ya kufikisha goli la 15 idadi ambayo mshambuliaji wa Brazil, Ronaldo amekwisha funga katika historia ya mashindano ya Kombe la Dunia.

July 10, 2010

KATIKA SAFU YA MAPENZI: Kwanini ukubali kuchangia penzi?

Kati ya vitu vinavyowaumiza wengi walio katika uhusiano ni pamoja na penzi la kuchangia! Yaani uwe na mpenzi wako, halafu awe na mtu mwingine tena zaidi yako. Hakika inauma sana. Uhusiano wenye ladha ni ule wa mwenzi mmoja. Uwe wake peke yako, awe wako peke yake!

Mapenzi ni sawa na bustani nzuri ya maua, wakati mwingine inahitaji mbolea, kumwagiliwa maji na hata kupaliliwa. Kwa kufanya hivyo utazidisha ladha ya mapenzi na kuyafanya yazidi kuwa na nguvu zaidi ya awali. Lakini kama hutamwagilia, hutaweka mbolea, hutapalilia, hesabu kwamba mapenzi yako yanaweza kuanza kupoteza nguvu taratibu na hatimaye kufa kabisa.

Kikubwa ambacho nimepanga kuzungumza nanyi leo ni jinsi ya kumfanya mpenzi wako awe wako peke yako. Umeshawahi kufikiria kwamba, kama ukishindwa kutimiza mambo fulani katika penzi au ndoa yako, mwenzi wako anaweza kuwa wa kushea?

Kama bado, inakubidi ufahamu hilo kuanzia leo. Mpenzi anahitaji mambo mengi ili aendelee kuwa mwaminifu kwenye penzi lenu. Ni kweli kwamba uaminifu upo kwa mtu mwenyewe, kama mtu ni mwaminifu basi atadumisha uaminifu uliopo ndani yake, lakini kama kuna mambo unakosea, lazima utasalitiwa!

Tena basi, kama mwenzi wako anakupenda, atakusaliti huku analia! Kwanini? Kwasababu analizwa na kitendo ambacho hajapenda kukifanya ila wewe mwenyewe ndiyo umemlazimisha afanye hivyo.

Wanatafuta nini kwa wengine?
Tukiachana na tamaa, hulka na ushawishi, wakati mwingine mpenzi anaweza kusaliti kwa kukosa yale ya muhimu zaidi katika penzi au ndoa yake.

Kwa bahati mbaya sana, watu wa aina hii huwa hawasemi moja kwa moja kuwa wanakosa vitu fulani au wanapenda vitu fulani, badala yake hutumia lugha za ishara zaidi na kama hutaelewa basi huona suluhisho na kutafuta pumziko lingine nje.

Hapa sasa mwenzi wako anakuwa si wako peke yako tena! Lakini lazima uhakikishe mpenzi wako anaendelea kuwa wako bila kushea na mtu yeyote na jambo hili linawezekana kabisa ikiwa wewe mwenyewe utataka iwe hivyo.

Zipo hatua au mambo mengi ya kumfanyia mpenzi wako ili awe wako peke yako, lakini hapa nitakupa yale ya msingi zaidi yatakayokusaidia katika penzi lako.

Kama inavyoonekana hapo juu, nimeyafananisha mapenzi na bustani nzuri ambayo ina mahitaji yake. Sasa katika uchambuzi huu, nitaainisha jinsi ya kuitunza bustani (penzi) yako vizuri sana na kuifanya bora zaidi kila siku.

MOSI: Mapenzi yanahitaji mbolea. Hapa nazungumzia penzi ambalo tayari limeshakuwa penzi! Kama ni bustani basi tayari mboga-mboga zako zimemea vizuri.

Lakini ukumbuke kwamba, bustani yako haitaweza kuendelea kuwa bora kama haitakuwa na matunzo. Hapa penzi linahitaji mbolea. Mbolea ninayoizungumzia hapa ni maneno matamu yaliyojaa huba. Fikisha hisia zako kwa mwenzi wako kwa namna ya kipekee iliyojaa penzi la dhati.

Mweleze jinsi unavyompenda na jinsi maisha yako ambavyo hayawezi kukamilika bila yeye. Huu ni wakati wako wa kumsumbua kwa meseji zilizojaa tungo za mahaba, kadi, maua na zawadi ndogo ndogo.

