April 5, 2012

MAHAKAMA YATENGUA USHINDI WA GODBLESS LEMA JIMBO LA ARUSHA MJINI

Aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema katikati  akihutubia umati wa wafuasi wa chama hicho waliokuwa wamefurika mahakamani  kusikiliza shauri la kupinga ubunge wake, ambapo mahakama imeutengua ikidai Lema alikiuka sheria za uchaguzi na kuamuru uchaguzi urudiwe.

Lema akiwatia moyo wafuasi wa chadema katika eneo la mahakama baada ya kupokea matokeo ya kutengua ubunge wake leo, huku akieleza kuwa hata kata rufaa ila anasubiri tume ya uchaguzi itangaze rasmi kuanza kwa uchaguzi katika jimbo la Arusha Mjini.

Askari polisi wakiwa eneo la mahakama wakiimarisha ulinzi muda mfupi baada ya mahakama kutengua ubunge wa mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kutoka Chadema.

Polisi wakiimarisha ulinzi mahakamani hapo. 

PICHA NA NASS -DNB- ARUSHA

No comments:

Post a Comment