Baadhi ya wanandoa wakishaoana, huacha utaratibu huu. Kuna wanaosema: “Ah! Hayo mambo ya kizamani bwana, kipindi akiwa demu wangu, sasa hivi yupo ndani, kwanini nihangaike?”
Haya ni makosa makubwa ndugu yangu. Shamba bila mbolea kuna mavuno kweli?

PILI: Bustani yako itahitaji maji kwa ajili ya kuzidisha ustawi wa mazao yako. Hapa unatakiwa kuwa mbunifu zaidi katika mambo yanayohusu mapenzi moja kwa moja.

Unatakiwa kubadilisha mitindo ya chumbani, mahali pa kukutana na hata sehemu za mitoko. Inashauriwa ili kuboresha penzi ni vizuri kutoka sehemu mbalimbali na mwenzi wako. Inapendeza zaidi angalau mara tatu kwa miezi sita, kulala na mwenzako hotelini.

Hapa utakuwa unanakshi zaidi penzi lako. ‘Outing’ yako ni vyema ikawa ya kimahaba zaidi, kuanzia mavazi, sehemu mnazotembelea n.k

Mfanyie mwenzi wako mambo ya kimahaba mnapokuwa wawili. Mbusu, mkumbatie, mwambie jinsi unavyojisikia wa pekee kuwa wake.

TATU: Baada ya muda bustani huota majani mengine ambayo si mboga! Yawezekana kabisa, kwa bahati mbaya uchafu ukaingia bustanini. Wakati wa palizi ni muda sahihi wa kuondoa vyote hivyo.
Hata katika mapenzi pia hutakiwa kufanya jambo hili. Kugombana au kupishana kiswahili kwa wapenzi ni jambo la kawaida sana, hivyo ni vyema kuweka sawa tofauti hizo mapema, kabla tatizo halijawa kubwa zaidi. Hii ndiyo palizi ninayoizungumzia.

Usikae na kinyongo moyoni mwako, kuwa mjanja, hata kama ni yeye ndiye aliyekosea, zungumza naye ukimweleza jinsi ambavyo hupendi mgombane, mkimweleza hisia zako kwamba unatamani sana muelewane katika siku zote za maisha yenu. Weka mambo sawa.

Kwa kufanya hivi, kwa hakika penzi lako litazidi kuwa imara zaidi na atakuwa wako peke yako. Hatakuwa wa kuchangia tena. Naamini umeibuka na kitu kipya leo. Ahsante sana kwa kunisoma, tuonane tena wiki ijayo.

Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Mambo ya Mapenzi ambaye anaandikia magazeti ya Global Publishers, ameandika Vitabu vya True Love na Secret Love. Kwa makala zaidi, hadithi na mijadala ya kimapenzi, mtembelee kwenye tovut

HIVI NDIVYO FIESTA 2010 JIPANGUZE RAAAAAAAAAAAA RAAAAAA ILIVYOKUWA

Kundi la  wazushi Kutoka  A-Town likipangusa vilivyo  katika Fiesta 2010
Wakiwa kwenye Fiesta Jipanguse 2010 jijini A-Taun toka shoto ni Marry,Meneja Vipipndi wa Clouds FM Sebastian Maganga,Mtangazaji wa kipindi cha Michezo Clouds FM Ibrahim Masoud a.k.a Maestro,Tirra,Kida Waziri pamoja na Sophia Kesy Wa Clouds Fm

Hao hapo ni  nyomi ya mashabiki waliohudhuria katika fiesta 2010 pale Matongee Carnival
watu walifiestika vilivyo
Mwanamuzi mkongwe wa muziki wa dansi Ndandaa Kossovo kulia na skwadi lake zima wakitumbuiza katika Fiesta Jipanguse 2010 usiku wa kuamkia leo ndani ya Matongee Club jijini Arusha.

Picha Zote Na Nassir

July 8, 2010

HISPANIA YAINGAMIZA UJERUMANI 1-0

Fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini itakuwa kati ya Hispania na Uholanzi.
Mpambano huo wa kihistoria umetokana na Hispania kuishinda Ujerumani bao 1-0 katika uwanja wa Moses Mabhida mjini Durban na kufuzu fainali kwa mara ya kwanza katika historia.
Bao pekee la mechi hiyo lilifungwa kwa kichwa na mlinzi Carles Puyol katika dakika ya 73, alipopanda mbele kucheza mpira wa kona.
Ujerumani walionekana kikosi tofauti kabisa na timu ambayo iliiondoa England kwa kuifunga mabao 4-1 na baadaye kuitandika Argentina mabao 4-0 kwenye mechi ya robo fainali.

Uchochoro

Pengo la mshambuliaji Thomas Muller ambaye alikuwa nje kutokana na adhabu ya kadi mbili za njano lilikuwa wazi kabisa kwenye safu ya ushambuliaji ya Ujerumani.
Muller ambaye ameshafunga mabao manne kwenye Kombe la Dunia alipata kadi ya pili ya njano kwenye mechi kati ya Ujerumani na Argentina, na bila yeye, kocha Joachim Loew alikosa kabisa mbinu za ushambuliaji kwa timu ya Ujerumani.
Hispania walidhibiti mchezo katika muda wote, na wangeweza kufunga mabao mengi zaidi lakini umaliziaji ukawa mbaya, pamoja na mlinda lango wa Ujerumani, Manuel Nuer kuokoa mipira kadhaa.
Fainali ya siku ya Jumapili kati ya Hispania na Uholanzi katika uwanja wa Soccer City mjini Johannesburg itawakutanisha wafungaji wanaaongoza kwa sasa; Wesley Snijder na David Villa.
Ni mara ya kwanza kwa Hispania kucheza fainali ya Kombe la Dunia, na kwa upande wa Uholanzi itakuwa mara ya tatu, ingawa bado hawajapata kushinda Kombe hilo.
Mechi ya kutafuta mshindi wa tatu na wanne itachezwa Jumamosi kati ya Uruguay na Ujerumani.

July 7, 2010

GHANA YAITAKA FIFA KUBADILISHA SHERIA





Waziri wa michezo wa Ghana amesema shirikisho la soka duniani FIFA linatakiwa kubadilisha sheria za mchezo wa soka kufuatia kuondolewa kwa Ghana kwenye robo fainali ya Kombe la Dunia baada ya kutumika mikono.
Waziri huyo Akua Sena Dansua hajasema ni sheria zipi angetaka zibadilishwe, lakini watu wengi wamekuwa wakisema mwamuzi wa mchuano wa robo fainali kati ya Ghana na Uruguay angetakiwa kuipa Ghana goli, wakati mchezaji wa Uruguay Luis Suarez alipoondosha kwa mikono mpira uliokuwa unaingia kwenye lango la timu yake.
Kwenye mechi hiyo mshambuliaji wa Ghana Dominic Adiyah alipiga mpira kwa kichwa ukaeleka kuingia katika lango la Uruguay ukibakia muda mfupi sana kabla ya mechi kumalizika, lakini Suarez ambaye ni mchezaji wa ndani akauondosha kwa mikono.
Mwamuzi alimwonyesha kadi nyekundu Suarez na akawapa Ghana penati ambayo Asamoah Gyan alipiga nje.
Adhabu hiyo ni kulingana na sheria zilizopo za shirikisho la soka dunia FIFA.
Mechi ilimalizika kwa sare, ikalazimika kuingia mikwaju ya penalti na Uruguay wakaibuka washindi wa mabao 4-2.
Ghana ilikuwa timu ya Afrika kufikia hatua ya robo fainali katika Kombe la Dunia.
Baada ya kurejea nyumbani Black Stars walipokelewa kwa shangwe na nderemo mjini Accra.
Rais wa Ghana John Atta Mills alisema wachezaji hao watapewa tuzo za kitaifa na pia dola 20,000 kila mmoja.
Mashabiki wa soka kote barani Afrika waliishabikia Ghana wakati wa mchuano huo, na wengi walipigika sana baada ya Black Stars kuondolewa.
Ilikuwa ni timu pekee ya Afrika iliyobakia kwenye mashindano baada ya timu zingine tano za Afrika kuondolewa kwenye raundi ya kwanza ya michuano hiyo.

JIACHIE NA KAMERA YA DJ NASS


Katika Jiachie na camera ya Dj Nass hawa hapa ni washakaji wa kitaa nao waliamua kujiachia namna hiyo.

ARUSHA BARABARA HAKUNA


Kadri siku zinavyokwenda Mkoa wa Arusha unakabiliwa na ukosefu wa barabara hilo limebainika hasa pale inapofika mida ya Asubuhi na Jioni kunakuwepo na msongamano mkubwa sana wa magari.